Ndio maumbile Yao story na mashost saloon utasikia akipiz tu kule. Analala.
Utasikia yaani ana 48 akifikisha 50 basi tena Nitakuwa Sina mume mwenzenu
Nichangie jambo juu ya umri tendo na ndoa au mahusiano kamili.
Jambo muhimu linalobeba afya ya tendo la ndoa au mahusiano ni kujitunza kwa wote wawili mume na mke na kua ngalia nini unakula na nini unakunywa kwenye maisha kwa ujumla bila kuacha kufanya mazoezi japo kwa dakika tano kila siku au dakika 30 kwa siku mbili.
Pia aina gani ya vyakula na mafuta unatumia. Aina gani ya matunda unakula. Mfano tende, tangawizi, komamanga, tikiti maji, cantaloupe, seamoss, fenugreek powder, mtindi, walnuts, Cinnamon, shrimp, ugali, maji ya kutosha, na aina zote za wanaotoka baharini wenye Zinc.
Mapumziko ya kutosha. Mahusiano yenye afya, hivyo vyote vinafanya mwanaume uwe imara muda wote na saa zote unapohitajita na kupiga mabao yoyote yanayohitajika kwa mwanamke wako au mkeo.
Mazoezi yanasaidia kufanya mwili wako uwe vizuri kiafya kwa jambo lolote lile ikiwemo tendo la ndoa.
Lakini ulevi kutokula vizuri na kushindia chips mayai , kutokupumzika vizuri na umri unavyosogea basi hufanya viungo vingine viwe kizembe zembe...na ndiyo mwanzo wa kutosimamisha vizuri. Au kutokwenda umbali mrefu ikichangiwa na pumzi kukata mapema
.
Kula vizuri vyakula bora utaona matokeo yake.
Mimi hapo nimeweka baadhi tu ya mambo na vyakula vinavyoweza kuwafanya mfurahie mahusiano.