Wanaume kuwa na tabia za kikekike ni janga linaloikumba Nchi yetu

Wanaume kuwa na tabia za kikekike ni janga linaloikumba Nchi yetu

WANAUME KUWA NA TABIA ZA KIKEKIKE NI JANGA LINALOIKUMBA NCHI YETU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nyakati za zamani nikiwa nakua zipo tabia ambazo tuliaminishwa ni tabia za kike(inaweza kuwa ni kasumba), ambazo ilikuwa mwiko kwa mwanaume kuwa nazo.
Ilikuwa ni aibu na fedheha kwa kijana kuwa na tabia za namna hiyo.

Nilipofika Kidato cha tano na sita nikaanza kuona muelekeo tofauti wa kile nilichoaminishwa nikiwa mtoto. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona Wanaume Wambeya, wenye Majungu, Kijichi na wivu wa kipuuzi. Nilisikitishwa sana.

Hivi mwanaume unaonaje woga kum-face mtu na kumchana ukweli ikiwa kama anakosea au unaona hakufurahishi?

Hivi mwanaume unamchukiaje mtu iwe ni Mwanamke au mwanaume mwenzako ambaye hamuingiliani wala kuhusiana kwa jambo lolote?
Hivi mwanaume unamuoneaje wivu mwanaume mwenzako kisa amekuzidi jambo fulani?

Nikamaliza chuo na sasa nipo mtaani kwa kitambo. Aiseeh! Mengi nilichoaminishwa nikiwa mdogo yalikuwa ni uongo mtupu. Labda ilikuwa kweli lakini Wanaume wa sasa ndio wamebadilika na kuwa tabia za KIKEKIKE.

Kula chuma; tabia za kike ambazo vijana wengi wa sasa wapo nazo,

1. Wanaume wengi wa sasa ni Wambeya kuliko Wanawake.
Ni kawaida siku hizi kijana kuwa mbeya. Kuongea mambo ya wengine huku akisahau yake.
Ni kawaida hapo mtaani unapoishi ukipita kijiweni vijana wakaulizana; huyu jamaa anakaa wapi, anafanya kazi gani, ana nini?
Bora hata anayeuliza angekuwa demu tungesema anatafuta Bwana sasa wewe mwanaume mzima unauliza habari za wanaume wenzako ili upate nini?
Umbeya ndio mwanzo wa uchawi na matabia mengine ya hovyo.

2. Chuki za kijingajinga.
Hivi unaanzaje kumchukia mtu ambaye hakuhusu, hukujui wala humjui(ila unataka kumjua)
Unamsikia kijana kama chizi utasikia linasema; huyu dada simpendi anajishaua sana, anaringa sana, hasamilii, sijui anapaka sijui MakeUp za kishamba, n.k.
Au tabia ya kuchukia vijana wenye ubize na kazi zao. Utasikia unaona hiyo bajaji sio yake amepewa na Mjombaake, mara ooh! Ile gari ya mkopo. Ooh! Jamaa hasalimii utadhani salamu inakuongezea maisha. Hizo ni tabia za kikekike.
Kama unataka kusalimiwa Oa, zaa watoto wape chakula wakusalimie Boya wewe.
Haya Hivi huyo dada unayemchukia unamsaidia nini wewe ambaye maisha yako tuu yanakupiga chenga.

3. Majungu na kusengenya.
Hivi hamuwezi kuishi maisha yenu pasipo kuwapiga wenzenu majungu. Hiyo tabia ilihusishwa na jinsia ya kike. Lakini kadiri miaka inasonga ukweli unabainika kuwa hata wanaume wenye Majungu na kusengenyana ipo.
Na hili inatokana na kuoneana wivu, chuki lakini pia na roho mbaya.
Unamsema mwazeko alafu mara nyingi wenye tabia hizo wengi wanasaidiwa au ni Watu walioshikwa mkono yaani wapo sehemu fulani kimazabezabe.

