Wanaume wengi hufa kabla ya wakati wao kwa sababu ya laana kutoka kwa wazazi

Wanaume wengi hufa kabla ya wakati wao kwa sababu ya laana kutoka kwa wazazi

Unachekesha,

Ndio ninyi mko dar mkiulizwa kuhusu walipo wazazi wenu mnadai walishafariki,

Kumbe wapo hai na wanapitia moto hatari.

Malipo ni hapa hapa, Wana wenu watawalipeni.
Unijui lakini umeshajua wazazi wangu Kama wapo hai au wamekufa. Hongera sana
 
Mkuu kile kitendo ya mzazi kutamka maneno mabaya kama unavyoita laana , wewe ukiamini haya maneno na ukawa na mashaka yatakutokea kama yalivyo , hiyo ni law of attraction na maumbile yanavyofanya kazi kulingana na fikra zetu.

Bila hata laana mambo yako yana weza kwama sana , kutokana na unavyofikiri na kuchukua maamuzi na hata mda mwingne hisia zako zinaweza kuathiri matokeo.

Jinsi tulivyo ni matokea ya fikra zetu hasi au chanya .

Ukijenga fikra wanaume tunakufa mapema kwa sababu hatusaidii wazazi ,utakufa kweli kwa fikra hizo ukienda kinyume.

Na sio kwa sababu eti umepata laana kutoka kwa wazazi.

Katika kitu cha kuchunga sana ili kupata matokeo chanya kwa yale tunayotarajia ni kuchunga fikra zisiharibiwe.

Kwa sababu kanuni inasema fikra ikiharibika, hisia na mienendo na matokea huwa hasi .

Ndio maana matajiri hupenda kuweka makazi yao mbali na maskini na watu wenye fikra duni ili kulinda fikra zao kwa sababu fikra chanya ndio hazina.
Wapo matajiri wa mchongo wasiojali wazazi wao,

Ni Kweli msoto maishani una vyanzo vingi, ila ni UKWELI usiopingika kuwa kutowajali wazazi ni chanzo mojawapo kikuu Cha changamoto tunazopitia.

Ubarikiwe.
 
saanyingine nikikaanikifikiria najilaumu sana kuzaliwa aisee.

hadi umuabudu mtu ndio upate baraka☹️☹️?

wengine bado hatakazi zakueleweka hatuna kula yenyewe shida hao wazazi utawasaidiaje sasa?
Muhimu ni kutowasahau,

Washirikishe wakuombee na washirikishe katika Kila Hali.

Pia usisahau Kutoa ZAKA ,sadaka na matoleo Kwa Kila kidogo ukipatacho utabarikiwa.

Amen
 
Wapo matajiri wa mchongo wasiojali wazazi wao,

Ni Kweli msoto maishani una vyanzo vingi, ila ni UKWELI usiopingika kuwa kutowajali wazazi ni chanzo mojawapo kikuu Cha changamoto tunazopitia.

Ubarikiwe.
Ni kweli kabisa kama utaamini hivyo, ila kuwatelekeza wazazi sio jambo la busara na pia sisi kama wazazi tujipangae badae tusije lialia tukitegemea laana, kwa sababu pia laana hutoka kinywani mwa maskini.
 
Uko sawa kabisa,

Maana pia haiingii akilini mtoto awe tajiri mzazi akose hata sabuni ya kufulia, ilhali upande wa wazazi wa mke wako njema kupitia mkeo!!

Huo nao ni utajiri wa mashaka!!
 
Uko sawa kabisa,

Maana pia haiingii akilini mtoto awe tajiri mzazi akose hata sabuni ya kufulia, ilhali upande wa wazazi wa mke wako njema kupitia mkeo!!

Huo nao ni utajiri wa mashaka!!
Ni sawa mkuu ,ila mkuu hakuna utajiri wa mashaka utajiri ni utajiri tu .
 
Ni sawa mkuu ,ila mkuu hakuna utajiri wa mashaka utajiri ni utajiri tu .
Utajiri wa mashaka upo,

Haiwezekani uwe na nyumba ya ghorofa halafu uwe unalala chooni!!

Pia Kwa kuishi kwangu kwingi, nimeiona matajiri "WAPUMBAVU" wengi Si haba!!
 
saanyingine nikikaanikifikiria najilaumu sana kuzaliwa aisee.

hadi umuabudu mtu ndio upate baraka☹️☹️?

wengine bado hatakazi zakueleweka hatuna kula yenyewe shida hao wazazi utawasaidiaje sasa?
Walimie Shamba au wafulie nguo zao.
 
Rabbon hebu hariri mada yako unganisha na para kutoka eneo hili hapa Mwanzo 2:24 na Marko 10:6-8, then tuendee na mjadara maana nashindwa kureply!.
 
Utajiri wa mashaka upo,

Haiwezekani uwe na nyumba ya ghorofa halafu uwe unalala chooni!!

