Kuna wanawake wanacheat bila hata waume zao kuwacheat. Kila mmoja afanye kulingana na nafsi yake ilivyomtuma, kesi ikiletwa mezani kila mmoja atajitetea kivyake na atahukumiwa kivyake. Tusihalalishe kosa la mwanamke kwa sababu mwanaume pia amefanya. Mbona kwenye mema hawalipizi iweje kwenye mabaya tu, mbona sisi tunawapa hela lakini wao hawatupi? Kama wanataka twende sambamba kwenye kila kitu na wagharamie cost za ku-mantain mahusiano kama tunavyofanya sisi bwana wako kakununulia IST na wewe mnunulie passo, bwana wako kakununulia iphone pro max 15 na wewe mnunulie samsung s23 ultra., wasiishie kulipiza kwenye ku-cheat tu.