Wanaume, watoto wako hawawezi kukugeuka ikiwa ulishiriki malezi Yao tangu mwanzo

Wanaume, watoto wako hawawezi kukugeuka ikiwa ulishiriki malezi Yao tangu mwanzo

Kila nikisikia mtu anaongelea malezi ya baba huwa nawaza sana, "malezi yake yakoje, upendo wake kwa wanawe je?" malezi yake na ya mama yana utofauti upi?
Ila ndio hivyo sikubahatika kuyapata wala kuyaona😥 RIP Baba.
Hongereni kwa kila aliewahi kupata malezi na upendo wake.
Wengine hata huyo dingi hatujui kama kafa au yuko hai.

Nadhan mfumo wa maisha hasa mjini baba harakati nyingi, kutoka kumi na mbili kurudi night kali madogo washalala, wanaishia tu kujua ni baba ila time nao hana.
Ni mbaya sana sana hii kitu, baba unakua upo kama haupo vile.
 
Huu uzi umenigusa sana,,,niliishi na wanangu miaka saba kabla ya kutengana na mama yao,,miaka minne now tunaonana vipindi kwa vipindi na sikuwahi kudhan nitakuja kuishi na wanangu wawili mbali mbali

Kubwa nashukuru kazi zangu katika miaka mitatu ya mwisho ya utengano na mama yao nilikuwa mkoani so nilikuwa nakuja mwisho wa mwezi nakaa nao siku nne kisha namsha ,kwahiyo hata ndoa ilivyokufa hawakuathirika sana kwakuwa walishazoea kutokuwepo nyumbani sana

Ila huwa tunaongea kwenye simu na nashukuru mungu niliwazoesha kuwaambia nawapenda kila ninapoongea nao basi mpaka raha,mwisho wa maongezi yetu ni love you dady,miss you dah inapendeza

Hasa wa kike ndio dady utakuja lini basi nampa sound tu ntakuja hivi karibuni si unajua mabinti na baba zao

ILa nashukuru mama yao huwapa simu waseme wenyewe wanataka nini,labda kuhusu ada ndio wakubwa wenyewe tunaongea lkn sijui study tour wanaongea nami direct,,nawapenda sana,na hakuna atakaye simama kati yao dhidi yangu

Hata kama upo mbali waonyeshe upendo wanao
Subiri wa kiume wamalize shule uone kali yake!
 
Grahams babu vipi watoto wako Huwa unafanyaje kuwaonyesha wewe ndio mzee wao
Huwa nashiriki kwenye malezi yao tangu wakiwa mimba...

Unaposhiriki malezi tangu wakiwa tumboni then hata baada ya Kuzaliwa kwao, hutengeneza bond baina yao na Mimi.

Kingine, nawajibika. Mimi ni Baba ninayependa kuwajibika Kwa malezi na makuzi ya watoto wangu. Kuwajibika huku ni pamoja na kuwafanya watoto waone hakuna Baba mzuri na anayeweza kuwahudumia Kwa chochote zaidi yangu.

Kingine wanapotaka hela ya shopping nampa Mama yao hela mbele yao

Bila kusahau kuwashirikisha Mipango yetu ya maendeleo. Mfano Kuna Kiwanja nataka kuanza Ujenzi huwa nawaambia.

Nikiwa napitia kipindi kigumu cha kifedha, huwa nawaambia na huishia kuniambia Baba tunakuombea uwe na hela kama Jana 🤗🙏🙏
 
Subiri wa kiume wamalize shule uone kali yake!
Unataka kusema atanimind,,,nadhan inategemea na malezi ya mama yao,lakini mama yao yupo smart sana na anajali makuzi ya wanae,,,wamama wabaya ni wale ambao wanapandikiza chuki kwamba baba yenu mbaya na mambo kama hayo
 
mimi mzee hata kula nae meza moja ni kipengele.. sijui alikua na shida gani mbinafsi balaa
Mi mzee alikuwa sio mbinafsi, ila akianza kutoa kichapo utatamani kuhama maskani. Ukizua mambo ya skuli akikupeleka anakusulubu mboko mpaka waalimu wanakuombea msamaha hata kama ilikuwa wakuadhibu.
 
Huwa nashiriki kwenye malezi yao tangu wakiwa mimba...

Unaposhiriki malezi tangu wakiwa tumboni then hata baada ya Kuzaliwa kwao, hutengeneza bond baina yao na Mimi.

Kingine, nawajibika. Mimi ni Baba ninayependa kuwajibika Kwa malezi na makuzi ya watoto wangu. Kuwajibika huku ni pamoja na kuwafanya watoto waone hakuna Baba mzuri na anayeweza kuwahudumia Kwa chochote zaidi yangu.

Kingine wanapotaka hela ya shopping nampa Mama yao hela mbele yao

Bila kusahau kuwashirikisha Mipango yetu ya maendeleo. Mfano Kuna Kiwanja nataka kuanza Ujenzi huwa nawaambia.

