Pre GE2025 Wanasiasa wenye msimamo mkali wanakaribia Kushinda, Kuongoza CHADEMA kuelekea 2025?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Fortilo

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
5,807
Reaction score
17,416
Harakati ndani ya Chadema zinachangamka siku hadi siku..

CCM wamepuuza siasa za majadiliano na maridhiano ndani ya CDM na nje ya CDM..

Sio ACT wala vyama vidogo kwamba vinapatiwa ahueni...

Upande wa Chadema shida inaonekana Freeman Mbowe amekuwa mpole sana kwa dola hadi kufika kipindi anaambiwa amepewa Rushwa ..

Na hili limetokana na maridhiano ya Mbowe na Dola ambayo hayajazaa matunda yeyote...

Wahafidhina wanasema lazima Mbowe aachie Ngazi kwakuwa Chama hakiwezi kuendeshwa kwa siasa zile zile za miaka takribani kumi iliyopita...

Kwa sasa CDM ina mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa, wachache zaid toka uchaguzi wa 2005...

Sababu za wahafidhina ni kwamba Mbowe amekuwa mpole sana kwa Dola na CDM kimekuwa chama cha majadiliano... "Wanataka mabadiliko"

Hatari ninayoiyona, wanaoongoza mapambano hayo hawana cha kupoteza, wakiongozwa na wafuatao..

1. Tundu Lissu
2. Petet Msigwa
3. Liberatus Mwangombe
4. Lyenda
5. John Jambo Media
6. John Heche
7. Saed Kubenea
8. Rose Mayemba
9. Wilbroad Slaa
10. Rose Mwakitwange
11. Lifeof Mshamba etc

Pamoja na kundi hili la wazi, bado kuna wanachama wengi wanadhani Mbowe ni kikwazo kwao kufanya harakati za kuhakikisha hawaendi kwenye uchaguzi mkuu hali ikiwa kama ilivyo na wanataka 'mabadiliko' ya uongozi haraka sana.

Kwa Mtazamo wangu kutokana na niayoyaona mtandaoni ni kama wanakaribia kushinda...

Na ukitazama kwa undani ni kama hakuna mbinu mbadala ya kufanya CDM iache "kukatwa" kama ilivyokuwa 2020....

Muda utakuwa rafiki mzuri, lakini muasisi wa yote haya ni kukwama kwa Maridhiano, au angalao, minimum reforms kutokufanya kazi kama ilivyoyarajiwa...

Siasa zetu kubadilika sana kuelekea 2025, pengine kuliko tulivyotarajia?

Muda utasema.
 

Attachments

  • Screenshot_20241209-094823.png
    160.1 KB · Views: 5
Unajua ukiitazama kwa jicho la mtoto wa chekechekea CCM ,utagundua kua ni CCM ambayo Ndani yake kuna GOVERNMENT -MILITARY SYMBIOSIS.


Aina hiyo ya Uhusiano ambayo chama na jeshi vinategemeana utakubaliana namm kua UNAHITAJI SIASA ZA KIANAHARAKATI KAMA ZA LISSU, SILAA , N.K.


hizi Siasa za Akina LISSU, Huwa zinafanikiwa Kwa sababu kua Moja, HUFANIKIWA KUTEKA MIOYO YA WATU NA KUWAJAZA HASIRA .

SIASA NI SUALA LA HISIA, KAMA ULIVYO MPIRA NA MAPENZI.... MTU YUPO TAYARI KUJIUA, PALE ANAPOONA KITU HAKIPO SAWA.

Hivo Kwa Afya ya CDM , Mbowe amuachie LISSU, Nyinyi ni mashuhuda mpelampela wa LISSU ,kwenye UCHAFUZI wa 2020, mliuona.
 
Ila kwa taifa ni hatari,

Kwakuwa watu watainga road mambo yakibaki kama yalivyo.
 
Tamaa Za viongozi Na kuendekeza kuhongwa hongwa ndo vinaelekezwa Sasa kuhakikisha upinzani unagawanywa Na kuuwawa kama ya 2015 ukawa vs Chadema.

Kinachosikitisha Sana Ni, sijuhi kwanini kila uchao Hawa watu hawaelevuki. Yaani kila siku wanategwa mtego ule ule Na kila siku wananasa, Kuna Mda unajiuliza Sasa hata kama walienda shule walisoma ili kuwasaidie Nini kama kitu kidogo kama hiki kinawapa Shida kuking'amua.

Japo tunajua pia, maagizo ya ndani Ni lazima mtu apewe Na akubali kuchukua mpunga ili akaharibu nyumba kubwa aendelee kuwa madarakani ama la Maisha yako Na wanao Kwa miaka uliyoishi inatosha. Ukishikiwa kisu Shingoni huna namna vinginevyo futi 7 hii hapa. ..Afrika Ni taabu Sana.
 
