Wanaume: Munatumia njia gani kuwasiliana pengine hata kukutana na mzazi mwenzio aliyeolewa?

Mpaka hapo kulikuwa hakuna haja ya kuweka andiko lako humu mkuu, endelea kufurahia maisha.
 
Unafanya vizuri sana, na hii ndio njia sahihi nilitaka kukuambia
Bora kuwasiliana man to man ili kuepuka mtafarukano baina yenu
Tena mnakuwa washikaji kabisa na jamaa na ukimuhitaji kumtoa mwanao unamchukua bila kinyongo wala hiana
Kila wakati lazima unakuwa karibu na mume inaleta uhusiano mwema
 
Siruhusu hata kwa dawa mwanamke kumchukua mwanangu labda awe mdogo kisheria. Pili siruhusu kamwe mawasiliano na mtoto ili nisimlaumu katika makuzi na malezi. Ila akiwa mkubwa namruhusu aende hata akimjengea ghorofa hainihusu, nimeishatimiza wajibu wangu.
 
mwanamke ni adui yako?
 
kuepusha hayo yote oa uliyempa mimba, kama huna mpango naye acha mawazo ya kuzaa naye
Ujana ni umri wa makosa na makosa hayo ndio ambayo huwapa watu uzoefu wa maisha so jamaa inaonekana anayo nia njema ya kutokutana kuvunja hiyo ndoa ndio maana anaomba ushauri kwa watu wenye uzoefu hapa so kuliko kumlaumu kwenye makosa ambayo tayari yameshatendeka nadhani ni vyema apewe uzoefu kwanza wa namna ya kufanya.
 
Taabu kweli kweli. Mimba umpe wewe, mtoto wa kwako ila ndo hivyo kuna mwanaume anakuamulia unamuonaje mwanao.

Njia nzuri ni kuwa na dalali.

Mtoto ana bibi, mjomba, shangazi n.k mmoja awe ndo dalali wa mawasiliano.

Mfano, baba unataka kumuona mtoto, mpigie dalali shangazi au dalali yoyote anayeheshimika na baba mwenzako yeye ndo awasiliane na mama mtu, mama mtu awasiliane na mumewe ambaye ni baba mwenzako, dalali aruhusiwe kuja kumchukua mtoto umsalimie.

Ukikosea kidogo ukajifanya mwamba ndo umevunja ndoa na utamlea wewe huyo mwanao aliyekushinda mpaka uruhusu akalelelwe na baba mwingine.
 
M
Kabisa hata kule shuleni kwenye sherehe za shule anaenda huyo mume wa mzazi mwenzangu na panapotokea shida hunipigia simu kuniarifu maendeleo
Mkuu unatoa huduma hewa bora husitoe pesa kabisa kwanini mtoto wako anakua kama mmechangia kumzaa na huyo Jamaa yani yeye ndiyo ana kuongoza, Mimi niliachaga kutuma pesa za mtoto wangu kwa Mama yake kwasababu yeye huyo mzazi mwenzangu kumbe alishaolewa bila mimi kujua na akawa ana taka niwe natuma pesa kwa mwanangu tu na alikua hataki Ndugu zangu wapajue mtoto anapoishi na hataki nijue mtoto anaishi kwenye mazingira gani yeye anachotaka ni tume pesa tu, Baada ya kuchunguza nikaja kujua kaolewa na ana mtoto mchaga kwahiyo pesa ninazo tuma za mwanangu anatumia kwa mtoto wake na mume wake uchumi wake siyo mzuri! Nikawaza sasa nikituma pesa za mwanangu kila baada ya siku moja ale Maziwa mayai na nyama, Samaki je atapikiwa na je kama atapikiwa anaishi nyumba ya watoto wangapi isijekua wanaishi familia kubwa ya watoto wengi akipikiwa maziwa na mayai wanagombania.
 
Suala lako na langu ni tofauti,mimi na huyo mume wa mzazi mwenzangu,tunazungumza kila kitu na kika nachofanya nakifuatilia na hakuna kinachoharibika na kwa taarifa yenu nyote huyo jamaa ni msomi na ni mtu mwenye pisa hivyo hachukui hata senti ya mtoto
 
Ramli chonganishi hizi
 

Tunaheshimu ndoa za watu kwa kuwasiliana na kupata ruhusa kwa waume zao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…