Nikiwa napitia kipindi kigumu cha kifedha, huwa nawaambia na huishia kuniambia Baba tunakuombea uwe na hela kama Jana 🤗🙏🙏
Wewe ni baba Bora sana
Waje wachukue notes hapa
 
Duh! Stori za humu zinanitisha.

Mimi baba yangu alitujali sana. Anatupeleka shule na gari yake na kisha anapitia kazini kwake.

Muda wa kurudi nyumbani dereva wake anatufuata au tunarudi wenyewe. Wakati wa kula familia tunakula pamoja mezani na mzee alikuwa na tabia kama mboga (nyama) mama alikuwa anamwekea za kwake maalumu. Baba yetu alikuwa anatoa za kwake na kutugawia tena sisi watoto. Mama utamuona anamwambia sasa wewe utakula nini? baba anamwambia; waache bhana watoto hawa.

Siku ya jumamosi na jumapili muda wa jioni anakaa na watoto wake ana kaa karibia na eneo la parking kuna mahali pa kupumzika tunakaa tunapiga naye stori.

Muda wa mpira tunaangalia naye wote. Nilikuwa namtania nacheka kama yeye anavyocheka ataniangalia basi mama atacheka mpaka bhasi!

Kwenye mipango yake ya biashara alitushirikisha. Kwa ufupi alitujali sana! Yeye na mama walitujali sana na tulipokesea waliturekebisha.

Kwa sasa nina umri wa miaka 31. Baba yangu ameshatangulia mbele ya haki. Kila siku kila baada ya swala huwa namuombea kwa Mungu. Na kila baada ya wiki moja au mbili huwa nafanya dua maalumu ya kumuombea.

Nawapenda wazazi wangu wote wawili. Na huwa sipendi kabisa kusikia mama yangu ana tabu. Akiwa na changamoto yoyote chapu kwa haraka naishughulikia.
 
Haha pole sana siis tumeenjoy kweli lazima jioni tule nae
Tena mama akiwa amesafir anapanga ratiba ya kupika mm nilikuwa mpishi wa mboga
Yeye wali au ugali mdogowangu muandaaji wa vyombo
🤣🤣Ila ugali wake kula uwe Mwana mazoez unakuwa mgumu balaa🤣🤣
Sisi baba yetu siku za jumamosi au jumapili asubuhi utamuona anatengeneza mkate wa kukaanga ana kaanga na mayai. Basi mama anamwangalia tu!

Utamsikia baba anasema hii ni tamu sana! Halafu anaonja mwenyewe utamsikia ewaaaa! Hii safi kabisa! Mtaipenda.

Kingine amenifanya kwenye chai au uji naweka asali badala ya sukari. Ndiyo ilikuwa tabia yake sukari kwake hapana.
 
Kila siku nashukuru kwa kuwa na baba huyu niliyenayee, huwa nawaza je angekua mwingine ingekuaje kwa upande wangu?

Baba angu nampenda kuliko chochote, nae ananipenda na ananithaminiii, Nafurahia uwepo wake na aishi miaka mingi zaidi ili niendelee kufaidi matunda yakee.

[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Natumain mna afya njema
Kuna namna malezi yanakuwa magumu Kwa walezi wa kiume hasa kubadilisha fikra za watoto wao na kuthaminika Kwa watoto wao japo walijitahid kufanya hivo ila hawakuzngatia code

Kiukweli mm ni miongoni mwa watu ambao huwezi kuniambia chochote kibaya kuhus babaangu nikakuelewa Kwa sabbu nimekuwa katika hali ambayo namuona akiwa anahangaika kwaajili ya yangu na familia yetu

Ngoja niwape mambo hapa machache

Kwanza jitahidini kuwa karibu na watoto wenu wawaone mnashiriki kikamilifu kwenye ukuaji wao kuanzia kiimani na kiakili baba jitahid kuwa rafiki Kwa mtoto kwenye nyakati zote

Watoto wakiwa wadogo hujifunza sana Kwa kuona kilakitu kutoka Kwa wazazi
Akikua akiwa hakuoni na uko hai ni mbaya hata kwenye ukuaji hawezi kuelewa hata kama ulipambana huko nyuma ya pazia onyesh upendo wa wazi nae ataishi hivo hivo ukubwani

Kuna kutofautiana Kwa wale ambao wako mbali na watoto acha kumtumia mama kufikisha ujumbe Kwa mwanao Kila mara labda kama ni mdogosana
hakikisha unawasliana na anakuwa uhuru kusema kinachomsumbua aone wewe ndio babayake halisi hata uwe umbali mara elf 5 inaongeza upendo Kwa mtoto

Shiriki matukio ya furaha na wanao tenga muda wa kuwa nao pamoja hata mara chache kuongea nao na kufurahi

