Wanaume kuwa na tabia za kikekike ni janga linaloikumba Nchi yetu

Hii post imewanyanyapaa sana wanawake na kukuonesha wewe kuwa ni mtu mbaguzi wa kijinsia mwenye stereotypical misogyny.

Zaidi, imekuonesha kuwa unaamini sana katika gender stereotypes nyingi ambazo hazina msingi wowote katika ukweli na sayansi.
 
Je zile tabia mbaya zinazofanywa na wanaume, wakifanya wanawake mbona hamuwaambii kuwa wanatabia za kiume?
 
Husitembelee historia kwani huandikwa upya kila uchao. Na husibaki na asili kwani uvumbuzi wa mambo mapya hufanyika kila iitwayo leo.
Ukigombea mwanamke zama hizi ili kumlazimisha awe nawe unapunguza siku za kuishi makusudi. Take it!
Ngaruma ni majina ya Rufiji, huko kuna mzee mmoja namfahamu alikuwa anaitwa Mohamed Ngaruma, mungu amrehemu... Nimeona hilo jina nimekumbuka...

Kuhusu mwanamke, kama ni mzuri lazima agombewe, au unasemaje sheikh... Hiyo ndio asili ya mwanaume, zama hizi zimegubikwa na tamaduni za ajabu ajabu
 
Hata ukienda Serengeti ukikuta madume yanazipiga mara nyingi sababu huwa ni mbili tu - chakula na mademu!
 
Hii post imewanyanyapaa sana wanawake na kukuonesha wewe kuwa ni mtu mbaguzi wa kijinsia mwenye stereotypical misogyny.

Zaidi, imekuonesha kuwa unaamini sana katika gender stereotypes nyingi ambazo hazina msingi wowote katika ukweli na sayansi.
Huyu kijana inaonekana bado mdogo na huenda kuna sababu iliyo nyuma ya pazia ambayo inamfanya awe na hasira na chuki dhidi ya wanawake. Nyuzi zake nyingi anaonyesha machungu mengi dhidi ya wanawake.
 
Unakuta mwanaume anapelekeshwa na mwanamke na lenyewe lipolipo tu

.mfano siku moja mpoto mshairi asiyejua kuvaa viatu alinena mbela ya camera kuwa mke wake ni kichwa cha familia na yeye hawezi kuzungumza chchte mbele ya watu au vyombo vya habari mpka apate ruhusa kwa mkewe.


Nilisikitika sana
 
Huyu kijana inaonekana bado mdogo na huenda kuna sababu iliyo nyuma ya pazia ambayo inamfanya awe na hasira na chuki dhidi ya wanawake. Nyuzi zake nyingi anaonyesha machungu mengi dhidi ya wanawake.
Watu wa aina hii wengi, wana tatizo la kukosa elimu, kukosa nafasi ya kutembea duniani na kuona maisha tofauti, watu tofauti, tamaduni tofauti.

Yani mtu anaweza kuangalia wanawake wa kijijini kwake kwenye umasikini na elimu duni, halafu akarahisisha mambo tu kwamba wanawake wote wako hivyo.

Kumbe, yale anayoona ni matatizo ya umasikini na elimu duni ya kijijini kwake, si matatizo ya wanawake.
 
Jomba umeishiwa kabisa nondo za kushusha hapa JF? Huu uzi wako umejaa tu chuki kwa wanawake kana kwamba wao ndo wamiliki wa tabia mbaya. Acha hizo fikra za kibaguzi. Mwanaume kuhonga ni jambo la kawaida na ni la kiasili. Wakati Isaka anaenda kuposa kabla hata ya maongezi alimpa yule binti vito vya thamani. Kama wewe ni mhanga wa jambo lolote baya ulilowahi kufanyiwa na mwanamke samehe endelea na maisha. Kuandika nyuzi za kuonyesha chuki dhidi yao kunakufanya uonekane MWANAUME DHAIFU. Unavyosema mwanamke sio wa kulazimishwa ni kama vila unataka kukimbia majukumu yako kama mwanaume... TOKA HUKO KWENYE FIKRA ZA KIVULANA UJE KWENYE UANAUME.
 
Inasikitisha sana. Ila dogo kupitia nyuzi zake kajitambulisha kama mhitimu wa UDSM. Nadhani hiyo kutoka nje ya nchi labda hajatoka kwasababu kwenye nyuzi zake panatajwa Morogoro na Dsm tu.
 
Hapo kwenye kufuatilia "huyu jamaa anafanya Kazi wapi ,hivi ana gari ? ," wapo wanaume wengi Sana hasa WA DSM Kazi yao Ni hiyoo hasa kama hujichanganyi vijiwen Kwao [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu neno "CHAWA, ndio linafanya wanaume wengi wamebadilika na kuuvaa uhalisia wa KIKE ukubwani
Jaribu kuangalia wanaume wambea na watanashati wengi wapo nyuma ya mwanaume mwenzao ama mwenye cheo au pesa
Ova
 
Wengine tuko nao humu muda wote kufatilia mambo ya wanaume wenzao
Km vipi taicon wataje πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Me naimarisha ulinzi hapa
Yaani wewe nishakuona una viukorofi vya chini chini unauma unapuliza , unauma unapuliza huku ukitabasamu...kimoto kikikaribia kuzima unakimwagia tumafuta twa taa halafu unakaa pembeni kujichekelesha chekelesha. Yaani...πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…