Mmmmmmhmn kwa wanawake wa kaskazini akitulia labda aone una mtonyo na mambo yanakwenda. Na hapo anakuwa anakulia timing awe anakuibia na kujenga kwao kisiri, huwa hawana amani hadi ajue aidha ana nyumba yake au ile mliojenga ipo kwenye umiliki wake.
Wapo very obsessed na kumiliki mali na pesa zake personal tabia ambayo ni mbaya sana kwenye mahusiano na ndicho chanzo cha migogoro.
Mwanamke akishakuwa na falsafa ya kumiliki mali yake ndani ya ndoa tayari anakuwa amembolea utengano kati yenu na huwezi muamini wala kumpa nafasi ile ya nusu yako au msiri wako maana utamuamini vipi mtu ambaye anajitafutia mali zake katika mali zenu.
Na hii sio kwa wanawake tu hata wanaume. Nina shangazi yangu alifunga ndoa na mwanaume wa kichagga jamaa alikuwa akimpa hela mfano 50,000 ,laki, anahesabu kamkopesha na huwa anaidai maana hachukulii kuwa yule ni mke na kumpatia ni kama amejipa mwenyewe yeye anaidai na anakomaa alipwe.
Ila yeye alikuwa akiomba pesa anakausha kulipa sasa huu ni ubinafsi ambao unatakiwa kukemewa sana kwenye mahusiano na ndoa ama sivyo nyingi zitafika mwisho. Kwani kuna ubaya gani ukishare pesa na mali na mwenzako na mkaweka mbali ndugu zenu ambao wanazishobokea?
Kwann sifike mahali watu wakaheshimu na kuyatunza mahusiano kuliko kitu chochote wanapokuwa pamoja.