KWANGU

Kila kitu kilikuwa wazi tunajua nani ni kichwa Cha familia,akosi chochote Cha kishiriki na watoto kama ana nafas atakuita hata mbrash viatu vyake
bond Ilikuwa Bora sana

Hakutaka kumtumia mama aseme chochote Zaid tulikuwa tunawasiliana moja kw moja hafanyi chochote Hadi neno litoke kwangu direct na atanipa majibu mwenyew pia

Hakuna anaweza kuniyumbisha kuhus kumpenda Wala siwez mkubaliana mtu akisema alikuwa mbaya hata mama siwez muelewa
Jitahid kuwa karibu na kishiriki malezi acheni kuona nyie sio wahusika kwenye kuwajenga watoto wenu

Nimeongezea na kavideo hapo chiniView attachment 3038392
Thanks for sharing madam, kuna vitu nimevinote nitavi apply..
 
Sisi baba yetu siku za jumamosi au jumapili asubuhi utamuona anatengeneza mkate wa kukaanga ana kaanga na mayai. Basi mama anamwangalia tu!

Utamsikia baba anasema hii ni tamu sana! Halafu anaonja mwenyewe utamsikia ewaaaa! Hii safi kabisa! Mtaipenda.

Kingine amenifanya kwenye chai au uji naweka asali badala ya sukari. Ndiyo ilikuwa tabia yake sukari kwake hapana.
Mungu amtunze sana 🙏
 
Kila siku nashukuru kwa kuwa na baba huyu niliyenayee, huwa nawaza je angekua mwingine ingekuaje kwa upande wangu?

Baba angu nampenda kuliko chochote, nae ananipenda na ananithaminiii, Nafurahia uwepo wake na aishi miaka mingi zaidi ili niendelee kufaidi matunda yakee.

[emoji120][emoji120][emoji120]
Kma nakuona unavodekaga 😃😃
 
Wale wanaodanyana kwa harakati uchwara za KATAA NDOA waisome
 
Usiongee ukamaliza
Hizi fikra mimi nazikataaga

Kupata watoto wema ni tawfiq ya Allah kwa hiyo Allah anawachagulia watu fulani wawe na watoto wabaya na wengine wawe na watoto wazuri ?

Hizi ni itikadi zisizokuwa na mashiko kabisa ambazo binafsi nazipiga vita,LAZIMA UFANYE JUHUDI NA UTUMIE AKILI ALIYOKUPA ALLAH KULEA WATOTO.

Kulea sio kupeleka watoto shule na madrasa pekee,kulea kuna mambo mengi na ukiyakosea lazima upate toto ovu na wala jambo hilo halihusiani na tawfiq ya Allah.

Tunamsingizia sana Allah kwa mambo ambayo yapo mikononi mwetu.

وما أصابكم من مصيبة فبما كسبت أيديكم ويعفو عن كثير

[ ASH-SHUURA - 30 ]
Na misiba inayo kusibuni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye anasamehe mengi.
 
Moja; usiongee neno haiwezekani...
Mbili: Kukugeuka ni nini ? Huenda kuna watu wanataka vitu zaidi sababu tu by proxy fulani ni baba yake.., kwahio kama alifanya wajibu wake hata kuhakikisha tu unapata chakula and roof over your head without extras kama una kitu between your ears inabidi ushukuru (mfano huwezi kusema mama yangu alikuwa mkali na hanipendi wakati angeweza kutoa mimba au kukutupa ukiwa mdogo na hakufanya hivyo)
Tatu: damu nzito kuliko maji binafsi hata kama mzazi alikuwa mkali na mtukutu lakini bado tampa nafasi ya mzazi haijalishi sababu hakunipa extras au angeweza kunipa extra na hakufanya hivyo...

Mwisho kabisa nakuacha na hii story ya jinsi mtoto alivyomzira baba yake sababu kwenye birthday yake alimpa zawadi ya bible na sio Ferrari (might be a made up story lakini ni plausible)
Shukrani mkuu
Kumradhi km neno haiwezekani huenda nimelitamka sehemu isiyo sawa
Kukugeuka nimemaanisha kwenda kinyume na wew lakin pia sikumaanisha ni Kwa watu wote Iko hivo inategemea na moyo pia wa mtoto hakuna mzazi asiempenda mwanae ila changamoto ni kuwajibika na kusimama km baba
Fuatilia watu wengi tunajifunza tukiwa wadogo sana na chanzo Huwa ni familia,shule na vitu vingine ni ziada ila Huwa tunajifunza kuanzia nyumbni
Mtoto aliefanyiwa ukatili akiwa mtoto kuwa mwema ni kitu kigumu

Mtoto alieonyeshwa upendo kuwa na upendo ni rahis japo pia sio wote pia
Ukimkuta mtu hajali chochote kuhusu wengine ukimuuliza sabbu hawez kukosa kusema nae hakuthaminiwa hivo Hainamaana kujali
 
Back
Top Bottom