Wanaume: Kosa dogo linaweza kutufanya tusipendwe na watoto wetu hapo baadaye. Mwanangu wa miaka mitano amenistua leo

Sasa mbona umejijibu? Asingekuwa na hela angemuoa pisi kali Jack? [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Jack ni pisi kali yule mzee?? Kashafumuliwa na wahuni wa mjini mpaka akakosa soko akajibanza kwa wazee wa mvi kwenye pufumbu?? Yule alienda kimaslahi sio kukidhi kile Dr Mengi alichosusiwa na familia.
 
Habari za Ijumaa wikenda wapenzi wasomaji wa MMU.

Kwanza napenda nitoe maelezo kuhusu tabia yangu ya kimaisha.

Declaration; Mimi nimeoa mke wangu Mama wa nyumbani. Nimefanya hivi kwa kuwa napenda sana starehe. Yaani napenda ninaporudi nyumbani
Nimechokaaaa eti 'nikirudi nyumbani nyumba safi amanipikia sijui napenda starehe etc'
Bro maisha ya wawili wapendao ni two way street
Pesa sio kila kitu
Mwanamke naye Mungu alimpa uwezo wa kufikiri kutenda na kuwajibika
Mwanamke sio chombo cha matumizi eti mie mtafutaji naleta pesa nafanya hivi na vile
Na huyu aliyebeba miezi tisa akazaa kwa uchungu sio mtafutaji au utafutaji ni pesa tu
Malezi ya watoto Utafutaji wa pesa kutunza nyumba sijui kupika kusafisha ni jukumu la wote wawili. Watoto hujifunza kupitia kwenu wazazi. Kazi za nyumbani hakuandikiwa Mwanamke tu ni wajibu wa kila mmoja. Ukiwa na watoto waonyeshe umuhimu wa kutafuta pesa na umuhimu wa kutunza nyumba. Leo wanaume wengi waliopoteza wenzi hawajui waanzie wapi wanaishia kuangukia kwenye mikono ya watesi wa watoto wao kwa mtindo 'come we stay'
Mtoto atakuthamini na kukuheshimu wewe kama Baba au Mama ukiwaonyesha majukumu ya kulea na kutunza familia na nyumba kwa ujumla ni la wazazi wote wawili..
 
Wewe sidhani kama una makosa mkuu maana unatafuta na kama ulivosema kuwa ukiwa free unakaa na familia Yako that's nice, shida ipo Kwa mama anapowapa zawad yoyote anatakiwa awaambie watoto imetoka Kwa baba
 
Naheshimu sana na kumpenda mama watoto wangu. Mchango wake kwangu naukubali mno. Ndio maana nampenda. Hapo tumegawana tu majukumu. Ila haimanishi yangu ni ya thamani kuliko yake. Na ndio maana nawakumbusha na wanaume wengine tubadilika mtazamo kidogo kwa manufaa ya familia zetu.
 
Wewe sidhani kama una makosa mkuu maana unatafuta na kama ulivosema kuwa ukiwa free unakaa na familia Yako that's nice, shida ipo Kwa mama anapowapa zawad yoyote anatakiwa awaambie watoto imetoka Kwa baba
Kweli na kisa la sisi wanaume wa type yetu tunachukulia mambo poa. Ambayo yanaweza kuwa na impact baadae.
 
Siku moja moja mpe mkeo pesa mbele ya watoto wako itawasaidia kujua wewe ndio unatoa hizo pesa mama aweza waambia lakini wakiona kwa macho itaweza saidia zaidi
Ni kweli kabisa.
 
Hii imekaa poa sana
 
Mkuu samahani kwa kukuambia ukweli.
"nimeharibu mahali naomba ushauri"(Rudi kwenye huu Uzi wako,then jitathmini Kama una haki ya kuchangia huku)[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
"nimeharibu mahali naomba ushauri"(Rudi kwenye huu Uzi wako,then jitathmini Kama una haki ya kuchangia huku)[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji2211][emoji2211][emoji2211]
 
Kweli hii ni mbinu moja wapo. Asante. Wanaume tujifunze
Nakubali kwamba kwa sasa ni wadogo na hawajui.Ina maana hawatokua na kuujua ukweli kwamba;
-mama huwa yupo nyumbani muda wote kulea familia hiyo?
-hawatojua kwamba mama hana kibarua kinachompa ujira?
-hawatojua kwamba fedha atumiazo mama au anazowapa wao watoto ni kutoka kwa baba?
NB:Kama hawatokua na kuyajua hayo,hao watoto ni aidha wana matatizo ya kutosoma mazingira,kuongopewa na mama yao au hawapendi kuujua ukweli tu.
HATA HIVYO:Upatapo wasaa(lazimika kuupata)jenga uhusiano mwema na watoto/familia yako.
 
Umemaliza...
 
ni rahisi sana kwa babakumfool mtoto mdogo ili ampende pengine kuzid hata mama yake mfano kwenye huo mfano kwani glori hiyo ni sh ngapi ?? hata kama hutaki **** hela basi kanunue mwenyewe pamoja na hayo maputo umletee mfano mimi niliokua mdogo baba yangu mzazi hakua na kazi mama ndo alikua anafanya kazi ila mzee alikua akija pale home ni vurugu mzee akipata shilingi mia huko au akipewa na mama ataleta pale vitoy ya kuchezea sijui ice cream jumapili kama yupo home anatuchukua anatupeleka mahala tunakunywa soda nini ilifikia wakati kwamba tukawa tunaona bila baba maisha hayaendi kumbeni style tuu alikua anatumia kutuonesha kulea mtoto kama sio rocket science hata kama ungekua wewe mzee wako hayuko karibu lazima umuone kama anazingua
 
Jack ni pisi kali yule mzee?? Kashafumuliwa na wahuni wa mjini mpaka akakosa soko akajibanza kwa wazee wa mvi kwenye pufumbu?? Yule alienda kimaslahi sio kukidhi kile Dr Mengi alichosusiwa na familia.
Bado hoja ni nyepesi mno, sasa hata akienda kimaslahi kwani naye si lazima afanye Dr. Mengi alichohitaji ili apate hayo maslahi? Napo pia huelewi bado? Issue ni hela, hata kama alikwenda kuchuma sio big deal, the deal is, alifanya alichotaka kufanyiwa Mengi ili apate pesa, hakuna cha bure ujue!
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…