4. Hasira na kuendeshwa na mihemko.
Siku hizi ni kawaida kumkuta kijana analia ati kisa amefanyiwa jambo fulani hata kama ni dogo.
Au unakuta kijana anasusasusa kama jinga fulani.
Au kijana hataki kuambiwa ukweli na kama ikitokea ukimwambia ukweli ati anakuchukia. Hizo tabia wanazo wanawake. Mwanaume ni yule kiume ambaye yupo tayari kuambiwa ukweli na akaustahimili. Sio unaambiwa ukweli unanuna au unarusha ngumi kama mpuuzi hivi.

5. Woga hasa kwa Maboss
Mwanaume mzima unakuwa bendera fuata upepo kama mwendawazimu. Ati chawa! Haya sawa kuwa chawa kwa vitu vya maana, hilo limekushinda.
Woga unasababisha unafiki. Unachekacheka kama Mwanamke mbele ya boss hata kama unaona kabisa hapa Boss kakosea. Hizo ni tabia za kike Boya wewe.

Inakuwa ni aibu kwa Mkeo na watoto. Ati baba yao anatabia za kiajabuajabu. Mwoga, sio jasiri (sio mwanaume).

6. Kuchunguza Maisha ya wengine.
Ufukunyuku ilikuwa tabia za wanawake kufukunyuana mpaka wajue mwenzake anamiliki nini ndani ya nyumba. Lakini siku hizi vijana ndio wamegeuka wafukunyuku.
Hivi kijana unamiaka zaidi ya 25 unafuatilia maisha ya mtu mwingine unataka akuoe au?
Ujue anamiliki nini? Amepataje pesa ya kununulia kiwanja au gari? Ndani kwake ana nini? Unataka akugeuze Mke?
Au ndio unatafuta...? Acha tabia za kiajabuajabu, wewe ni mwanaume.

7. Wivu na tamaa.
Vijana wivu sio tabia ya kiume. Hupaswi kumwonea mwanaume mwenzako wivu wala kuwa na tamaa ya vitu alivyonavyo mwenzako.
Ridhika na kazi yako, Ridhika na mshahara au kipato chako. Fanya kazi kwa bidii. Kupata ni majaliwa. Wajibu wako ni kuchapa kazi kwa bidii na weledi wa hali ya juu, wakati wako ukifika utapata.

Sio uanze kusumbua Watu. Kutafuta Watu ubaya na kuwapa majina yako mabaya ya chuki.

Maisha yasikuendeshe kama kiberenge. Fanya maisha yako na Ridhika na hali yako.

8. Kujipodoa kikike kike.
Wengi wanaotafuta kuwa handsome boy huishia Kufirwa na kuwa Mashoga.
Unataka uzingatiwe kwa utanashati umekuwa mlimbwende?
Unakuta kakijana Kamepaka Kokoto kichwani, Lipustiki midomoni, Kamepaka MakeUp usoni. Kametoboa masikio au kuweka Hereni za kubandika, kamejipigilia unyunyu kananukia, alafu kana onyesha mapaja au kanavaa visuruali vinavyoyatepesha matako yake yawe laini. Utaacha Kufirwa kweli kwa upuuzi wako?

Tabia ya kike ni pamoja na kujipendezesha ili upendwe na Wanawake, uwavutie, wengi huishia kubaya.

Vaa kama mwanaume. Hata kama ni utanashati uwe wa kiwango cha kati kurudi chini.
Vaa suruali nzito ya kium kama unatoka mtoko inaweza kuwa Kadeti, jeans au kitambaa.
Sio uvae vikaptura au nguo za mazoezi wakati haupo kwenye mazoezi.

Pensi vaa lakini angalau zitoke kwenye Goti kwenda chini na kisikubane. Ukisema nisikupangie maisha Fresh,

Ongea kama mwanaume. Usiwe mtu wa lawama lawama kama kinga fulani hivi.

Usiwe mtu wa kuendeshwa na vitu hizo ni tabia za kikekike.

9. Kugombea mademu.
Kugombea demu ni tabia za kike hizo. Wanawake ndio wanagombea wanaume kwa sababu wanaume ni wachache lakini pia wanaume wenye Quality ni wachache zaidi.
Sasa mwanaume mzima unalilia Mapenzi kama jinga fulani hivi.
Unampigia mwanamke magoti kama mwehu. Hizo ni tabia za kipuuzi.

