Wanasheria wa Serikali Wakwama Mahakama ya Kimataifa. Bilioni 300 Kuchotwa

Yaani Bilioni 300 ambazo ni sawa na pesa ya kujenga km 250 za Lami tunaenda kuwalipa Matapeli wa Indiana Resources ambao Wanashulikiana na Mafisadi wa Serikalini.

Daa inauma Sana aisee
---

Mapendekezo au hoja mbili kati ya tatu ilizowasilishwa na Tanzania kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) yamepigwa chini.

Serikali iliwasilisha hoja hizo baada ya ICSID, Julai 2023 kutoa hukumu, hivyo walitaka Mahakama hiyo kufuta hukumu inayoelekeza kulipa fidia ya Dola 109 milioni za Marekani (Sh272 bilioni) kampuni ya Indiana Resources (IDA).

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya ICSID hela hiyo imefikia Dola za Marekani 112.9 milioni (Sh282 bilioni) pamoja na gharama za ziada za Dola 4.2 milioni (Sh10.5 bilioni) ambayo ni jumla ya zaidi ya Sh292 bilioni.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo riba ya Dola za Marekani milioni moja (Sh2.5 bilioni) itaongezeka kila mwezi hadi Tanzania itakapolipa kiasi hicho au Indiana itakapozuia mali ya Tanzania itakayoendana na thamani ya madai hayo.

Desemba 2023, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania alitoa barua ya uthibitisho kwa ICSID kwamba Tanzania ingelipa bila masharti na bila kubatilishwa kiasi chote cha fedha hiyo ndani ya siku 45 baada ya uamuzi wa mwisho wa kubatilisha. Hata hiyo ni takribani miezi miwili sasa tangu hilo litokee.

Mapitio ya Tanzania kubatilisha kesi yatafanywa Machi 15, 2024 na wadai kujibu Aprili 26, 2024. Kisha kila upande utakuwa na majibu yao mtawalia.

Mei 24, 2024 na Juni 21, 2024 kutakuwa na mkutano wa pamoja wa wiki tatu kabla ya tarehe ya mwisho ya maamuzi.

Mwananchi
Kwa mwanasheria mkuu aliyepo sasa hivi kwenye serikali hii ni kizungumkuti maana yeye ni kubambika kesi kwa wananchi wanaohoji kuhusu masuala mbalimbali yenye maslahi ya taifa.

Ni bora ang'olewe awekwe mwingine ambaye hawezi kuwa 'compromised'
 
..ktk hili suala sio Mwanasheria Mkuu kuwa "compromised."

..labda tuseme Mwanasheria Mkuu kuwa "compromised" kwa kushindwa kumshauri Rais [magufuli]asifanye maamuzi ya kibabe, yatayoitia nchi hasara.

..Magufuli aliwahi kusababisha hasara ya sh bilioni 15 baada ya mahakama kuu Mwanza kutoa hukumu kwamba alivunja kituo cha mafuta bila kufuata sheria na kwa kukiuka ushauri aliopewa.

..Kwa maoni yangu tatizo lilikuwa ni Magufuli na tabia zake za kibabe.
 
Hata huyu aliyepo sasa hivi kuna madudu na rais atakayekuja atakuja kupindua meza kurejesha maslahi ya nchi sio wenye uwezo wa kipesa na watakaoathirika kutokana na maamuzi hayo kwa manufaa ya nchi watafungua kesi nao kwa kushauriwa na wanasheria hawa hawa kwamba fanyeni hivi ili mlipwe kwa hiyo sio sawa kumlaumu hayati JPM
 
..unatakiwa kupindua meza kwa kutumia akili sio kukurupuka.

..Magufuli alikuwa tatizo tangu akiwa Waziri wa ujenzi.

..kuna kesi ya kuvunja kituo cha mafuta Mwanza hasara yake bil 15.

..kuna kesi ya kuvunja mkataba wa ujenzi kibabe iliyopelekea ndege yetu bombardier kukamatwa Canada.

..Kuna jamaa amewahi kuandika hapa JF kwamba mikataba yote ya madini aliyoikuta Magufuli ilikuwa na kipengele cha kuijadili upya baada ya kipindi fulani.

..Kama madai hayo ni ya kweli basi kulikuwa hakuna ulazima wa Magufuli kufanya vurugu alizofanya.
 
Alikuwa na uthubutu kukataa ujinga kwa ajili ya wananchi kwa gharama zozote zitakazojitokeza. Kama kulipa lipeni kwa sababu ya viongozi wasio wazalendo walilitumbukiza taifa kwenye mikataaba yenye nia OVU na kwa faida ya watu wachache hasa baadhi ya viongozi wasio waaminifu.
 
..kiongozi anaposema kwa "gharama zozote" inabidi zitoke mfukoni kwake, na sio zitokane na kodi za wananchi.
 
.. Etwege na genge lake walikuwa wanashangilia eti hatujashtakiwa miga!!

Mjinga huyo dogo, yaani kwa kuivaa kichwa kichwa mikataba ya hatari vile tungeachwa? Au alidhani hayo makampuni ya kimataifa yangemuogopa yule mlevi wa madaraka?
 
Waliotuingiza kwenye hasara kama hi inatakiwa washtakiwe huu ni upuuzi hiyo pesa tunalipa sisi wananchi.
Hapa ndipo tatizo la siasa zetu lilipo. Hakuna atakayekubali jina lake kutajwa kuwa alihusika na kuandaa mkataba uliozaa janga hili. Hasa alieweka sahihi kuidhinisha jambo hilo angetolewa hadharani tukamfahamu au tukawafahamu.
 
