Nimesoma malalamiko mengi ya wanaume JF kuhusu wanawake,naweza kusema kuna aina ya watu wanne humu,masculine men,feminine women,masculine women na feminine men.
Battle zikianza masculine men na feminine women wanakua Team moja ya kushambulia,kwenye defense Masculine women na feminine men wanakua team moja..
But with all that sijawahi kuona mtu aki address mzizi wa tatizo or kutojua malalamiko yanasababishwa na nini(as I see it)..
Let's assume wanawake ambao wanalalamikiwa ni hawa modern women wenye miaka 20-35
Karibu miaka 40 sasa Tanzania kuna asasi nyingi za kumkomboa mtoto wa kike,mafundisho,semina,vijarida,NGos and all that yote kubadili makuzi ya mtoto wa kike,mtazamo na kumjengea uwezo binti
But mtoto wa kiume kaachwa vilevile,mitazamo ileile,jadi zilezile,tamaduni zilezile ambazo karithishwa na babu zetu or kaona kwa mama yake na baba yake
Mtoto wa kiume wa aina hiyo akikutana na mwanamke ambae ana mtazamo tofauti unafikiri wataelewana?Lugha gongana kichwa lazima kiwake moto..
So watoto wa kiume inatakiwa nao lazima wafundishwe dunia gani tupo nayo this is not 1960s mambo yamebadilika kama sivyo tuendelee kulazimisha visivyoonekana.
Kuna Youth Organization inaitwa TAMASHA walikua wanasaidia vijana hasa mabinti wasiojiweza kujikwamua kiuchumi,kuna dada alisaidiwa na mzee wangu(friend)alipo kua financial independent tu binti alisema
"Asante Mungu sina haja tena ya kua na boyfriend "