Mwanamke anakuletea maringo piga chini. Kwani lazima wewe uwe naye. Kulazimisha mapenzi ni dalili ya ukike, hujiamini.
Mtu umemfuata, umemueleza hisia zako, kakuringia au analeta manjonjo, sawa ukasema labda ndio Mikogo ya wanawake ili uwambeleze. Taikon atakuambia bembeleza lakini sio uzidishe mipaka.

Mwanamke hakutaki unamlazimisha wa nini Boya wewe.
Ashakuona humfai, au labda hapati anayoyataka. Kwa nini ulazimishe. Matokeo yake ndio ninyi mnaenda mpaka kwa waganga wa kienyeji kisa mapenzi. Hizo ni tabia za kikekike...

Tenda Haki, usiwe mtu wa kulinda pinda, nyoosha maelezo. Usiwe mwoga.

Mtu yeyote (hasa Haters au Watu wasiopenda kujadili mambo kwa hoja"ukweli") asikupangie Maisha kama unachofanya hakikudhuru wewe, familia yako na future yako. Hakikisha unaelewa Watu na kuwaweka kwenye makundi yao.
Hata kama ni mimi Taikon. Kama siongei hoja nipuuze tuu.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Hii post imewanyanyapaa sana wanawake na kukuonesha wewe kuwa ni mtu mbaguzi wa kijinsia mwenye stereotypical misogyny.

Zaidi, imekuonesha kuwa unaamini sana katika gender stereotypes nyingi ambazo hazina msingi wowote katika ukweli na sayansi.
 
Mwanamke amedhalilishwaje hapo na Taikon?
1. Wanawake hawajipambi kwa shedo na lipstik?
2. Wanawake hawacheki mtu kwa sauti anayepita mbele yao (umbeya)?
3. Wanawake hawadekideki kutaka upendeleo kila mahali?

Kula chuma hiyo ya Taikon, kama uko hivyo badilika.
Je zile tabia mbaya zinazofanywa na wanaume, wakifanya wanawake mbona hamuwaambii kuwa wanatabia za kiume?
 
Husitembelee historia kwani huandikwa upya kila uchao. Na husibaki na asili kwani uvumbuzi wa mambo mapya hufanyika kila iitwayo leo.
Ukigombea mwanamke zama hizi ili kumlazimisha awe nawe unapunguza siku za kuishi makusudi. Take it!
Ngaruma ni majina ya Rufiji, huko kuna mzee mmoja namfahamu alikuwa anaitwa Mohamed Ngaruma, mungu amrehemu... Nimeona hilo jina nimekumbuka...

Kuhusu mwanamke, kama ni mzuri lazima agombewe, au unasemaje sheikh... Hiyo ndio asili ya mwanaume, zama hizi zimegubikwa na tamaduni za ajabu ajabu
 
Hii kugombea mademu ni asili ya kiumbe chochote cha kiume.

Kwenye maandiko kwenyewe Ibrahim alitaka kunyanganywa mke wake na mfalme...


Kiasili Mwanamke hatakiwi kugombea mwanaume, mwanamke anapaswa kutulia. Wewe lini uliwahi kuona kuku jike wakigombea jogoo... Kiasili Mwanaume ni mtawala, anayetaka kumiliki, hivyo atapigana kumiliki.

Hizo tabia za kulia kisa mwanamke ni Agenda nyingine.

Kitendo cha kutongoza tu ni kugombea mwanamke, kwa sababu mnaorusha sound hapo utakuta ni wengi, mwenye sound ya maana ndio anachukua chombo.

Ushamba ni wewe kukataliwa na mwanamke unaanza kulazimisha kwa nguvu, labda useme inabidi mwanaume ujifunze kukubali matokeo ya kukataliwa
Hata ukienda Serengeti ukikuta madume yanazipiga mara nyingi sababu huwa ni mbili tu - chakula na mademu!
 
Hii post imewanyanyapaa sana wanawake na kukuonesha wewe kuwa ni mtu mbaguzi wa kijinsia mwenye stereotypical misogyny.

Zaidi, imekuonesha kuwa unaamini sana katika gender stereotypes nyingi ambazo hazina msingi wowote katika ukweli na sayansi.
Huyu kijana inaonekana bado mdogo na huenda kuna sababu iliyo nyuma ya pazia ambayo inamfanya awe na hasira na chuki dhidi ya wanawake. Nyuzi zake nyingi anaonyesha machungu mengi dhidi ya wanawake.
 
