Wanaume wenzangu mnaweza ku-deal vipi na mdada uliemtongoza halafu akakukataa, mbaya zaidi unafanya nae kazi ofisi moja

Wanaume wenzangu mnaweza ku-deal vipi na mdada uliemtongoza halafu akakukataa, mbaya zaidi unafanya nae kazi ofisi moja

Cv yako itashuka vipi kama hao wadada wengine wakijua? Ukipigwa kibuti maisha yanaendelea tena ukikutana nae mnapiga story kama hakuna kilichotokea. Shida mkitongoza huwa mnaweka na msisitizo wa sms unahisi atawaonyesha mashairi yako (formula ni moja tu sms za kimahaba hutumwa ukishakula mzigo)

Alafu utatongozaje mwanamke wa ofisini! Si unaona sasa una athiri kazi za taasisi na performance yako pia.

Ofisini huwa wanatongoza kiutani utani aka Kwa formula ya "sizitaki mbichi hizi" mwisho unakula "tunda kimasihara"
 
Unampotezea unafanya kama hujawahi kumtongoza ila salamu ni kama kawaida japo epuka kumshibokea au kumsusa utaona kazi chungu.. ukishindwa mtongoze rafiki yake wa kazini ili wagombane
 
Ushenzi wa kutongoza na kukataliwa, si unaona jamaa kajishobokesha kwako kuwa ufungue pm, ukampa Cha mbavu Kelsea
Unatakiwa kubadilisha hayo mawazo. Huwezi kubalika na kila mtu. Labda nikuulize swali dogo tu, wewe apo unakubali kila mtu maishani mwako? Huna chaguo kila mtu twende? Ukipata jibu basi hutakuwa na mawazo uliyo nayo sasa. Ukikataliwa kubali endelea na maisha yako wala haidhuru.
 
Hizo efforts kubwa ulizoweka ni zipi?
Besides mwanamke kazini hatongozwi boss bali unaangalia kuwa yeye ndio kakupenda na dalili utaziona
Labda anatembea na manager aliempa kazi na ni siri kubwa huenda ana mke wake
Ni mengi sana ya kuangalia kwa watu unaofanya nao kazi

Sio jambo zuri kutongoza wa kazini bora mheshimiane tu na kuendelea na majukumu yenu
Kwa mimi ni vigumu sana kumtongoza mwanamke kazini hata beki 3 😄
 
Sisi wanawake kwenye kikao chetu tulichokifanya tarehe 25 December...
Chini ya mwenyekiti wetu (jina kwenye mabano)

1-MARUFUKU KUANZISHA MAHUSIANO NA KAZINI (JOB MATE) MFANYAKAZI MWENZYO.

2-MARUFUKU KUANZISHA MAHUSIANO NA MPANGAJI MWENZYO AU JIRANI YAKO.

3-MARUFUKU KUMTONGOZA MWANAUME,

4-MARUFUKU KUMKARIBISHA MWANAUME MAHALI UNAPOISHI,

-MARUFUKU KUMFULIA NGUO BOYFRIEND

-MARUFUKU MARUFUKU KUMPA HELA MWANAUME KWANZA SISI HATUNA HELA

-MARUFUKU KUBEBA MIMBA KABLA YA NDOA,WEWE HAUNA KIZAZI CHA MAJARIBIO


MWISHO,

MWIKO KUDATE NA MWANAUME AMBAYE HAKUHUDUMIII.
Mwenyekiti wenu si alisema sasa ivi nyie masuperwoman!? Mnataka 50% kwa 50% kila kitu mbona mnasema tena kuhudumiwa?
 
Habarini,

Katika harakati za kutafuta mkate wa kila siku, unaweza jikuta unafanya kazi ofisi moja na mdada mrembo, she is young, hana mtoto, hajaolewa, unafanya nae kazi ofisi moja, unarusha ndoano, mbaya zaidi kimoyomoyo unamchukulia serious, kipindi chote ulichokaa nae hapo ofisini, kwa tabia zake unaona huyu akinikubalia tukiendana, anafaa kuoa, unamtongoza halafu anakukataa.

Ukute na hapo ofisini ana marafiki zake wengine wa kike, obviously ukimtongoza akikukataa, kwenye story zao atawaambia rafiki zake wa kike kuwa flani alimtongoza akakataa, hivyo CV/status yako kwa ujumla kwenye hiyo kampuni/mbele ya co-workers inashuka.

Mbaya zaidi unakuwa unaonana nae kila siku, heri angekuwa wa mtaani ukimtongoza akikataa unabadili njia ya kupita, sasa unamuona everyday, mara paap siku zinaenda unaona ameletewa posa, kaolewa, mara kapata ujauzito, na wewe uko hapo hapo. Sipatii picha hiyo awkwardness

How does it feel as a man, that pain, that embarrassment, all that effort uliyoweka, all that respect is flushed down the toilet. Unabaki unacheka usoni, moyoni umejaa maumivu na aibu

Hii scenario mimi binafsi haijanikuta in real life, ila najaribu tu ku-imagine.

Huu uzi bila comment ya Extrovert hautanoga
Pole Kwa kukataliwa bro,swala la kumtongoza tu huyo dada atakuheshimu sana. Hata awaambie wengine,ni sawa tu itakujengea heshima kwamba ww ni fearless man, pia ni rijali,kaa ukijua mwanaume hanidhi ndio hudhalilikambele ya mwanamke na sio rijali. Huyo mwanamke Iko siku utamla akishazaa na mme wake wakachokana,lazima arudi kwako kupooza hasira za mme wake just chill.
 
Kumtongoza mfanyakazi mwenzio Ni kosa moja kubwa Sana la kiufundi.

Mimi nikiwa boss wako afu nikukute unatongozana na your fellow workmates lazima nikupige kalamu.
Hapo unaingilia maisha binafsi ya mtu
 
Hizo efforts kubwa ulizoweka ni zipi?
Besides mwanamke kazini hatongozwi boss bali unaangalia kuwa yeye ndio kakupenda na dalili utaziona
Labda anatembea na manager aliempa kazi na ni siri kubwa huenda ana mke wake
Ni mengi sana ya kuangalia kwa watu unaofanya nao kazi

Sio jambo zuri kutongoza wa kazini bora mheshimiane tu na kuendelea na majukumu yenu
Kwa mimi ni vigumu sana kumtongoza mwanamke kazini hata beki 3 😄
Your not a real man😁😁
 
Bahari hilo ni Wimbi dogo sana.
Tafuta hela zaidi then utaleta jibu kesho.
 
Unatakiwa kubadilisha hayo mawazo. Huwezi kubalika na kila mtu. Labda nikuulize swali dogo tu, wewe apo unakubali kila mtu maishani mwako? Huna chaguo kila mtu twende? Ukipata jibu basi hutakuwa na mawazo uliyo nayo sasa. Ukikataliwa kubali endelea na maisha yako wala haidhuru.
Mwambie asiogope kusema kwa hofu ya kukataliwa, asiposema atajuaje kama kakubaliwa au kakataliwa?
 
Back
Top Bottom