Wanaume na wazazi wenye watoto wa kiume, hii imeshawahi kuwatokea?

Wewe uliyepata malezi mazuri, wakati unakua mahusiano yako na baba yako yalikuwaje.
Ulikulia nyumbani kipindi cha balehe au walikutupa huko shule za bweni?
Kwa mimi binafsi japo haukuniquote, mshua alikuwa ni mkali balaa! Ni kutii sheria bila shuruti..so boarding ndio lilikuwa kimbilio la kwenda kufanyia karaha za balehe...ktk kipindi hicho pia shida zenu na malalamiko yote tuliyapitishia kwa mama.
 
Asante sana, nashukuru kwa kushare experience yako.
Nimeyachukua yote πŸ™
 
Umeua mkuu, shida yao hawa wanaleta demokrasia kwenye kila kitu. Uzungu mwingi kuzidi wazungu wenyewe.
 
Kama wamerithi kwa asilimia kubwa basi inahitajika hekima sana kuvuka kipindi hicho, unapaswa uendelee kuwa katikati yao hasa kwa watoto kuwafundisha mipaka yao kama watoto.

Wanapaswa wajue kipi cha kufanya na kipi sio cha kufanya hata kama wakiwa wamekwazika. Vinginevyo wanaweza kujiharibia mahusiano yao na baba yao kwa miaka kadhaa mpaka pale watakapokuwa wamepata utambuzi wa waliyokuwa wakiyafanya kuwa sio sahihi na wengi wanakuja kutambua hayo 27+ na pengine ikawa too late.
 
πŸ˜‚ Watoto wa nyoka ni nyoka, sasa hivi unavyopambana na wanao bila shaka unaheshimu zaidi jitihada za wazazi wako kwenye malezi.

Mimi huyu baba wa wanangu ni mpole ila ana misimamo na hasira za haraka haraka akikasirishwa. Na watoto wake ni hivyo hivyo, kila nikiwaangalia naona kabisa baba amejicopy na kujipaste. Japo hawana ukorofi wala tabia za hovyo mtaani wala shuleni, hapo tunashukuru Mungu.
 
It's good if it worked then and it's working for you now.
Safi sana πŸ™ŒπŸ‘πŸ™
Kabisa mkuu, utamaduni wa kula pamoja chakula cha usiku unasaidia sana. Baada ya chakula cha usiku tutapiga stori mbili tatu na kama Kuna concern yeyote itajadiliwa halafu tunasambaratika. Dinner ni sehemu ya muhimu sana kwetu.
 
Asante kwa ushauri.

Ni kweli kabisa wanatest mipaka na baba anasimama mahali pake ndiyo maana uhusiano unayumba.
Zamani walikua wanafanya kila kitu na baba yao, weekend wanatoka, wanaenda michezoni etc. Kwa sasa hawataki kabisa, chochote kinachomhusisha baba yao hawataki kushiriki unless ni shughuli ya familia au jambo la lazima.

Ni uooga uliojawa na elements za chuki, na mimi hali hiyo inanisumbua kidogo.
 
Kabisa mkuu, utamaduni wa kula pamoja chakula cha usiku unasaidia sana. Baada ya chakula cha usiku tutapiga stori mbili tatu na kama Kuna concern yeyote itajadiliwa halafu tunasambaratika. Dinner ni sehemu ya muhimu sana kwetu.
Sisi tunakula pamoja pia, ila watoto haowaongei chochote (au wanaongea kidogo sana, wakiulizwa kitu wanajibu ila hakuna story) na wakimaliza kula wanaomba kuondoka mezani πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”

Nikiwa nao peke yangu wanapiga stori mpaka basi, baba yao akiwepo wanakua mabubu.
 
Ni kweli nauona kabisa ule msemo wa "mafahari wawili hawa hawakai zizi moja"
Baba na mtoto hata siku moja hawawez kuwa mafahari wawili hata siku moja.
Nimekua nikimuheshimu mnoo mzee wangu na kumsikiliza kwa kila jambo.

Nimeanza kwenda tofauti (mara chache) na misimamo ya baba angu baada ya kuwa na familia ya watoto wanne, hapo ndipo kuna mambo atasema nami kwa hekima nitakataa kukubali.

Nafikiri suala ni malezi.
Lakin kwa hatua hiyo walipofikia, baba akae chini na vijana hao, awaeleze. Waijue mipaka yao na kufaham kwa makini nafasi zao wao kama watoto na yeye kama baba yao ambapo nafas yake kamwe haiwez kuwa challenged katika dhana kwamba hata kama wao ni wanaume, ila hawatakaa waweze kuwa baba kwa baba yao. Hawawez kuwa mume wa mama yao.

Awaeleze wazi namna dunia kiuhalisia ilivyo mbali na illusions ambao wanazizi grab huko mitandaoni na kwenye jamii.

Mzee asipaniki. Hawez kushindan na watoto wake, awaeleweshe kwa umakini. He should act as an eye for them kwa kuwaonyesha mambo ambayo wao katu hawayaoni kwa sasa
 
NNi

Ni kawaida hutokea pale baba anaponirekebisha kila kitu huku najiona kukijua zaidi yake, nilimsumbua hicho Kipindi.

Now mdogo angu anamsumbua nimerudi nimemwambia aniachie namuelekeza taratibu.

#nrne
Asante kwa kushare.
Labda itakua hivyo pia kwetu, huyu wa kwanza akipita kwenye balehe atatusaidia na mdogo wake.
 
Kabisa.Yule mama yangu,alivyokuwa akinikung'unta hadi na mche wa kutwangia viungo nilidhani ananionea muda ule.Yaani unabondwa hadi unahisi kufa kufa mixer kiu Kali hata ukipewa sifongo unakunywa bila shida.Siyo kama hawa watoto wetu wa siku hizi wakiguswa kidogo tunapelekwa kwa mwenyekiti au mahakamani.Aiseee,alifanya jambo zuri sana kuninyoosha.Hawa watoto wetu tusiwachekee.Kipigo kwa kipimo,kiasi tu tusipite Akili zizidi nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…