Wanaume wa siku hizi ni waoga kueleza hisia zao

Wanaume wa siku hizi ni waoga kueleza hisia zao

Ni kweli! Vijana wengi wa siku hizi ni waoga. Siku hizi wametuiga wanawake kuonyesha kwa vitendo kuwa nakupenda lakini jiongeze mwenyewe mimi sikuambii.

Wanajipitishapitisha, kucheka hovyo, kutuma msg kila mara.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbona wengine tunatongozwa live, hadi aibu tunaona sie? Hao unao wazungumzia wee wa wapiii?? LOL
 
Ni wewe tu ndo hatukufati sasa mtu una uzoefu wa kuelezwa hisia na wanaume wa enzi hizo bado tu unataka hadi wanaume wa sasa tukufate kukueleza hisia zetu je kama hazipo
 
Unaeleza hisia zako baada ya masaa machache,mtu anakuwa anadaiwa kodi,kioo cha simu kimevunjika anataka simu mpya,Anaumwa,anasikia njaa,viatu vyake vimeharibika, kila siku hana bundle.Hapo bado hajakuambia pesha zake za vikoba na mchezo ambao ana majina matatu, ndio maana sometimes tunakulaga buyu ili kuepusha stress husizo plan.
Kuna kadada nimejilipua kwake kakaniambia nitakupa jibu. Kesho yake asubuhi naambiwa pasi imeungua nikasaidie hela kanunue. 25K.
Nikasema tayari yamenikuta ya wanajf
 
Ni waoga kuwaface live wanawake na kuwaeleza hisia zao.

Tofauti na zamani, angalau wengi walikua brave pia tech haikuwa kubwa na Pana kama leo. Upo Dar unaelezea hisia zako kwa binti yupo Iringa au hata Marekani. Lakini zamani unam-face mpaka kieleweke.

Siku hizi kizazi hiki ujasiri Ule hawana tena.

Ishukuruni technology.
Kumbe wewe Ni wazamani. Endelea na mapenzi ya kizamani. Siku hizi pesa inamaliza kila kitu. Mabinti wa kileo hawataki longolongo.
 
Shida ni nyinyi wenyewe. Ukishatongozwa na kikaeleweka unaanza kupata matatizo muda huo huo.
Kodi inaisha
Unaibiwa iphone
Unapata mgonjwa ambaye inabidi usafiri ukamuone
Mjomba anameza shoka nk nk.
Sasa hawa vijana jobless ukishamtwisha furushi la madai kama hilo nguvu ya kuwa na wewe anaitoa wapi? Hata kutongoza wanaogopa
Poleni
 
Ni wewe tu ndo hatukufati sasa mtu una uzoefu wa kuelezwa hisia na wanaume wa enzi hizo bado tu unataka hadi wanaume wa sasa tukufate kukueleza hisia zetu je kama hazipo
Ni wapi nimeandika nimeomba nifatwe
 
Back
Top Bottom