Pia Kwa kuishi kwangu kwingi, nimeiona matajiri "WAPUMBAVU" wengi Si haba!!
Kama upo utajiri wa mashaka basi pia upo umaskini wa mashaka ,hizi stories za matajiri kulala chooni zipo kwetu Africa tu.

, japo ni fununu tu hazina udhibitisho wa moja kwa moja , ila matajiri wengi wakubwa ukikaa nao hizi stori huwez zisikia.

Habari nyingi za mataji utazipata kwa maskini ,tena waliokithiri.
 
MAISHA hayana laana Binadamu Hana Huwezo wa kumlaani Mtu yoyote wanaume hufa mapema kutokana na Kazi ngumu na stress za wanawake plus Majukumu.
 
Kama upo utajiri wa mashaka basi pia upo umaskini wa mashaka ,hizi stories za matajiri kulala chooni zipo kwetu Africa tu.

, japo ni fununu tu hazina udhibitisho wa moja kwa moja , ila matajiri wengi wakubwa ukikaa nao hizi stori huwez zisikia.

Habari nyingi za mataji utazipata kwa maskini ,tena waliokithiri.
Huo ndo. Ukweli matajiri wanapambana Sana wanwekeza Akili Yao katika kutafuta maokoto

Uchawi upo ila hauna Nguvu za kukupa maokoto Kama ya Bakhressa
 
Huo ndo. Ukweli matajiri wanapambana Sana wanwekeza Akili Yao katika kutafuta maokoto

Uchawi upo ila hauna Nguvu za kukupa maokoto Kama ya Bakhressa
Hiyo akili kubwa ya kuona fursa na kuzitendea kazi ndio uchawi wenyewe, ila maswala ya vibuyu na mapembe ya ng'ombe ni danganya toto tu ili uamini upige kazi bila uoga ukiamini kuna vibuyu vinakulinda .
 
INTRODUCTON.

Salaam, Shalom!!

Leo naandika mada hii nikiwa na Sina furaha sababu Mimi Rabbon pia ni Mwanaume.

Wanaume tulipoambiwa tuishi Kwa akili na wake zetu, au na wanawake ,Kuna Siri imejificha nyuma, ipi hiyo?

Under Ceteris peribus, while other factors remain constant,

Ni Kweli, wanaume wengi huoa wake wanaowazidi umri hivyo wengi wanapotangulia kufariki ndugu na jamaa hutoa sababu hii, lakini Si Kweli, IPO sababu zaidi ya hiyo.

Wanawake ujiwauliza watakwambia wti Kwa Sababu wao hawatunzi jambo moyoni na hulia machozi sana ndo sababu ya kuishi maisha marefu.

Wanasayansi wengine hudai kuwa sababu wanawake wao Wana matiti ambayo hutunza maziwa ambayo ni chakula kinachowapa kusurvive muda mrefu, hapo ni Kweli Kwa kiasi fulani, bt si sababu kuu.

Wanaume wenzangu tujiulize inakuwaje mwanamke anazaa Kwa uchungu hadi watoto 14, na wote tunajua shughuli pevu ya kuzaa mtoto ilivyo, lakini mwanamke huyo huyo utaondoka na kumwacha duniani, nini sababu? Tatizo ni LAANA hii nitakayoiongelea leo.

Dunia nzima imeweka mfumo thabiti kwamba Mali anazomiliki mwanamke ni zake pekeake, lakini Mali anazomiliki mwanamume ni za wote, Kuna kitu hapo kimejificha ambacho wanaume Bado hawajakijua kinachopelekea kuchomoka duniani mapema.

Namwongelea Mwanaume anayehangaisha KICHWA usiku na mchana kutafuta riziki ya familia na hapumziki, nini kinachomwondoa mapema?

Namwongelea Mwanaume anayevuja JASHO, anamhudumia mkewe na hawara na machangudoa na anamudu wote kuwapa mahitaji yao, kwanini anawahi kuchomoka duniani mapema?

Namwongelea Mwanaume aliyeokoka mwenye baba na mama wa kiroho, anawatunza wazazi wake wa kiroho, lakini Bado anawahi kuchomoka duniani kabla ya siku zake, nini chanzo?

Naongea na Mwanaume unayeacha Kodi ya meza Kila siku, unajibana Ili familia yako isonge, kwanini bado huna maisha marefu, ipi sababu, ni hii:

LAANA YA WAZAZI NI CHANZO KIKUU CHA WANAUME WENGI KUFA MAPEMA KABLA YA WAKATI WAO.

Wanaume wengi tumelisahau hili.

Kwani hamkusoma maandiko katika Amri ya Mungu isemayo,

"Waheshimu baba Yako na mama Yako, Ili siku zako zipate kuwa nyingi katika Nchi upewayo na BWANA Mungu wako"

Pia hamkusoma kuwa,

" Baba na mama (Wazazi) ni miungu wa Dunia hii?

