Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukizeeka na una mahela yako fresh tu. Tafuta hela, kwani hakuna ambaye atakuona tajiri akakususa.Habari za Ijumaa wikenda wapenzi wasomaji wa MMU.
Kwanza napenda nitoe maelezo kuhusu tabia yangu ya kimaisha.
Declaration; Mimi nimeoa mke wangu Mama wa nyumbani. Nimefanya hivi kwa kuwa napenda sana starehe. Yaani napenda ninaporudi nyumbani nikute nyumba imesafishwa, inang'aa, chakula kimeandaliwa cha kifalme. Chumba ninacholala kimewekwa maridadi kama vile Mwana wa Mfalme Mohamed Bin Salma wa Saudia anaingia leo. Hivyo kwa tabia zangu hizi na zile zingine za kiutu uzima ambazo sote tunazifahamu nilipendelea sana niwe na mke asiyechoshwa sana na mihangaiko ya hapa na pale. Napenda kuona watoto wasafi muda wote walishwe vizuri na kumwagiwa upendo na mama yao muda wote.
Baada ya maamuzi yangu haya mimi nikajipa wajibu 100% kutafuta pesa, kuwaza vitu vikubwa kama vile kusaka madaraka kwa kuchukua nchi kikatiba na kidemokrasia na amani, kumiliki njia kuu na miundo mikubwa ya kiuchumi, kununua magari, ndege na kwenda masoko makubwa ya kibiashara kama Tokyo, Yokohama, Gwanzhou na Shenghanz n.k
Hakuna hata siku moja utanikuta nanunua fenicha za ndani, vyombo, nguo wala vifaa vya umeme. Hata Ada hata siku moja sijawahi kwenda shule za watoto wangu. Nyumba na viwanja sijawahi kutafuta. Kuanzia hatua ya ununuzi, ujenzi hadi kukamilika kwake yote anasimamia Mama watoto. Kazi yangu ni kukamilisha michakato ya hatimiliki na taratibu zingine za kiserikali na kisheria.
Nguo za watoto hata namba za viatu sizijui.
Ofcourse nikitoka kazini au safarini natumia muda mwingi kukaa na wanangu na mke wangu.
Baada ya kueleza tabia hizi ambazo japo sio mbaya lakini zinaweza kunicost. Nimeelezea ili wale wenye tabia kama zangu tushtuke. Tubadilike for good reason.
Leo baada ya kutoka kazini nimeshaoga na kula chakula kizuri sasa niko na pitia habari za hapa na pale kwenye account mbali mbali( Tundu Lissu account). Of course he is my role model. Tuache siasa.
Mwanangu huyu wa kiume miaka 5 akanijia nilipo. Akaniambia Baba naomba hela nikanunue glori( ball za kuchezea watoto). Nikamjibu sina pesa. Nakwepa kumpa pesa kila wakati asije kuwa na tabia mbaya.
Akanijibu Wewe Baba hujanipa pesa siku nyingi naomba leo pesa sh miatano nikanunue glori na bofu(maputo ).
Akaendelea kulalamika kuwa Mama ananipa pesa lakini wewe nikikuomba hunipi.
Likanijia wazo kichwani palepale. Nikawaza nikatafakari. Inamaana huyu mtoto anaona kabisa mimi simjali? Hajui hata hizo miatano anazopewa na Mama zinatoka kwangu??
Inamaana kuna siku nikizeeka nikawa sina nguvu hawa watoto watampenda mama yao na kuniacha mimi kwa kuamini kuwa sikuwa nawathamini enzi za ujana wangu?. Sasa itakuwaje? nitajiteteaje niaminike.
Ndipo nikasogea pembeni kwenye droo nikachukua sarafu ya jero nikampa akashukuru akatoka nje kwenda kucheza na watoto wenziwe.
Ni hayo tu.
Wanaume wakati tunawaza mambo makubwa kama kushika nchi, kumiliki viwanda vya Uraniam na nyukilia tusisahau mambo madogo madogo kwenye familia zetu yasije kutucost badae.
Na nyie wake zetu basi muwe mnatuwakiliasha wambie hizo pesa na mali wanazoona watoto nyumbani kuwa zimetokana na nguvu zetu sote. Tusije tukatengwa huko mbeleni.
Yangu ni hayo tu Nawatakieni Jumaa Kareem.
Asalaam Aleykum
Huwa nikifikiria hili suala akili inachanganyikiwa..Jambo la kuzingatia mwanaume yeyote ni kuhakikisha unatunza pesa ztakazo kutunza uzeen,hakksha hukos hela mpaka utakapo kufa panda hata miti iwe kama akiba au fuga mifugo za kutosha kama akiba.
