Wanaume wengi wanashindwa kuhudumia wazazi wao kwasababu ya vimada

Wanaume wengi wanashindwa kuhudumia wazazi wao kwasababu ya vimada

DHANA kuu ya tunazaa watoto Ili waje kutukomboa na kutatua matatizo yetu tuiondoe kabisa bali tunazaa Ili tulelewe tunapozeeka sio kutatuliwa matatizo AMBAYO sisi wenyewe tulishindwa kutatua tukiwa vijana!

DHANA ya kutumia mapesa mengi kusomesha vijana Ili wapate kazi kubwa Ili waje watuhudumie iondoke kwenye jamii kwani elimu ya Sasa haitoi majibu au haijazi NAFASI zilizowazi za ajira na kipato tuondoe dhana hiyo!!

Watoto wasome kawaida tu tena KWA uwezo wao huku wakijamiiana na jamii Ili kuwajengea uwezo wa ku adapt mazingira halisi ya mtaani na Maisha yajayo ya kujishighulisha kuliko kulipa gharama kubwa ya shule zenye gharama kubwa huku kafungiwa kama kuku au mnyama!ni kweli atafaulu Sana lakini hatofaulu mazingira na kujitegemea na mwisho wa siku Baada ya kuhitimu atashindwa KU adapt mazingira ya kiutafutaji akitegemea ajira ambazo hazipo!na mzazi keshauza KILA kitu KWA ajili ya Elimu yake!!

Sisi wazazi tuwekeze kwenye vitegauchumi ambavyo Mtoto atashiriki kuendesha huku anasoma kumjengea uwezo wa kiakili kimazingira!!

Nafurahi Sana ninapowaona wanangu wakiuza duka na mama yao Baada ya muda wa masomo!!!

Wazazi tuwekeze kwenye vitegauchumi na sio kufanya elimu ya Mtoto Kuwa kitegauchumi wakati hailipi!!

Tumakinike!
Ushauri Bora kabisa kuusoma 2023.

Tatizo wengi wanaishi Kwa mkumbo
 
Back
Top Bottom