Uzazi wa pili Kipindi kile corona imepamba moto 2020 ingawa ilikua vyepesi sana lakini kidogo akili iliyumba.
Uzazi wa kwanza ndio sita sahau!
Kwanza kabisa hospitali ya jirani walisema uzazi wa kwanza lazima mwananyamala ama sinza.
Nikaomba sinza tukaelekezwa maana tulikuwa wa geni dar, hatuna mwenyeji hata mmoja.
tukaenda, kipimo tukaambiwa kurudi tarehe fulani, siku hio tulivyorudi nikaambia anabaki nirudi nikaandae chakula na vinginevyo, bahati nzuri tulipewa abc za kujifungua so vifaa alikuwa navyo.
Siku ya kwaza ikakata, siku ya pilli nayo ikakata!
Nikashauriwa na daktari kwamba njia imekataa kufunguka inatakiwa dawa fulani kama kumbukumbu ziko vizuri ni dinoproston, bei 50,000 kidonge kimoja! Nilizunguka mji wa dar es laam karibu kila famasia hio dawa hamna, siku inayofuata nikarudi pale namwambia ness nimekosa akanijibu ongea na watu vizuri dawa ipo hapa hapa lete hela nikuchulie!
Nusu saa nyingi dawa ikapatikana!
Akapewa dawa hata haikusaidia, siku ya nne ikaisha , siku ya tano asubuhi na fika pale mtu wa kwanza naulizia mapokezi pale nikaambiwa bado, mwanamke alishuka gorofani maana sehemu ya kujifungulia pale sinza ipo juu, ile tunakutana alikua ana lia! Nilijikaza kiume ingawa machozi yalikua yananilenga mno! Tulivyo achana nisiseme uongo nilitoka nje nikalia kwa kweli! Akaja mama mmoja simjui ila alisha nisoma, akanipeleka kwenye mgahawa akanunua chai akanipa, akaniambia wewe ni mwanaume kuwa mwanaume!
Nikarudi nyumbani kuandaa chakula jioni nikaenda tena hali ni ile ile.
Mungu ni mwema asubuhi siku ya sita saa 12 asubuhi nafika pale nikajitambulisha nikaambiwa panda juu, kufika naonyeshwa mtoto mama bado hakaa sawa katika operation dakika kumi zilizopita, nilishukuru aisee mtoto wa kiume uzito kg 4.2.