Maana kuna kutengwa uzeen,wanao na mama yao wakawa mbali na wewe
Unajua kisa cha Mengi kuoa Klyn vizuri. For your informations ni baada ya kususwa na familia yake. Pamoja na kuwa bilionea.Ukizeeka na una mahela yako fresh tu. Tafuta hela, kwani hakuna ambaye atakuona tajiri akakususa.
RIP mengi.
😅😅😅😅umenifurahisha mchango wako. Hata kama kanunua Mama anipe nimpatie au sio?Hata ukitoa pesa mbele yao na wewe hujui hata size ya viatu vya watoto ni bure kabisa. Mtoto kitu kidogo tu anaona anapendwa. Akipewa zawadi kidogo na mtu mwingine ambaye sio mzaz hatomsahau huyo mtu na zawad aliyompa kamwe.
Ameona umempa mama hela ya viatu au toys lakini mama ndio amemchagulia hivyo vitu. Kua na time na watoto sio home ni nje ya nyumbani au uwaletee tuvitu hata mama akinunua lakini akupe kinyemela umpe mtoto.
Ndio sisi wanaume tumepewa Dhima ya kuongoza familia vizuriAsante kutukumbusha
Umdmpa mama pesa amnunulie mtoto kitu. Akupatie wewe ndio umkabidhi mtoto[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]umenifurahisha mchango wako. Hata kama kanunua Mama anipe nimpatie au sio?
Nimeichukua hii pointiUmdmpa mama pesa amnunulie mtoto kitu. Akupatie wewe ndio umkabidhi mtoto
Hawa watoto wetu baadae uzeeni huwa Wanakuwa closed Sana na Mama zao,Jambo la kuzingatia mwanaume yeyote ni kuhakikisha unatunza pesa ztakazo kutunza uzeen,hakksha hukos hela mpaka utakapo kufa panda hata miti iwe kama akiba au fuga mifugo za kutosha kama akiba.
Maana kuna kutengwa uzeen,wanao na mama yao wakawa mbali na wewe
Naitumia sana hii...Siku moja moja mpe mkeo pesa mbele ya watoto wako itawasaidia kujua wewe ndio unatoa hizo pesa mama aweza waambia lakini wakiona kwa macho itaweza saidia zaidi
Mm hata nikisafiri kikazi... nikirudi Buti imejaa mazagaza... namwambia dada njoo na Mtoto... haya tushushe... dada... Mikungu, Bint... toa kuku hao... mwenyewe najitwisha maroba ya Mahindi ama Mchele .... Mama yao pembeniyeah tena itoe bila kuona haya inasaidia mno watoto wanajua baba anatuhudumia na ndie anamuachia mama hela
hii imekaa poaMm hata nikisafiri kikazi... nikirudi Buti imejaa mazagaza... namwambia dada njoo na Mtoto... haya tushushe... dada... Mikungu, Bint... toa kuku hao... mwenyewe najitwisha maroba ya Mahindi ama Mchele .... Mama yao pembeni
ahah nipo mbonaNaitumia sana hii...
Mm hata School Fees... namchukua Mwanangu mpk ATM... natoa nae Muhamala... Haooooo mpk Bank Wakala.... nalipa... nachukua receipt namshikisha... safari Shuleni... namwambia kampe Muhasibi....
BTW umepotea
Tuanze michakato mapema yasitukuteHawa watoto wetu baadae uzeeni huwa Wanakuwa closed Sana na Mama zao,
Sie mababa mwendo wa kutengwa tu
😅😅😅safi sana MkuuNaitumia sana hii...
Mm hata School Fees... namchukua Mwanangu mpk ATM... natoa nae Muhamala... Haooooo mpk Bank Wakala.... nalipa... nachukua receipt namshikisha... safari Shuleni... namwambia kampe Muhasibi....
BTW umepotea
wee ni noma. Maroba unajitwisha kichwani unaingiza ndaniMm hata nikisafiri kikazi... nikirudi Buti imejaa mazagaza... namwambia dada njoo na Mtoto... haya tushushe... dada... Mikungu, Bint... toa kuku hao... mwenyewe najitwisha maroba ya Mahindi ama Mchele .... Mama yao pembeni
Bottom line ni kuwa unamiliki gari.Mm hata nikisafiri kikazi... nikirudi Buti imejaa mazagaza... namwambia dada njoo na Mtoto... haya tushushe... dada... Mikungu, Bint... toa kuku hao... mwenyewe najitwisha maroba ya Mahindi ama Mchele .... Mama yao pembeni
Bottom line ni kuwa unamiliki gari.