Mkuu siasa ilipoanza kuwa na mahela utitiri ndio mambo yalibadilika sana..

Watu wanaingia kwenye siasa kwa minajili ya kupata kipato na ajira na sio kiu ya kutawala kwenye mfumo mpya..

No wonder wengi walikimbia upinzani wakaelekea jikoni kupata mapesa ya "bure"

Sio upinzani tu, ni takribani kote CCM halikadhalika...

Tusipokuwa makini upinzani pia utakufa tutabaki tunatoleana macho hapo hapo jikoni..... Na kila kitu kitabaki kama kilivyo au kubaya zaidi...

Tusisahau pia kwamba upinzani wa "kweli" ni mateso na mchezo hatari sana.
 
Mbowe apumzike tunataka amsha amsha
Labda tuwasaidie, hao wote mlionao hayupo wa afadhari. Mngekuwa Na plan mlihitaji kuunda timu nzuri Mpya Mapema Sana lakini kuendelea kuwafikiria Mbowe Na Lisu wake mnapoteza tu wakati kama si kufanya ilmradi liende, maandalizi ya hovyo yanazaa vitu hovyo pia
 
Tatizo wanafadhiliwa na shirika la ujasusi la Marekani na Uingereza, kila mara wanamuita Lissu Ubelgiji kufanya naye vikao vya siri na kumpa mamilioni ya dola ili asababishe machafuko.

Cha kutanya ni kama alivyofanya Mugabe kwa Moses Tsvangirai, mpaka leo nchi iko chini ya wazalendo waliopigania uhuru
 
magufuli na bashite walijaribu kufanya wakashindwa Mungu yupo
 
Hii habari ni ya kutunga na haina ukweli wowote. KlMch. Peter Msigwa na Saed (Sio Kocha wa Yanga) Kubenea wapi na wapi Chadema?
Hata mimi sikuelewa alipotajwa msigwa.
Ila Mbowe ndo roho ya CDM mana ni Mwenyekiti Mfadhiri.
CDM haiwez kufanya ukombozi kwa kuwa na viongozi maskin kias hiki. (Maskin hana kiapo)
Siasa ni uwekezaji.
Kwa sasa siasa za kiuhanaharakati kama atakavyo Lisu na Mwabukus sharti watu muhimu wawe nje ya nchi wakiratibu.
Kila muumini wa ukweli anakiri mabadiriko bila nguvu na hata umwagaji damu ni haiwezekan tena.
Chama dola kinamaanisha linapokuja suala la kuendelea kushika hatamu.
Isitoshe kina mtaji mzuri wa waumini na nyenzo.
Wasomi wazuri na wabaya wako CCM.
Kumbuka the majority are always not right
Kiuhalisia watanzania wenyewe wamegawanyika, kiwango cha woga, hofu na ujinga binafs kiko juu!
Wanaosubiri haki kwenye silver plate watasubiri vizazi 4.
Kwa udhoofu uliopo ni heri sala na dua ielekezwe zaid aliyeko madarakan ajifanyie renaissance for good
 
Propaganda

Lissu ndiye kiongozi pekee aliyebaki Hana makando kando chadema

Weka na Heche

Chama kikienda na Hawa nakuhakikishia 2025 tutagawana mbao!!
 
Siasa sio pesa tu ingekuwa pesa Lowassa angekuwa Rais wa Tanzania

Mkapa, Mwinyi na Magufuli wasingekuwa Marais

Siasa ni sayansi

Umeona uchaguzi wa Marekani

Trump katumia 350 us dollars na Kamala Katumia dollar bilion 1 lakini Trump kashinda !!

Pesa sio kila kitu kwenye siasa sema hapa kwetu CCM wanafanya wanavyotaka sababu ya Watanzania wamelala pono!!
 
Ni vema kukawa na mabadiliko ya mwenyekiti.Miaka 20 ni kipindi cha kutosha.Mbowe kaifanyia mengi mazuri sana Chadema.
Sasa Chama kipate uongozi mpya Mbowe akiwa bado mshauri wake.
 
Naunga mkono hoja.
Nashangaa Mama anaamini pesa za waarabu zitamvusha 2025.
 
Ndani ya CDM bado hawaaminiani kihusu kuachia madaraka hasa nafasi ya juu ya mwenyekiti. Halafu wanataka demokrasia ya nchi. Kituko hiki. Tungekua na watu makini wa kuhoji demokrasia Chadema wasingekua chama cha siasa hadi sasa hivi.πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…