Wanaume: Munatumia njia gani kuwasiliana pengine hata kukutana na mzazi mwenzio aliyeolewa?

Wanaume: Munatumia njia gani kuwasiliana pengine hata kukutana na mzazi mwenzio aliyeolewa?

Kabisa hata kule shuleni kwenye sherehe za shule anaenda huyo mume wa mzazi mwenzangu na panapotokea shida hunipigia simu kuniarifu maendeleo
huyo mtoto ana bahati mno hapa duniani! Ana wazazi wa nne , kwa maturity hii sitarajii mkeo awe tofauti nanyi watatu
 
Ni kweli,tulikutana na kuongea details zote za kulea mtoto wangu na huyo jamaa,he is a good man,yapo mengine pia tunashirikiana japo siwezi kuyaweka hapa
Mpaka nasisimka vile unamuelezea huyu baba.
Hizi familia mbili zimebarikiwa, Mungu adumishe upendo na uelewa wenu pamoja!
Nimewapenda kiukweli
 
Habari mara nyingi Watu wengi wanajikuta wamezaa nje ya ndoa na mwenzie kuolewa Na mnamtoto tayari.

Mtoto anahitaji malezi ya baba na mama.

Sasa njia gani unatumia kuwasiliana na mzazi wenzio aliyeolewa tayari afu utakuta huko anaishi na mtoto wako au mtoto unaishi naye sometimes mtoto atataka kukutana na mama yake, pengine hata na baba.

Njia gani Mnatumia kufanikisha hili?
Karibuni.
Pitia kwa ndugu zake maana ukianza kuwasiliana naye direct utavunja ndoa yake maana hakuna mwanamme akatayevumilia huo Upuuzi wa kuwasiliana na X.
 
huyo mtoto ana bahati mno hapa duniani! Ana wazazi wa nne , kwa maturity hii sitarajii mkeo awe tofauti nanyi watatu
ha ha moja ya matatizo ya binadamu,badala ya kulifahamu tukio vizuri,ni kukimbikia kutoa lawama,hujui ilitokeaje nikazaa na huyo dada,hujui ilikuwaje akaolewa na huyo kaka,unakimbilia vuuupu kukaumu,sasa kwa taarifa yako mie nina wake 2 na wote hata kabla sijawaoa niliwataatifu kuwa nina mtoto wa nje na huwa anakuja likizo anakaa kwangu
 
Mpaka nasisimka vile unamuelezea huyu baba.
Hizi familia mbili zimebarikiwa, Mungu adumishe upendo na uelewa wenu pamoja!
Nimewapenda kiukweli
Unajua ni lazima tukubali kuwa kitu kinapotokea ni vizuri kutuliza vichwa iki kupata ufumbuzi unaokubalika pande zote 2,muhimu ni mimi kutoa matumizi kama tulivyokubaliana na pale wanalotoa wao ni wajibu wangu kuwarudishia
 
ha ha moja ya matatizo ya binadamu,badala ya kulifahamu tukio vizuri,ni kukimbikia kutoa lawama,hujui ilitokeaje nikazaa na huyo dada,hujui ilikuwaje akaolewa na huyo kaka,unakimbilia vuuupu kukaumu,sasa kwa taarifa yako mie nina wake 2 na wote hata kabla sijawaoa niliwataatifu kuwa nina mtoto wa nje na huwa anakuja likizo anakaa kwangu
mbona ni kama hujaelewa nilichoandika na ulichojibu ni tofauti.
Nilimaanisha kuwa mtoto analelewa kwa upendo na maelewane pande zote mbili. Sijalaumu mahali, sijahoji ilikuwaje mkazaa na huyo dada. sikuhitaji hata kujua ilikuwaje akaolewa. Yote HAYANIHUSU!
Nilikuwa nakusifu/nawasifu aina yenu ya co-parenting kuwa iko salama sana kwa mtoto mhusika.
Hii kuwa na wake wawili, hata pia sihitaji kujua kiasi iwe taarifa yangu!
Tubaki kwenye mada mezani na ulichoandika kuhusu namna unawasiliana na mume wa dada umezaa nae na mnashirikiana kulea mtoto.

HAPO TU. ndo nilipo na interest napo na nimewapongeza!

sawa?
 
