Wanaume wa enzi hizo mpo bado au yalishawafika? Tujuzane!

Wanaume wa enzi hizo mpo bado au yalishawafika? Tujuzane!

Zamani wanaume wenye familia tulikuwa tunanunua vitu kwa jumla, mchele kilo 50, unga kilo 25, sukari kilo 25, mafuta ya kula lita 20, sabuni kiroba kizima, sabuni carton nzima, ges mtungi wa kilo 30, nk, nk na mambo yalikuwa shwari kabisa familia haina shida.
Mkuu zamani kulikuwa na ges au unazungumzia zamani ya mwaka gani?
 
Hyo tag juu sikuiona my dear...pole sana aiseee...una stress ya nini sasa...acha stress maliza dose kunywa maji mengi...lala kwa wakati...halafu uje unambie tena kama stress bado zipo nikupe ushauri
Stress za upweke na kazi nyingi i guess dose inakaribia kuisha i feel better now Asante bestie wangu kwa kunijulia hali

Be blessed 🤗❤️🐰
 
Zamani wanaume wenye familia tulikuwa tunanunua vitu kwa jumla, mchele kilo 50, unga kilo 25, sukari kilo 25, mafuta ya kula lita 20, sabuni kiroba kizima, sabuni carton nzima, ges mtungi wa kilo 30, nk, nk na mambo yalikuwa shwari kabisa familia haina shida.

Sasa jifanye unanunua vyote hivyo ndo utakuwa mwanzo wa kuua familia maana wanawake wa siku hizi Ukifanya hivyo huyo mama ataenda mtaa wa mbali na kufungua genge au duka na kupiga nusu ya kila kitu na kuanza biashara! Ziko familia nyingi zimeshindwa kuvuka baada ya mume kugundua 😣
Familia kufanikio inategemea aina ya mke uliomo ndani mo
 
Wanawake wa siku hizi wamejiingiza kwenye tamaa za mamikopo na mamichezo yanayohitajia pesa kila muda....hivyo ukiwa mtu wa kurundika mahitaji ndani anajua Kodi ya meza itakuwa ya kubembelezana hivyo itakwenda kinyume na mipango yake.......

Wewe unajaza vitu vya muhimu ndani kwa manufaa ya familia yeye baada akupongeze ndio kwanza ananuna.....
 
Haya masimango wanayo Vijana wa miaka hii pekee

Sisi enzi zetu mwaka 47 hatukuwahi kuwa na masimango Kwa Bibi zenu, ndiyo maana tumeendelea kudumu pamoja hadi tumezeeka sasa 🤗
💐🥰
Ongeeni na vijana jamani, kama ugali nao ni kitu cha kumsimanga mtu ni heri wabaki kuishi kwao
 
Back
Top Bottom