Watu wengi hasa vijana na wanaume huangaika sana na hukumbwa na mabalaa na kufungwa vipato vyao duniani bila kujua Chanzo ni LAANA ya wazazi!!

Wakati ukiacha Kodi ya meza Kwa mke wako, atahakikisha anatenga kiasi kidogo kidogo Kila siku, Kisha hukituma Kwa mama yake mzazi.

Mzazi wa mke wako ambaye mara nyingi ni mwanamke sababu mzazi wa kiume mara nyingi anakuwa ameshaiaga Dunia, mzazi yule wa kike, huipokea sadaka Ile na kumwombea baraka aliyeitoa ambaye ni mwanae wa kike, baraka hizo hazitakufikia wewe Mwanaume sababu nawe unao wazazi wako kijijini hawana hata mia mbovu[emoji24]

Wazazi wako ewe Mwanaume wanaweza kata hata mwaka hujawatumia chochote kuwatunza, wanaishi nyumba chakavu wanalala chini, hata godoro hamna, wewe umehangaikia familia Yako wanakula na kulala vizuri, unamsahau baba na mama Yako!!

Ikitokea umeenda kijijini, utamwita pembeni mama na kumshikisha bulungutu la pesa, Kisha baba unampa pesa kiduchu ilhali ndo anajukumu kutunza familia.

Wazazi wako wanaposikia umenunua gari Kwa ajili ya mkeo kutembelea na wakisikia umejenga ukweni kwa mkeo, kinachotokea huwa wanahuzunika[emoji24]

Mama anashika tumbo na kumlilia Mungu, baba hushika kiuno na kulia, Kila Mmoja sirini Kwa wakati wake.

Ugumu wa maisha wanaume wengi tunaoupitia mijini, chanzo kikuu ni LAANA ya wazazi.

Mwaka mzima unaisha hujapeleka Kwa wazazi hata mia mbovu, lakini unapata pesa ya kuhonga MAKAHABA. LAANA inakunyemelea......

Unapomuhonga kahaba, yeye huchukua pesa hiyo na kutumia pesa kiasi Kwa wazazi wake, Kwa maana ingine, pesa yako inatumika kuwa baraka kwa mwanamke while wewe hupati kiasi cha kuchota baraka za wazazi walokuzaa.

Na wanawake ni Wachache sana ambao huwakumbusha waume zao kuwatumia chochote wazazi wa waume zao.

Mwanaume mwenzangu, hasa vijana ambao hamjaoa bado, msisubiri kupata KICHAA kitokanacho na LAANA ya wazazi wanapohuzunika Kwa ajili yetu. Msisubiri kupelekwa kijijini mkiwa katika majeneza.

SOLUTION.
1. Hakikisha unatunza Kwa Siri chochote kitu, unatumia Kwa wazazi wako kimya kimya, sababu najua wake zenu wengi Wana gubu na wasingependa mbarikiwe.

2. Pata muda wa kuongea nao hata Kwa simu na uwashirikishe changamoto unazopitia, ukijua kuwa hao ni miungu wa Dunia hii.

Wazazi wanapokuhuzunikia Kwa kutowajali wazazi, humpa KIBALI shetani kukushambulia Kwa mapigo na LAANA mbalimbali!!

3. Tafuta muda ukatubu, wajengee wazazi wako nyumba nzuri, watumie zawadi, nenda kusali lakini jua miungu mwenye FUNGUO za maisha Yako duniani ni wazazi,

4. Ishi na mke wako Kwa Akili sana, hakikisha unamzidi akili na Maarifa.

Ningeongea zaidi bt inatosha Kwa sasa!!!

Karibuni Kwa shuhuda na MAONI [emoji120].
Kwann mwanaume ujali mkeo kuliko wazazi wako, huo ni upumbavu na laana kwelikweli
 
Kwann mwanaume ujali mkeo kuliko wazazi wako, huo ni upumbavu na laana kwelikweli
Soma post no 33 ya ndugu TODAYS amequote Mwanzo 2:24 kwamba Mwanaume atamwacha babaye na mamaye na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja!!

Kwake kuwaacha wazazi Ili kuambatana na mke, ni pamoja na kutowahudumia kabisa, kwamba wapambane na Hali zao.
 
  • Kicheko
Reactions: BRB
Rabbon hebu hariri mada yako unganisha na para kutoka eneo hili hapa Mwanzo 2:24 na Marko 10:6-8, then tuendee na mjadara maana nashindwa kureply!.
(Mwanzo 2:24) na (Marko 10:6-8) says.

Mwanaume atamwacha babaye na mamaye na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Kwamba kwako ulivyoelewa, kuwaacha baba na mamako ndo kutowahudumia, kwamba wapambane na Hali zao?

Mbona hujiulizi kwann mwanamke anachukua Mali zenu na kuwatunza wazazi wake?

Naamini hujalishwa kanyama maarufu Kwa Jina " Limbwata".
 
Back
Top Bottom