PostGE2025 Wanasheria watinga ICC na kufungua kesi dhidi ya Rais Samia na wakuu wa Vyombo vya Usalama Tanzania

PostGE2025 Wanasheria watinga ICC na kufungua kesi dhidi ya Rais Samia na wakuu wa Vyombo vya Usalama Tanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Nyaraka zilizotumwa kwa mwendesha mashtaka mkuu wa ICC zinadai kuwa kati ya 2019–2025, Serikali ya Tanzania ilitekeleza uhalifu dhidi ya binadamu kama sehemu ya mpango mpana wa mashambulizi dhidi ya raia, hususan wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Zinaripoti mauaji ya raia, utekaji na kutoweshwa kwa watu, mateso, ubakaji, ukamataji holela, na matumizi ya jeshi na vikosi maalum dhidi ya waandamanaji na makundi ya raia wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025, pamoja na kuwahamisha kwa nguvu maelfu ya watu wa jamii ya Wamaasai.

Pia zinataja kuzimwa kwa intaneti kwa siku kadhaa wakati wa uchaguzi kama kitendo kibaya kilichochangia kuficha mauaji na kuzuia huduma muhimu.

Katika mlolongo wa uwajibikaji, anayetajwa kama mwenye dhamana ya juu kabisa ni Rais Samia Suluhu Hassan , akifuatiwa na viongozi wa usalama wakiwemo Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro pia anatajwa Waziri wa Mawasiliano aliyehusishwa na kuzima intaneti.

Aidha, yupo Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baadhi ya majaji pamoja na wakuu wa mikoa, polisi na vikosi maalum ambao ni watekelezaji wa moja kwa moja wa ukamataji, mateso na mauaji.

Pia soma> Kwa huu ushahidi uliowekwa na CNN, Samia, DGIS, CDF na IGP tukutane ICC
 

Attachments

Taarifa za chinichini zinapenya kwamba mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) inaandaa hati ya mashtaka dhidi ya serikali ya Tanzania kufuatia mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia yaliyotekelezwa kati ya tarehe 29 Oktoba na tarehe 5 Novemba, 2025 ambapo inakadiriwa kwamba zaidi ya raia 10,000, wengi wao wakiwa vijana (Gen Z), waliuawa kwa risasi za moto hadharani.

Hatua hii inakuja baada ya vyombo mbali mbali vinavyotetea haki za raia vya ndani na nje ya nchi kutoa wito kwa ICC kuifungulia mashtaka serikali ya Tanzania dhidi ya uhalifu wa kibinadamu. Aidha, imekuwa rahisi kwa ICC kuifungulia serikali ya Rais Samia kesi kufuatia kuzagaa kwa video na picha za zilizothibitshwa kisayansi ambazo zitatumika kama ushahidi mahakamani. Kwa ICC, hakuna ushahidi mdogo. Hata ushahidi wa kikosi cha watu waliofanya mauaji kilichotoka Zanzibar kikiwa kimevalia nguo za kiraia kilichoonekana kikiwapiga risasi raia mitaani, ni ushahidi usioweza kuacha shaka yoyote.

Na pia wanajeshi kutoka Uganda (UPDF) wanaosemekana kuja kuwasaidia polisi kuwaua watanzania ni ushahidi tosha kuwa serikali ilikuwa imedhamiria kutoa roho za raia.

MAONI YANGU
Mimi nafikiri ni sahihi kabisa kwa ICC kuifungulia mashataka serikali ya Tanzania kwa ushahidi walioukusanya hadi sasa. Kama serikali haina hatia katika hili, basi watashinda kesi misa ya kwanza na ICC watalipa gharama zote za kesi. Lakini ikiwa serikali itaonekana kuwa ilihusika kuwaagiza na kuwawezesha polisi na UPDF kuua maelfu ya raia, sheria ichukue mkondo wake. Sheria ni msumeno na haina huruma kwa wauaji. Mungu ibariki Tanganyika, Mungu wabariki watanganyika. Amen.
​
 
Huyu mama kaongoza kwa kuua watu miongoni mwa kesi zote zilizowahi kuendeshwa Icc.👇
Baada ya kimbari ya Rwanda, inafuata kimbari ya samia!👇
1000040505.jpg
 
Nimeona dossier ya kurasa 83 mashtaka ya mama na washirika wake kule ICC. Mungu awarehemu ndugu zetu watanzania waliouawa bila hatia. Uhai wa mtu ni kitu kikubwa sana, Ukiua mtu mmoja na wewe tunajua adhabu yako ni nini........Huyu ameua watu 23,000 inaweza ikawa zaidi. Kila mahali wameua watu wengi.
Nachosema, Mungu wetu ni mwema. Huyu mama na washirika wake siku yao imefika.
 
Nimeona dossier ya kurasa 83 mashtaka ya mama na washirika wake kule ICC. Mungu awarehemu ndugu zetu watanzania waliouawa bila hatia. Uhai wa mtu ni kitu kikubwa sana, Ukiua mtu mmoja na wewe tunajua adhabu yako ni nini........Huyu ameua watu 23,000 inaweza ikawa zaidi. Kila mahali wameua watu wengi.
Nachosema, Mungu wetu ni mwema. Huyu mama na washirika wake siku yao imefika.
Hivi huku yake ikoje?
 
Back
Top Bottom