Huyu kijana inaonekana bado mdogo na huenda kuna sababu iliyo nyuma ya pazia ambayo inamfanya awe na hasira na chuki dhidi ya wanawake. Nyuzi zake nyingi anaonyesha machungu mengi dhidi ya wanawake.
Watu wa aina hii wengi, wana tatizo la kukosa elimu, kukosa nafasi ya kutembea duniani na kuona maisha tofauti, watu tofauti, tamaduni tofauti.

Yani mtu anaweza kuangalia wanawake wa kijijini kwake kwenye umasikini na elimu duni, halafu akarahisisha mambo tu kwamba wanawake wote wako hivyo.

Kumbe, yale anayoona ni matatizo ya umasikini na elimu duni ya kijijini kwake, si matatizo ya wanawake.
 
1. Wanaohonga ni wanaume walioshindwa kutumia nguvu ya ushawishi au waliopungukiwa sifa fulani za kuwavutia wanawake.

2. Majike ndio yanayogombea wanaume ndio maana Mwanaume anaweza kumiliki majike wengi lakini wanawake ni ngumu kuolewa na wanaume wengi.

3. Mwanaume ameumbwa kupambana kwa vitu na sio kulazimisha Watu
Jomba umeishiwa kabisa nondo za kushusha hapa JF? Huu uzi wako umejaa tu chuki kwa wanawake kana kwamba wao ndo wamiliki wa tabia mbaya. Acha hizo fikra za kibaguzi. Mwanaume kuhonga ni jambo la kawaida na ni la kiasili. Wakati Isaka anaenda kuposa kabla hata ya maongezi alimpa yule binti vito vya thamani. Kama wewe ni mhanga wa jambo lolote baya ulilowahi kufanyiwa na mwanamke samehe endelea na maisha. Kuandika nyuzi za kuonyesha chuki dhidi yao kunakufanya uonekane MWANAUME DHAIFU. Unavyosema mwanamke sio wa kulazimishwa ni kama vila unataka kukimbia majukumu yako kama mwanaume... TOKA HUKO KWENYE FIKRA ZA KIVULANA UJE KWENYE UANAUME.
 
Watu wa aina hii wengi, wana tatizo la kukosa elimu, kukosa nafasi ya kutembea duniani na kuona maisha tofauti, watu tofauti, tamaduni tofauti.

Yani mtu anaweza kuangalia wanawake wa kijijini kwake kwenye umasikini na elimu duni, halafu akarahisisha mambo tu kwamba wanawake wote wako hivyo.

Kumbe, yale anayoona ni matatizo ya umasikini na elimu duni ya kijijini kwake, si matatizo ya wanawake.
Inasikitisha sana. Ila dogo kupitia nyuzi zake kajitambulisha kama mhitimu wa UDSM. Nadhani hiyo kutoka nje ya nchi labda hajatoka kwasababu kwenye nyuzi zake panatajwa Morogoro na Dsm tu.
 
Hapo kwenye kufuatilia "huyu jamaa anafanya Kazi wapi ,hivi ana gari ? ," wapo wanaume wengi Sana hasa WA DSM Kazi yao Ni hiyoo hasa kama hujichanganyi vijiwen Kwao [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu neno "CHAWA, ndio linafanya wanaume wengi wamebadilika na kuuvaa uhalisia wa KIKE ukubwani
Jaribu kuangalia wanaume wambea na watanashati wengi wapo nyuma ya mwanaume mwenzao ama mwenye cheo au pesa
Ova
 
Wengine tuko nao humu muda wote kufatilia mambo ya wanaume wenzao
Km vipi taicon wataje 😂😂😂
Me naimarisha ulinzi hapa
Yaani wewe nishakuona una viukorofi vya chini chini unauma unapuliza , unauma unapuliza huku ukitabasamu...kimoto kikikaribia kuzima unakimwagia tumafuta twa taa halafu unakaa pembeni kujichekelesha chekelesha. Yaani...🔥🔥🔥
 
Back
Top Bottom