..wanasheria wa bongo hawajasajiliwa kutetea kesi ktk hizo mahakama.

..kesi ikishakwenda nje Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Tz anatafuta mawakili wa kututetea ktk mahakama za nchi ambako kesi inaendeshwa.

..baada ya hapo kunakuwa na mpambano baina ya mawakili wetu na mawakili wa waliotushtaki.

..tusilaumu wanasheria wetu ktk hili. Kilichotuponza ni kuvunja mikataba bila kufuata utaratibu.
Hapa kuna shida, unajiuliza nchi nzima inaingia mkataba bila ufahamu wa namna ya kuusitisha?
 
Mkuu hapo sina clue ya idadi ya cases.
Nitachangia issue ya Mr. Mpina na ulipwaji kama ifuatavyo; Mikataba yai ujenzi huwa ina kipengere cha adhabu kwa ucheleweshwaji wa either malipo ama ucheleweshaji wa kumalizika kwa mradi. Hayo yote ili yatokee kuna sababu zinakuwa zimeainishwa kwenye mkataba. Ikitokea mteja/serikali ikachelewesha malipo basi itaadhibiwa kwa mujibu wa mkataba na huo ucheleweshaji wa malipo uta affect maendeleo ya kazi (muda wa kumaliza mradi) ma serikali haitokuwa entitled kulipwa kwa kuchelewa kumalizika kwa mradi kwani yenyewe ndiyo imesababisha delay.
Kuna obligation pia za kila pande kwenye mkataba na usipotimiza ya kwako inakuondolea entitlement ya fidia.
Vile vile kuna sababu ambazo ziko nje ya uwezo wa pande za mkataba na uwepo wake u affect muda wa mradi( eg. Shutdown ya Corona)
Kifupi fidia siyo an automatic button kuna test lazima i qualify
Hapa nikitamka kwamba kwa hali ilipofikia haitakuwa sahihi mzigo huu kwa kuanzia akabebeshwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali? La sivyo tuonyeshwe aliishauri nini serikali. Kama ushauri alitoa kupinga swala hilo na serikali haikuzingatia ushauri huo, kwanini basi hakujiuzulu?
 
Alikuwa na uthubutu kukataa ujinga kwa ajili ya wananchi kwa gharama zozote zitakazojitokeza. Kama kulipa lipeni kwa sababu ya viongozi wasio wazalendo walilitumbukiza taifa kwenye mikataaba yenye nia OVU na kwa faida ya watu wachache hasa baadhi ya viongozi wasio waaminifu.
Uthubutu ni sahihi lakini ingetakiwa kuwepo mchakato wa kuhakikisha kuwa maamuzi yanafanyika kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
 
Kavipi kizimkaz apewe mwalabu afu io ela tukalipe ao machalii wa IDA
 
Hapa kuna shida, unajiuliza nchi nzima inaingia mkataba bila ufahamu wa namna ya kuusitisha?

..umesahau kwamba Rais wa Tz ni mungu-mtu?

..mtu akishakuwa Rais wa Tz mara moja anatunukiwa PhD na anakuwa na maarifa ktk kila jambo kuliko raia wote.
 
Yaani Bilioni 300 ambazo ni sawa na pesa ya kujenga km 250 za Lami tunaenda kuwalipa Matapeli wa Indiana Resources ambao Wanashulikiana na Mafisadi wa Serikalini.

Daa inauma Sana aisee
---

Mapendekezo au hoja mbili kati ya tatu ilizowasilishwa na Tanzania kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) yamepigwa chini.

Serikali iliwasilisha hoja hizo baada ya ICSID, Julai 2023 kutoa hukumu, hivyo walitaka Mahakama hiyo kufuta hukumu inayoelekeza kulipa fidia ya Dola 109 milioni za Marekani (Sh272 bilioni) kampuni ya Indiana Resources (IDA).

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya ICSID hela hiyo imefikia Dola za Marekani 112.9 milioni (Sh282 bilioni) pamoja na gharama za ziada za Dola 4.2 milioni (Sh10.5 bilioni) ambayo ni jumla ya zaidi ya Sh292 bilioni.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo riba ya Dola za Marekani milioni moja (Sh2.5 bilioni) itaongezeka kila mwezi hadi Tanzania itakapolipa kiasi hicho au Indiana itakapozuia mali ya Tanzania itakayoendana na thamani ya madai hayo.

Desemba 2023, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania alitoa barua ya uthibitisho kwa ICSID kwamba Tanzania ingelipa bila masharti na bila kubatilishwa kiasi chote cha fedha hiyo ndani ya siku 45 baada ya uamuzi wa mwisho wa kubatilisha. Hata hiyo ni takribani miezi miwili sasa tangu hilo litokee.

Mapitio ya Tanzania kubatilisha kesi yatafanywa Machi 15, 2024 na wadai kujibu Aprili 26, 2024. Kisha kila upande utakuwa na majibu yao mtawalia.

Mei 24, 2024 na Juni 21, 2024 kutakuwa na mkutano wa pamoja wa wiki tatu kabla ya tarehe ya mwisho ya maamuzi.

Mwananchi
Mifumo ya mahakama ya kiupendeleo inawafanya mawakili wetu wasiwe vichwa. Huwa wanashinda kesi kwa maagizo ya juu. Sasa wakienda huku, vichwa chali...
 
..msimlaumu Samia ktk suala hili.

..kesi tuliyoshindwa imetokana na maamuzi ya Magufuli, akishauriwa na Prof.Kabudi, na Prof.Kilangi.
Mahakama zao

Walalamikaji wao?

What else .
 
Back
Top Bottom