Wanaume wenzangu fanyeni mazoezi acheni kula chips yai

Wanaume wenzangu fanyeni mazoezi acheni kula chips yai

Niajee wakuu,

Mazoezi ni muhimu sana.

Shauri yenu!!!

Mwanaume ata kupiga push ups 10 huwezi, kukimbia nayo huwezi, ata kutembea mdogo mdogo km ½ nayo huwezi.

Achaneni na chips yai wazee pigeni tiz(mazoezi ya viungo).

Hivyo vitambi waachieni wake zenu.

Mazoezi kwa afya bora.
niko hap mfanya tizi
 
Naunga mkono uzi, ila Mkuu kiepe yai upate na mirinda bariiidi kwa mara moja moja sio dhambi.

Kuna kiepe fulani hivi hakikauki kipo teketeke yai halijaungua, aisee acha kabisa Mkuu, na ka kuku choma nusu kidari mixer ukwaju. Piga mambo Chifu.

Uzuri kiepe yai kinakubaliana hadi na bia.

Au upate ndizi mzuzu zikaangwe fresh na hako ka nusu kuku, usisahau ukwaju mixer mayonize iwe American Gadern. Aisee acha utani chifu.

Kila siku tupigilie misumari tu au makande!!?, hapana bhana.

Oyaa Wakuu kiepe tupige na matizi kwa kubalance, au sioo!?
We hujakutana na makande yaliyoungwa na nazi kisha yakalala.😂😂
 
Back
Top Bottom