WANAUME WENZANGU: Umewahi kufanya jambo ukaja kujuta baadae kama mimi ninavyojuta mpaka sasa?

WANAUME WENZANGU: Umewahi kufanya jambo ukaja kujuta baadae kama mimi ninavyojuta mpaka sasa?

Habari wana Jf nipo na ID nyingine niliifungua karibu siku 26 zilizopita. Twende kwenye mada.

Mimi nina umri wa miaka 35 kwa sasa nina watoto 3. Nimeoa na nina mke nimezaanae watoto 2. Mtoto wangu wa kwanza nilizaa na dada mmoja chuoni. Mama yake sikumuoa nilioa mwanamke mwingine ila mtoto ninaishi nae mimi. Kitu hiki ndo kinanifanya kuwa na majuto kitendo nilichomfanyia mama yake. Daa kinaniumiza sana sometime nawaza bora ningemuoa mama yake.

Kipindi nipo chuo mwaka wa 3 naingia. Mwaka wa kwanza ndo walikuwa wanafika chuoni. Sasa si unajua mambo ya chuo mabinti wapya kutoka form 6 ndo wanakuja. Vijana mambo ya chuo naamini mnaelewa. Sasa nikamuona binti mmoja, nikaanza kumvizia sana, nakumbuka kipindi kile na rafiki zangu tulikuwa tunagawana mabinti, mimi huyu wewe yule.

Nilizoeana nae na kuanza kumfuata ili kuanzisha mahusiano nae. Nilijitahidi kuvizia na kupeana mbinu wa friends. Wenzangu walifanikiwa baadhi hadi kuwa nao first year. Ila mimi bado ananiangaisha.

Yeye alisema issue ya mahusiano hapana labda kuwa friends kawaida tuu. Mimi nikaona poa ila bado namvizia yule dada. Japo alikuwa mgumu sana.

Siku moja chuoni night watu walikuwa wanafanya discussion. Sasa nilikuwa na yule binti night siku ile tulipiga story kadhaa. Nilipanga kusex nae anytime nitakapo pata chance.

Siku ile nilipanga leo ni leo nitafanikiwa. Nakumbuka niseme kwa kifupi tuu nilimlaghai sana kwa kumshika shika akawa anasema tuu acha. Baadae akatoka akaamua kuondoka kurudi hostel, mimi nilikuwa sikai mbali na chuoni ghetto langu ni maeneo hayo ya chuoni tuu.

Nilimshikashika mpk akasema usinishawishi kuzini mimi siitaji.

Niliendelea tu.

MWISHOWE alilainika na akajikuta anakubali , nilienda nae ghetto tukasex na alilala mpk morning.

Asubui anashituka daa nikamkuta analia sana na kunilaumu, aliondoka na kwenda hostel .

Hatukuwa karibu kama 2 weeks hivi. Baada ya wiki 3 na siku kadhaa akaniambia siku zake haziona. Mimi eeeeeee. Nilishituka sana. Kumbe siku ile alikuwa siku zake za hatari . Nikili tuu nilitake risk sikutumia condom.

Niliisi kama kuchanganyikiwa hivi nikaona au ananimbambikizia nini. Niliwaeleza wadau wakasema Katoe , mimi daaa kitu hicho sijawahi hata kufanya , nikimuangalia binti yeye namuona she is not okay muda wote mpk wenzie wanamuliza shida nini.

Nikaa kimya tuu siku zinaenda naona tumbo hilo. Baada ya miezi kama 3 hivi ujauzito ukaanza kumsumbua sana. Mpk akaanza kunilaumu mimi. Akalazimika kwenda kwao. Kwao walimzingua sana tena sana.

Alikuwa ananipigia simu huku akinilaumu kwa siku ile.

Akalazimika kusitisha chuo. Baada ya kujifungua mimi nilikuwa nishamaliza chuo.
Mbaya zaidi akajifungua kwa operation mda wa kukaa home ndo ukazidi.

Akarudi chuo wenzie wako mwaka wa 3 yeye anaendelea na semester ya 2 mwaka wa kwanza. Mshono wa operation ulimsumbu sana.

Mimi nilisena tuu home wakanitupia maneno sana kwani wazazi wangu ni watu wa dini sana. Tukio lile lilinifanya niache kuzini kabisa.

Ila baadae nilikutana na binti mwingine. Na kumuoa .
Japo mama alinisisitiza sana muoe mama mtoto wako. Kwa sababu pale umemuaribu mtoto wa watu. Mimi wala sikujali.

