Wanaume: Munatumia njia gani kuwasiliana pengine hata kukutana na mzazi mwenzio aliyeolewa?

Wanaume: Munatumia njia gani kuwasiliana pengine hata kukutana na mzazi mwenzio aliyeolewa?

Habari mara nyingi Watu wengi wanajikuta wamezaa nje ya ndoa na mwenzie kuolewa Na mnamtoto tayari.

Mtoto anahitaji malezi ya baba na mama.

Sasa njia gani unatumia kuwasiliana na mzazi wenzio aliyeolewa tayari afu utakuta huko anaishi na mtoto wako au mtoto unaishi naye sometimes mtoto atataka kukutana na mama yake, pengine hata na baba.

Njia gani Mnatumia kufanikisha hili?
Karibuni.
Kama A alizaa mtoto Q akiwa na X, basi siku X akiolewa mawasiliano yao juu ya mtoto yatakuwa kwa protokoo maalumu, kwamba A akitaka kuwasiliana na X juu ya mtoto Q, yeyote kati yao atakaye initiate mazungumzo atatakiwa kuongea akiwa na mwenza wake wa wakati huo
 
Tafuta mwingine mkuu..mi ninavyo vitoto viwili vya nje. Nina amani kabisa. Wala sitishiki na vitisho vya watu hapa JF kuhusu kuzaa nje ya ndoa. Nina mpango wa kuongeza mmoja wa mwisho wa nje ya ndoa.
Usizae watoto wote kwa mama mmoja.
Mkuu umetumwa?
 
Sio kidogo, anataka kuharibu ndoa ya binti wa watu wakati hakumuona wa maana alipompa ujauzito, vijana wasiowajibika kwenye makosa yao ni waharibifu sana
Acha utoto, kwani wakati anamuoa hakujua kuwa tayari kuna mtoto wa mwanaume mwenzake?;
Acha hasira za kuachwa hukua çhaguo jamaa alikuwa anapita njia ukapata mimba bila kupanga.
 
Habari mara nyingi Watu wengi wanajikuta wamezaa nje ya ndoa na mwenzie kuolewa Na mnamtoto tayari.

Mtoto anahitaji malezi ya baba na mama.

Sasa njia gani unatumia kuwasiliana na mzazi wenzio aliyeolewa tayari afu utakuta huko anaishi na mtoto wako au mtoto unaishi naye sometimes mtoto atataka kukutana na mama yake, pengine hata na baba.

Njia gani Mnatumia kufanikisha hili?
Karibuni.
Achana na mke wa mtu nyie ndio huwa mnaharibu ndoa za watu
 
Kwann uoe mwanamke mwenye mtoto mm hata uwe pisi kali kama una mtoto sikuoii
 
Suala lako na langu ni tofauti,mimi na huyo mume wa mzazi mwenzangu,tunazungumza kila kitu na kika nachofanya nakifuatilia na hakuna kinachoharibika na kwa taarifa yenu nyote huyo jamaa ni msomi na ni mtu mwenye pisa hivyo hachukui hata senti ya mtoto
Inahitaji moyo kukaa hivyo, Basi tuu.
 
Mimi nilibahatika kuzaa mtoto na binti mmoja, mpaka sasa mimi nilioa mke mwingine na yeye aliolewa na mtu mwingine. Mtoto anakaa kwa mjomba wake(kwa shemeji yangu)
Mimi huwa nawasiliana na huyo mzazi mwenzangu moja kwa moja, lakini ni masaa ya mchana tu. Hakujawahi kuwa na shida yoyote ile.
 
Ungemuoa hizo shida usingepata
Mtoa mada anaomba tumpe uzoefu. Ilishatokea tayari kwa sasa si muda wa kumlaumu mtu kwa sababu hatuwezi kujua mazingira yaliyopelekea kutokuoana.
Tumpe uzoefu.
 
acheni ujinga kulinda ndoa sio hivyo kulinda ndoa ni mtu dhamira yake mwenyewe, huyo mke wa jamaa akiamua kuzini nayeyote anaweza kwanza anauhakika kiasi gani hawawasiliani..?

ndoa hailindwi, ukianza kuilinda ndoa tena mwanaume kuanza kumlinda mwanamke jua umeanza kuingia chaka! wenye ndo wanatakiwa wajilinde wenyewe maana ni kiapo!.. kama mtu huwezi kuingia kwenye ndoa nakuenenda na hiyo ndoa kuwa kama sisi tu washenyentaji...😅

Mantiki yako ya dhamira kwa wahusika katika kulinda NDOA au kuivunja ni Kweli Kwaiyo watu wanapoingi katika NDOA ni vyema kujenga dhamiri/nia ya kujenga, kuimarisha na kuilinda NDOA


Swala la kulinda NDOA sio la Mwanamke tu ni la wote kwa umoja i.e Mme na mke Lazima waungane na kuwa kitu kimoja katika kulinda agano la MUNGU
 
kuepusha hayo yote oa uliyempa mimba, kama huna mpango naye acha mawazo ya kuzaa naye
Mkuu hii hutokea wakati ambao hujajipanga kuzaa au kuoa na pengine uko shule unakuwa huna lengo baya kabisa
sasa ukiwa kwenye mihangaiko unasikia mwenzio huku kashaolewa na ukiuliza anakujibu wewe hata hueleweki na mimi siwezi kukusubiri na sijui lini utanioa je utafanyaje? hivi kumbe unajua anayeachwa ni mwanamke tu pasipokujua hata mwanamke hushawishika na kukuacha vilevile?

Hata mkeo anaweza kukuacha akaolewa na mwanao mdogo.
 
Back
Top Bottom