Wanaume: Munatumia njia gani kuwasiliana pengine hata kukutana na mzazi mwenzio aliyeolewa?

Wanaume: Munatumia njia gani kuwasiliana pengine hata kukutana na mzazi mwenzio aliyeolewa?

Hayo yote uliyosema yanawezekana,ila mimi nipo makini sana na singeweza kuyasema yote niyafanyayo,kaa ukijua namsimamia mtoto vizuri sana,na tuna kutana naye na sheninpua huwa naenda na huyu mume wa mzazi mwenzangu ni mtu mwema sana,na huwa wananitembelea nyumbani kwangu wakiwa na mkewe mara kwa mara
Mpaka hapo kulikuwa hakuna haja ya kuweka andiko lako humu mkuu, endelea kufurahia maisha.
 
Mimi nimezaa na mdada mmoja ambae kwa sasa kaolewa na anaishi na mwanangu na huyo mumewe,hivyo mawasiliano yangu yote kuhusu malezi ya mtoto huyo hupitia kwa mumewe,na kama kuna siku nataka kumuona mtoto namuatifi mumewe ambae ndio atamjulisha huyo mzazi mwenzangu ambae ni mkewe.Sina mawasiliano na huyo mzazi mwenzangu ya moja kwa moja
Unafanya vizuri sana, na hii ndio njia sahihi nilitaka kukuambia
Bora kuwasiliana man to man ili kuepuka mtafarukano baina yenu
Tena mnakuwa washikaji kabisa na jamaa na ukimuhitaji kumtoa mwanao unamchukua bila kinyongo wala hiana
Kila wakati lazima unakuwa karibu na mume inaleta uhusiano mwema
 
Habari mara nyingi Watu wengi wanajikuta wamezaa nje ya ndoa na mwenzie kuolewa Na mnamtoto tayari.

Mtoto anahitaji malezi ya baba na mama.

Sasa njia gani unatumia kuwasiliana na mzazi wenzio aliyeolewa tayari afu utakuta huko anaishi na mtoto wako au mtoto unaishi naye sometimes mtoto atataka kukutana na mama yake, pengine hata na baba.

Njia gani Mnatumia kufanikisha hili?
Karibuni.
Siruhusu hata kwa dawa mwanamke kumchukua mwanangu labda awe mdogo kisheria. Pili siruhusu kamwe mawasiliano na mtoto ili nisimlaumu katika makuzi na malezi. Ila akiwa mkubwa namruhusu aende hata akimjengea ghorofa hainihusu, nimeishatimiza wajibu wangu.
 
mwanamke ni adui yako?
 
kuepusha hayo yote oa uliyempa mimba, kama huna mpango naye acha mawazo ya kuzaa naye
Ujana ni umri wa makosa na makosa hayo ndio ambayo huwapa watu uzoefu wa maisha so jamaa inaonekana anayo nia njema ya kutokutana kuvunja hiyo ndoa ndio maana anaomba ushauri kwa watu wenye uzoefu hapa so kuliko kumlaumu kwenye makosa ambayo tayari yameshatendeka nadhani ni vyema apewe uzoefu kwanza wa namna ya kufanya.
 
Taabu kweli kweli. Mimba umpe wewe, mtoto wa kwako ila ndo hivyo kuna mwanaume anakuamulia unamuonaje mwanao.

Njia nzuri ni kuwa na dalali.

Mtoto ana bibi, mjomba, shangazi n.k mmoja awe ndo dalali wa mawasiliano.

Mfano, baba unataka kumuona mtoto, mpigie dalali shangazi au dalali yoyote anayeheshimika na baba mwenzako yeye ndo awasiliane na mama mtu, mama mtu awasiliane na mumewe ambaye ni baba mwenzako, dalali aruhusiwe kuja kumchukua mtoto umsalimie.

Ukikosea kidogo ukajifanya mwamba ndo umevunja ndoa na utamlea wewe huyo mwanao aliyekushinda mpaka uruhusu akalelelwe na baba mwingine.
 
M
Kabisa hata kule shuleni kwenye sherehe za shule anaenda huyo mume wa mzazi mwenzangu na panapotokea shida hunipigia simu kuniarifu maendeleo
Mkuu unatoa huduma hewa bora husitoe pesa kabisa kwanini mtoto wako anakua kama mmechangia kumzaa na huyo Jamaa yani yeye ndiyo ana kuongoza, Mimi niliachaga kutuma pesa za mtoto wangu kwa Mama yake kwasababu yeye huyo mzazi mwenzangu kumbe alishaolewa bila mimi kujua na akawa ana taka niwe natuma pesa kwa mwanangu tu na alikua hataki Ndugu zangu wapajue mtoto anapoishi na hataki nijue mtoto anaishi kwenye mazingira gani yeye anachotaka ni tume pesa tu, Baada ya kuchunguza nikaja kujua kaolewa na ana mtoto mchaga kwahiyo pesa ninazo tuma za mwanangu anatumia kwa mtoto wake na mume wake uchumi wake siyo mzuri! Nikawaza sasa nikituma pesa za mwanangu kila baada ya siku moja ale Maziwa mayai na nyama, Samaki je atapikiwa na je kama atapikiwa anaishi nyumba ya watoto wangapi isijekua wanaishi familia kubwa ya watoto wengi akipikiwa maziwa na mayai wanagombania.
 
Suala lako na langu ni tofauti,mimi na huyo mume wa mzazi mwenzangu,tunazungumza kila kitu na kika nachofanya nakifuatilia na hakuna kinachoharibika na kwa taarifa yenu nyote huyo jamaa ni msomi na ni mtu mwenye pisa hivyo hachukui hata senti ya mtoto
 
Njia mnayotumia inaweza kuwa nzuri lakini ni mbaya pia. Uzuri ni kuwa unalinda ndoa ya mzazi mwenzio na unamuongezea confidence na ubaya ni kuwa huenda mwanao anaweza asipate mahitaji unayompatia ikitegemea uwezo wa mume mwenzio. Pia kwa kuwa mawasiliano na mzazi mwenzio hayapo unawezajikuta unalipia bill za bia kupitia mtoto.

Mahitaji yote anayopatiwa mtoto lazima mama na mtoto wayajue kama ana umri wa kutosha. Na Ikiwezekana mama ampe simu mtoto ndio aseme mahitaji yake na yakikamilishwa aone. Vinginevyo unaweza kuwa unatunza mtoto sifa zinaenda kwao wewe unasagiwa kukunguni huna msaada wowote. Utabaki unashangaa mtoto amekuza chuki kwako hata huelewi sababu.

Kama yuko shule na una uwezo chukua peleka hata boarding huko likizo akae kwa mama yake wiki mbili aje kwako wiki mbili na upate nafasi ya kumtembelea shule.
Ramli chonganishi hizi
 
Habari mara nyingi Watu wengi wanajikuta wamezaa nje ya ndoa na mwenzie kuolewa Na mnamtoto tayari.

Mtoto anahitaji malezi ya baba na mama.

Sasa njia gani unatumia kuwasiliana na mzazi wenzio aliyeolewa tayari afu utakuta huko anaishi na mtoto wako au mtoto unaishi naye sometimes mtoto atataka kukutana na mama yake, pengine hata na baba.

Njia gani Mnatumia kufanikisha hili?
Karibuni.

Tunaheshimu ndoa za watu kwa kuwasiliana na kupata ruhusa kwa waume zao!
 
Back
Top Bottom