Wanaume wenye watoto tupeni uzoefu wenu. Mara ya kwanza unampelekea Mwanamke wako hospitali kujifungua, hiyo siku ilikuwaje?

Wanaume wenye watoto tupeni uzoefu wenu. Mara ya kwanza unampelekea Mwanamke wako hospitali kujifungua, hiyo siku ilikuwaje?

hujifungua kwa opereshen alafu mnasubiria mpaka uchungu umkamate hebu muwe mnajiongeza
Ni hivi madam kutokana na vipimo alivyofanya kulikuwa kama kuna siku nne au tano mbele kwahiyo hatukuwa na hofu yoyote ile,ila dogo tu ujuaji mwingi akaanza kutaka kuja duniani mapema,,hata hivyo baada ya kumpeleka hospitali alikuja kujifungua kesho yake alfajir
 
Wanaume ambao mnawatoto embu tupeni uzoefu wenu kwa mara kwanza unampelekea Mwanamke wako hospitali kujifungua,hiyo siku ilikuwaje na kipi utoweza kusahau kabisa
Mimi wakwangu aliniambia tutembee kwa miguuu ni Nurse mtoto alizaliwa 1989,kumbe mwanamke anapotembea anafanya mazoezi ya kukisukuma kiumbe
 
😂😂😂 huduma zote nilikua mwenyewe kama mimba nilijipea mwenyewe,, kuanzia first clinic ad siku ya kujifungua 😂😂😂😂🙌🏾🙌🏾 nashukuru tu nilitumia private hospitals.
 
Ya kwangu mimi ilikuwa experience ya kujifunza mambo mengi, ambayo mwanaume ambae hajaoa au kubahatika kupata mtoto hawezi kuyajua.

Kwanza, mimba zote za mke wangu ni zile ziitwazo risky pregnancy.YMimba ya mtoto wa pili ikibidi washone ile cervix ili kuzuia mimba isitoke. Nikapigwa marufuku kufanya chochote kinachohusisha sehemu zake za siri. Hii ilikuwa torture ya hali ya juu.. Ilihitaji nidhamu ya hali ya juu kutulia nyumbani.
Halafu tukaambiwa na daktari wake kwamba mtoto anaweza kuzaliwa mapema (premature birth) kutokana matatizo ya wife. Kichwani, binafsi huwa nahisi wife, kabla yangu, alikuwa chinjachinja sana, yaani aliabort mimba nyingi mdio maana kizazi kikatepeta) ingawa Sina uhakika na hilo.

Siku ya kwenda kujifungua ndio ikaleta mauzauza ya hali ya juu. Tulikaa hospital zaidi ya masaa 48. Njia ya kutokea ikagoma kufunguka au ikaanza kufunguka kidogokidogo. Kwa hiyo, kila baada ya masaa kadha daktari anakuja, anaingiza mkono au vidole ili kuona kama kuna maendeleo yoyote.

Kasheshe ilikuja jioni yake baada yaa shift mpya kuanza. Daktari kaingia kwenye chumba alipo mke wangu na kundi la wanafunzi.
Hiyo hospital ipo (attached na Medical School. Doctor akatufahamisha kwamba mimba kama hii ya mke wangu haziji mara kwa mara, hivyo basi akaomba ruhusa ili wale ma Medical interns wajifunze mambo ya risky pregnancy kupitia mke wangu. Nikamuuliza bibie kama yupo ok, akasema hamna tabu.

Mhhhh! Yaani, kila moja wao anavaa glove anazamisha mkono. Moja baada ya mwingine. It was the most eye opening experience kwa kweli. 15 hours later tukafanyikiwq kupata mtoto wa kike. Maisha ni safari ndefu sana. Pia, kushi kwingi huona mengi.
 
Inabidi ujipange haswa kwenye cash, endapo ikitokea ameshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida anahitaji kisu, apo mzee wangu jipange kwa gharama ..pia madakitari watakuwa wengi sana kipindi icho mzeemama anajifungua😀😀(apa ni wale majirani, ndugu, marafiki) mambo mengine ni kawaida tu kumuhudumia mzazi. Apo Sasa ndo uanaume unaonekana..😂😂😂

Siyo powa brooo
 
Unakimbilia wapi mkuu. Mimba yenyewe ilikuwa risky pregnancy, tumekaa labor karibia siku mbili, papuchi haujagusa karibia miezi mitano, unafanya mchezo kabisa.
Si nimekuambia nakimbilia hospital

Mkuu sio miez mitano, yaaan tangia Ile tu ameambiwa ni mjamzto mpaka Leo hii
 
Picha limeanza saa tisa usiku,,baby mama uchungu umempata na kumbuka baby mama wangu hujifungua kwa operesheni

So mwelekeo ni muhimbili na ndio mtoto wangu wa kwanza,nipo makazi africana mbezi,,mungu mkubwa nje kuna nissan march kadogo kadogo hivi ndio nikakapiga start hao muhimbili,,yaan baby mama anaugulia maumivu mwamba namtaja Allah kwa sana na kumtukuza atufikishe salama

Dah ilikuwa experience ya kipekee sana
Umesema ni mtoto ws kwanza na umesema hua anajifungua kwa operation,sasa ulijuaje kua ni operation na ndio kwanz mtoto wa kwanza?
 
Back
Top Bottom