Ni kwamba mimi na huyo dada tulipata mtoto bila kupanga na wala sikumpa ahadi yoyote kuwa ntamuoa,tuliongea sana nae na tulikubaliana tusitoe mimba ila nimsaidie kutunza,yeye alikuwa na kazi yake nzuri na mpaka leo anayo,basi baadae alipata mchumba na kabla hajaolewa alimwambia mchumba wake kuwa ana mtoto mmoja aliyezaa kabla hawajakutana.Mwanaume alikubali nami niliarifiwa kuwa anaolewa na nilitoa mchango na harusi yao nilihudhuria na sasa hizi familia 2 ni family friends.
 
mbona ni kama hujaelewa nilichoandika na ulichojibu ni tofauti.
Nilimaanisha kuwa mtoto analelewa kwa upendo na maelewane pande zote mbili. Sijalaumu mahali, sijahoji ilikuwaje mkazaa na huyo dada. sikuhitaji hata kujua ilikuwaje akaolewa. Yote HAYANIHUSU!
Nilikuwa nakusifu/nawasifu aina yenu ya co-parenting kuwa iko salama sana kwa mtoto mhusika.
Hii kuwa na wake wawili, hata pia sihitaji kujua kiasi iwe taarifa yangu!
Tubaki kwenye mada mezani na ulichoandika kuhusu namna unawasiliana na mume wa dada umezaa nae na mnashirikiana kulea mtoto.

HAPO TU. ndo nilipo na interest napo na nimewapongeza!

sawa?
Ok yawezekana sikukuelewa,nisamehe kwa hilo lakini nauthamini mchango wako
 
Yani watu mnasexy afu amjui matokeo ya kusexy , duuuuuu au mtoto?
 
M

Mkuu unatoa huduma hewa bora husitoe pesa kabisa kwanini mtoto wako anakua kama mmechangia kumzaa na huyo Jamaa yani yeye ndiyo ana kuongoza, Mimi niliachaga kutuma pesa za mtoto wangu kwa Mama yake kwasababu yeye huyo mzazi mwenzangu kumbe alishaolewa bila mimi kujua na akawa ana taka niwe natuma pesa kwa mwanangu tu na alikua hataki Ndugu zangu wapajue mtoto anapoishi na hataki nijue mtoto anaishi kwenye mazingira gani yeye anachotaka ni tume pesa tu, Baada ya kuchunguza nikaja kujua kaolewa na ana mtoto mchaga kwahiyo pesa ninazo tuma za mwanangu anatumia kwa mtoto wake na mume wake uchumi wake siyo mzuri! Nikawaza sasa nikituma pesa za mwanangu kila baada ya siku moja ale Maziwa mayai na nyama, Samaki je atapikiwa na je kama atapikiwa anaishi nyumba ya watoto wangapi isijekua wanaishi familia kubwa ya watoto wengi akipikiwa maziwa na mayai wanagombani
Duh! Bro wewe ni mbinafsi na mchoyo kinoma. Mbona kinacholetwa na mume mwenzio mwanao anapewa? Wewe tuma hela tsh 10,000 yako haiwezi kubadili hali za maisha ya familia mzee, mbaya zaidi hiyo hali ni temporary tu kwene maisha, kesho inawezekqna wewe ukashindwa hata hela ya kula. Wekeza wema mzee
 
Taabu kweli kweli. Mimba umpe wewe, mtoto wa kwako ila ndo hivyo kuna mwanaume anakuamulia unamuonaje mwanao.

Njia nzuri ni kuwa na dalali.

Mtoto ana bibi, mjomba, shangazi n.k mmoja awe ndo dalali wa mawasiliano.

Mfano, baba unataka kumuona mtoto, mpigie dalali shangazi au dalali yoyote anayeheshimika na baba mwenzako yeye ndo awasiliane na mama mtu, mama mtu awasiliane na mumewe ambaye ni baba mwenzako, dalali aruhusiwe kuja kumchukua mtoto umsalimie.

Ukikosea kidogo ukajifanya mwamba ndo umevunja ndoa na utamlea wewe huyo mwanao aliyekushinda mpaka uruhusu akalelelwe na baba mwingine.
wewe umemiss point
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom