Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
JPM ndio alifuta leseni yao kibabe, yeye kama alikua Indiana Resources wameshindwa honor mkataba angefungua kesi ICSID ili mkataba uvunjwe cha ajabu anaenda tu kubadili sheria hapo hapo na kuamuru zitumike kurudi nyuma!!Nadhani ni bora kushughulika na kiini cha hizi kesi kuliko matokeo ya hizi kesi .Mfano tushugjulike na watu wanaojicommit au kuingia mikataba isiyo na afya kwa Taifa .Ni ngumu sana kwa wakili anae lipwa milioni kwenda kushinda kesi ya billions .
Mama yenu anaupiga mwingi.Yaani Bilioni 300 ambazo ni sawa na pesa ya kujenga km 250 za Lami tunaenda kuwalipa Matapeli wa Indiana Resources ambao Wanashulikiana na Mafisadi wa Serikalini.
Daa inauma Sana aisee
---
Mapendekezo au hoja mbili kati ya tatu ilizowasilishwa na Tanzania kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) yamepigwa chini.
Serikali iliwasilisha hoja hizo baada ya ICSID, Julai 2023 kutoa hukumu, hivyo walitaka Mahakama hiyo kufuta hukumu inayoelekeza kulipa fidia ya Dola 109 milioni za Marekani (Sh272 bilioni) kampuni ya Indiana Resources (IDA).
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya ICSID hela hiyo imefikia Dola za Marekani 112.9 milioni (Sh282 bilioni) pamoja na gharama za ziada za Dola 4.2 milioni (Sh10.5 bilioni) ambayo ni jumla ya zaidi ya Sh292 bilioni.
Kwa mujibu wa hukumu hiyo riba ya Dola za Marekani milioni moja (Sh2.5 bilioni) itaongezeka kila mwezi hadi Tanzania itakapolipa kiasi hicho au Indiana itakapozuia mali ya Tanzania itakayoendana na thamani ya madai hayo.
Desemba 2023, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania alitoa barua ya uthibitisho kwa ICSID kwamba Tanzania ingelipa bila masharti na bila kubatilishwa kiasi chote cha fedha hiyo ndani ya siku 45 baada ya uamuzi wa mwisho wa kubatilisha. Hata hiyo ni takribani miezi miwili sasa tangu hilo litokee.
Mapitio ya Tanzania kubatilisha kesi yatafanywa Machi 15, 2024 na wadai kujibu Aprili 26, 2024. Kisha kila upande utakuwa na majibu yao mtawalia.
Mei 24, 2024 na Juni 21, 2024 kutakuwa na mkutano wa pamoja wa wiki tatu kabla ya tarehe ya mwisho ya maamuzi.
Mwananchi
Mkuu hapo sina clue ya idadi ya cases.Kesi ambazo serikali imewahi kuwa nazo, labda tuanzie awamu ya pili mpaka sasa, kuna ambazo serikali imewahi kushinda?
- Na zile ilizoshindwa, kuna lolote lilifanyika kuzuia kesi kama hizo zisitokee tena?
- Kama kuna ukanjanja uliosababisha kuwa kesi, kutokea serikalini, hao makanjanja waliotusababishia hayo, wako wapi? Ni kina nani? Nini kimefanyika dhidi yao?
Zile kesi tulizoshinda, kuna lolote tumejifunza? Nimesikia Accacia waliilipa serikali tsh 900bn, je ni kweli?
- Kesi zilizofufuliwa awamu hii, zinaendana na matatizo ya kutengeneza kama umeme, inflation etc
- Kwa mujibu wa Mpina, serikali inapaswa kuanza kulipwa fidia kwa mujibu wa mkataba kutokana na ucheleweshwaji wa bwawa la Nyerere, nini kinaendelea?
Kesi za awamu ya 5 ni zipi na status zake zikoje?
Inasaidia nini sasa katika hili?!Ndo maana tunahitaji Katiba mpyaa Majambazi yafufurushwe....
Msemo umetimia.Shamba la bibi Tanzania
Msemo umetimia.
Awamu hii yupo bibi watu wanajipigia tu mihela.
Nimesoma vibaya au macho yangu umesema Jimama?Makonda yuko Njombe huko akiwahadaa watu kuwa anatatua matatizo huku matatizo ya yakimtatua jimama lake huku
Wewe malaya wa Lumumba Etwege umeipata hii ya MIGA?
Huyo mwendawazimu Jiwe alikurupuka kufanya maamuzi kama mtu anayeogea nje leo kodi zetu zinapotea kijinga kisa wanasiasa wajinga wajinga
Shabhashhhh!
Duu jamaa alibrain wash ngumbaru kijiji!Etwege hawezi kutia pua kwenye hili, maana yeye ni mmoja wa waliotekwa na uzalendo uchwara wa dhalimu Magu.
Waliotaka kumuua Lissu wanaendelea kuoza..hayo makesi na mafaini yamesababishwa na ujuaji wa Magufuli, Kabudi, na Kilangi.
..Lissu alionya bungeni kuhusu suala hili lakini akawa anabezwa ati ni mwanasheria wa hovyo anayeogopa kushtakiwa.
..Zaidi kwasababu ya kupaza sauti watawala wakajaribu kumuua.
..Ukweli unabaki kwamba hii ni hasara ambayo imetokana na kiburi cha watawala wetu.
Etwege hawezi kutia pua kwenye hili, maana yeye ni mmoja wa waliotekwa na uzalendo uchwara wa dhalimu Magu.