WANAUME WENZANGU: Umewahi kufanya jambo ukaja kujuta baadae kama mimi ninavyojuta mpaka sasa?

On average ulikua unatumia 20M kila mwaka.

Ilikua biashara gani hii?
 
Kutofikiri kumuoa kwa mara ya kwanza yawezekana ni kwa sababu hukujuta kwa ulichokifanya ila hofu imekuja baada ya kupata binti na unahisi anaweza kulipia dhambi zako.

Kama inawezekana omba toba ya kweli lakini pia umuombee huyo binti afunguliwe maana kuna single mothers kibao wameolewa

Pamoja na kusema yote hayo, lakini moyo wangu ni mzito sana nikifikiria maisha ya huyo baby mama, ni wazi alikuwa perfect kid na staki hata kufikiria ni shida gani amepitia hadi sasa kwa kosa moja, huku akikuangalia ni kama unaishi perfect life. Daahh Mungu amtie nguvu
 
Mkuu ilibidi iwe hivyo ,wala usijali ukijilaumu sana utatengeneza negative emotions hiyo itapelekea ufeli kwenye mambo mengi ,wale wafia dini watapata sababu yakukuambia ni laana ya huyo dada , thinking positive bro , songa mbele achana na mawazo mfu mtunze mwanao. Jifunze low of attraction zinavyofanya kazi ili kuepuka mtego wa negative thoughts.
 
Wewe ndiye umesoma hadi chuo?Labda madrasa.Kwa nini haujui kujieleza wala kuandika?Be specific and to the points,dude!
 
Kosa ulilofanya hukusikiliza sauti ya Mama yako! Ungemuoa huyo huyo mwanachuo uliyempa ujauzito akakuzalia mwana.
Sikuombei mabaya! Lakini kama umezaa mtoto wa kike atafanyiwa hivyo hivyo kama ulivyomfanyia huyo binti.
Atazalishwa na atatelekezwa!
 
Jamani hapa mnasema singo mama wanaolewa ila kuna nyuzi nyingi tu mnasema singo mama hawawezikuolewa.
Wanaolewa vizuri tu ni kulingana na tabia na mienendo ya mtu !! Jf ni kundi dogo sana kusemea watanzania wote ! Users hawafiki hata Million humu , uhalisia ulioko nje ni tofauti sana na unaosemwa humu ndani !!
Jamii Forum ni watu tu kujimwambafy tu !!
 
Mzee hiyo kitu itakutafuna uzao wako wote ..ni kheri kama yeye angekupiga chini ..lakini wewe ulimlaghai ,ukamtia mimba...Kisha ukampiga chini ...dah....yani kiufupi karma is bitch hakuna Cha kusali Wala nini...Mungu hafugi ujinga na uzembe wako...maana alikuonyesha Toka awali...na ulijua....Kisha akakula warning ukaoa mwanamke mwingine....Sasa Kila chozia huyo Binti kwako ni adhabu ..na kwa familia yako pia....so kaka...jipange tu kiakili kuyapokea...na jua lisipokupata wewe ..binafsi...basi wanao..aua wajukuu zako watalipa hill deni.....sijui washikaji Huwa tunafeli wapi ....unampaje mtoto wa watu mimba ....ikiwa huna mpangi naye...!? Anyway ni kheri mngeitoa tu kipindi kile...ijulikane ni dhambi kuliko dhambi hii uliyoitenda kwa kukuharibia huyo Binti maisha ...
 
Kama uchumi unaruhusu fanya hima muinue kiuchumi nae yeye.
Hata akimuinua kiuchumi, mwanamke akiikosa ndoa huku age mates wenzake wote wameolewa hua wanahisi kuna kitu cha muhimu sana wana miss (that's the bitter truth)..

So hata awe na uchumi mkubwa kushinda bakhresa lkn atapata mfadhaiko wa moyo na stress maisha yake yote ikiwa hajapata bwana wa kumuoa. Feminist watapinga but that's the reality.

Kwahiyo ndugu jitahidi umuoe huyo binti hata mke wa pili. Afterall ameshakuzalia so ni muendelezo tu wa familia.
 
Ndugu Bangida asjkundangye mtu huko kufunga na kuondoa sijui roho ya malipizi hakutasidia kitu kama ulitenda kwa hiari yako ..na kwa kukusudia.....ikiwa unajua kabisa jambo Hilo litaenda kumiharibia mtu maisha ..lazima likurudi...Yani hio haikopeshwi...unalipwa sawasawa na vile ilibyotarajia
 
mimi hapa home nina mtoto wa kike nafikilia na yeye akikutwa na tukio kama lile itakuwaje huwa nafikilia sana na kumuangali binti yangu huyu hapa home.
Nafikiri hili ndio la msingi! Pole sana muite mfariji, japo haiwezekani kubadilisha kitu
 
Ndio maana mimi hupenda kufanya Caesarean Section kwa style ya J-Cohen. Sipendi kuacha kovu kwa mwanamke.

Yani akipona kidonda anakua na uwezo wa kuvaa crop top bila kovu kuonekana na hata kuogelea beach akiwa ameachia tumbo. It's good for cosmetic!
 
Muoe, au mhudumie kama mke wako
 
Ishu gani mkuu share hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…