Wanaume wengi wanashindwa kuhudumia wazazi wao kwasababu ya vimada

Wanaume wengi wanashindwa kuhudumia wazazi wao kwasababu ya vimada

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
2,864
Reaction score
8,328
Ukweli ndio huo. Wazazi wa familia nyingi wanahudumiwa na watoto wao wa kike.

Mbaya zaidi utakuta hao watoto wa kike wana kipato duni ukilinganisha na wa kiume.

Wa kiume hela zao ni za kulisha na kunywesha na kustarehesha wanawake

Pia wanawake tunaroga sana wanaume ili tupate control ya maisha yao na hela zao
 
Lakini pia wazazi wanawajibu wa kuandaa maisha yao ya baadae kuliko kukaa na kuwalaumu watoto wao
Wazazi wametumia nguvu zao zote kuwasomesha nyinyi halafu mukipata kazi munawasahau. Yale aliyoyazungumza Mhe Mashimba bungeni kuhusu watoto yana mantiki sana ijapokuwa wabunge walikuwa wanamcheka.

Hicho kipato cha kuwahudumia nyinyi miaka miingi huwa kinabaki na ziada ya kusave kweli?
 
Mzazi unatakiwa kuandaa uzee wako, usitegemee kijana wako awe msaada wako ukizeeka. Kwa maisha gani kijana amemaliza chuo ameoa aweze kuhudumia mzazi?

Tuandae uzee wetu sasa.
 
Siyo Kwa sababu ya vimada...hao tutakuwa tunawasingizia tu.Wanaume wengi hushindwa hudumia wazazi wao Kwa sababu ya roho mbaya za wake zao.Wanaume wengi waliingia kichwakichwa Kwa wake zao Kwa kuwaamini na kuwahusisssha Kwa Kila kitu then wake zao wametumia udhaifu huo kuwabana na kukataa kabisa kuhudumia mama wa waume zao.Mungu awafungue Kwa kweli
 
Mimi huwa napenda kumuuliza mzazi wangu hili swali japo mpaka leo alishindwa kunipa majibu kabisa....wewe uliwasaidia wazazi wako kama ambavyo mimi unanitaka nikusaidie?.......mzazi wangu huwa ananikomalia nimjengee nyumba nzuri na hali yakuwa mzazi wake (marehemu babu) mpaka umauti unamkuta alikuwa anaishi kwenye nyumba ya udongo...
 
Demand changes with time and technology
 
Back
Top Bottom