nachukia mtu umekutana nae dakika chache za story anauliza unaitwa nani? kaomba namba ya cm, dakika sifuri kauliza unaishi wapi? unafanya kaz gani? 😂😅 yaaan sikuzote ukitaka uonekane mpumbavu useless uwe na tabia hizo...
Kawaida kumjua mtu jina na kuhitaji namba yake inakuja automatically kutokana na kila mmoja kuona umuhim wa mwenzake kwa wakat huo au baadae, ktk mazingira haya nyote mtajikuta mnataka kubadirishana...
Ukiona umekutana na mtu ktk maongez na story za hapa na pale ukajiona wewe ndiye unahitaji sana kumjua jina na namba yake, nakushauri mwisho kabisa wa maongez ktk kuagana anza wew kujitambulisha unaitwa nani unatokea wapi au unaishu gani mjini. Halafu muache yeye aamue kujitambulisha jina lake na akiishia kutaja jina tu usimuulize unaishi wapi au ana mishe zipi mjini, kuishia kwake kujitambulisha jina pekee maana yake hataki au hapendi shobo, kwahio muage ondoka... Ila ukiona na yeye kajitambulisha jina lake na sehém anayoish au kaz anayofanya basi hapo unaweza kumuomba na namba yake...
All in all usiendekeze shida zako kwa mtu ili ufanikiwe kupata connect za maisha.