Wanaume mna shida gani? Unamuheshimu mtu, anakuja kukutongoza

Wanaume mna shida gani? Unamuheshimu mtu, anakuja kukutongoza

Nyie leo nimechemka kwa hasira mtu aje vizuri bila hivyo nitampiga kichwa cha pua😠😠
hivi kwanini nyie wanaume wengi wenu adabu hamna, unamuheshimu mtu vizuri tu na kumuita majina kama kaka, anko, baba, mwisho wa siku anakuja kukutongoza tena mchana kweupeeee tena live hata hapepesi macho, umetoka kuliamkia linakuja kukwambia "nakupenda sana kwa kipindi kirefu...." seriously!!!!

Jirani yangu niliyekua namuheshimu, namuita kaka, leo asubuhi asubuhi kaja kwangu anajifanya kuomba miche ya michai chai wakati nampa kisu akakate, si ndio ananishika mkono eti anajifanya yupo serious anamaanisha anachokisema nalinukuu "samahani mdogo wangu kama nitakukwaza lakini mimi navutiwa sana na wewe, naomba unikubalie tufanye maisha utafurahi", nilimuangalia kwa hasira nikautoa kwa nguvu mkono wake nikamwambie atoke nyumbani kwangu kabla sijapiga kelele, likatoka bila haya wala soni, WTF!

Kuna huyu mzee pia enzi hizo bado tunapanga, nilikua namuheshimu sana alikua mpemba nikawa namuita anko, huyu baba mwenye nyumba hakua akiishi hapo ila tulivyohamia na yeye akaja kuishi kwenye one of his apartments hapo hapo, siku moja ilikua jioni akanitumia meseji niende kwake, nakumbuka nilikua nimevaa a short pant na vest ilikua msimu wa joto, so nikaenda nikamkuta sitting room akanikaribisha akaniofa juice au soda nikamwambia i'm good, basi akaanza kutiririka, huyu mzee ana mke na watoto, namnukuu "Mariposa unajua wewe ni mrembo sana, sipendezwi na life style yako, nataka nikuoe tuzae watoto wawili tu sitaki niuchoshe mwili wako, baada ya hapo utaamua kuendelea na mimi au kurudi kwenye mambo yako ila watoto nitawalea mimi, nahitaji urithi wa hizi mali...." nilibaki nimeduwaaa maswali mengi yalipita kichwani nikakumbuka nilikua nimevaa kihasara hasara nikapata hofu asije akanivamia wee acha nitoke nduki, nikakimbilia ndani nikafunga milango na madirisha natetemeka, mpenzi wangu alikua kasafiri, nikampigia simu kumwambia akanicalm down akasema acha niongee nae mimi, lakini sikua na amani tena ndio sababu ilinifanya nikahamia kwenye nyumba yetu ikiwa bado hata haijaisha,

Ifike mahali nyie watu wazima visheti mjiheshimu kama mnavyoheshimiwa, kutamani tamani hovyo mtakuja kukutana na visivyoliwa oooonho msiseme sikuwaambia.

Adios!
@Dr Mariposa umeolewa?
 
Mpenzi wake ni mdada jamani mbona huwaga mnajisahaulisha kwamba alishasema yeye ni lesbian?alishasema hapendi wanaume,
Alaaah! Mie sikulijua hilo. Kumbe ndo maana kwenye stori yake kasema kuna siku alivaa kipensi kifupi na vest akampandisha midadi ba mjengo!

Hahahaaa sasa mbona alitoka nduki baada ya kutongozwa na ba mjengo? Si angemjibu tu dry kwamba "mzee ngoja nikakuvalie dushe la plastic ndo uujue undani wangu"
 
Ila daktari kuna siku njemba flani atakuotea utapelekewa moto mpaka uache kuwapuuza uwe unamuona kwenye glass😅
Ishu sio kupelekewa moto hata huku nilipo napeleka na kupelekewa moto, ishu ni hisia hazipo upande huo, yaan kama ambavyo wewe unaona mwanamke mwenzio hakupi hisia zozote basi na mimi ndio hivyo mwanaume hanipi hisia zozote.
 
Back
Top Bottom