Ila mzazi mwezangu yule. Tangu kamaliza chuo akipata mwanaume, akijua anamtoto jamaa anamuacha. Kila anayepata anamuacha. Baadae nikaona ngoja nimchukue mtoto nikae nae. Ili na yeye apate mtu amuoe . Ila wapi.

Mwaka juzi alipata mmoja alikubali ila alivyokuja kugundua alijifungua kwa operation akamuacha. Mara nyingine anakuwa ananilalamikia sana nimemualibia system mzima ya life yake.

Kwa sasa anaumri wa miaka 32. Rafiki zake wote tayari wameolewa ila yeye bado , mara nyingi anakuwa ni mtu wa huzuni sana , she is not happy always.

Hiki kitu mara nyingi kinaniumiza sana , maana naona kama nimemuaribia maisha binti wa watu.

Na mimi hapa home nina mtoto wa kike nafikilia na yeye akikutwa na tukio kama lile itakuwaje huwa nafikilia sana na kumuangali binti yangu huyu hapa home.

Daaa we acha .

KAMA NIMEKOSEMA UANDISHI NAOMBA RADHI.[emoji2969][emoji120][emoji120][emoji120]
Fanya kitu kuhusu huyo dada. Zungumza naye ni kipi unfanyie.
 
Wanaolewa vizuri tu ni kulingana na tabia na mienendo ya mtu !! Jf ni kundi dogo sana kusemea watanzania wote ! Users hawafiki hata Million humu , uhalisia ulioko nje ni tofauti sana na unaosemwa humu ndani !!
Jamii Forum ni watu tu kujimwambafy tu !!
Haya naisevu hii comment nisione unatoa maoni hasi Kwa singo Maza. Nisikuone kwenye kataa ndoa
 
Nikuulize kitu Kapeace

Wapi uliona vitabu vitakatifu vinazungumzia Karma?

Hizi ni mambo tu watu wamejitungia kutishana tu
Yani we mkware wewe,, hebu punguza dhambi unaona unavyohangaika umeniquote mara mbili kwa comment moja,, karma ipo kaa kwa kutulia hasa kwa makosa ya kukusudia km ya mtoa mada kumzalisha na kumtelekeza dada wa watu, chozi na simanzi ya huyo dada iko juu yake
 
Wanajiongelesha tu na wao ndio wa kwanza kuwakataa single mother.
1. Ana mtoto
2. Ana kovu la C-section, hata mwanaume akimvua siku moja tu anajua ana mtoto. Hata kama haishi na huyo mtoto lakini mwanaume anawaza daily atakuwa anaona hilo kovu na kukumbuka mtoto aliyesababisha hilo sio wake.
3. Ana miaka 32, jioni hii.

Kama ni probability hapo hata 0.2 haifiki. Alafu kitu watu hawaelewi ni attraction, mwanaume mwenye attraction hana tatizo lolote, ana nguvu, uchumi mzuri na akili sawasawa na mwenye maono haoi penye makandokando. Huyo anayejivika kwenye makosa mengi kuna kitu hayuko sawa, na hapo ni discourage kwa mwanamke mwenye hadhi ya wastani au ya juu kijamii. Mwishowe wanafanya compromise, wenye makandokando wanabebana kuvumiliana.
Singo mama, ana operation ya kuzaa, over 30 yrs
Dah huyo dada kazi anayo ila ajipe moyo atapata mume wa maisha.
 
Yani we mkware wewe,, hebu punguza dhambi unaona unavyohangaika umeniquote mara mbili kwa comment moja,, karma ipo kaa kwa kutulia hasa kwa makosa ya kukusudia km ya mtoa mada kumzalisha na kumtelekeza dada wa watu, chozi na simanzi ya huyo dada iko juu yake
Karma ipo watu wakubali ama wakatae
 
Kosa ulilofanya hukusikiliza sauti ya Mama yako! Ungemuoa huyo huyo mwanachuo uliyempa ujauzito akakuzalia mwana.
Sikuombei mabaya! Lakini kama umezaa mtoto wa kike atafanyiwa hivyo hivyo kama ulivyomfanyia huyo binti.
Atazalishwa na atatelekezwa!
angezaa wa kiume je?
 
Nilikutana tuu na mwingine nikampenda basi. Sio kwamba alikuwa na kasolo ,No.
Ulikosea sana mtu uliyepaswa kumpa kipaumbele ni huyu ambaye umekwisha zaa nae... Wengine mnawezaje kukubali kuwa na watoto kutoka kwa mama tofauti tofauti aisee....
 
MKuu, kufunga ili kuondoa roho za malipizi ndo inakuaje? Maana kuna majuto tunayo yanaeza kujaa kaunta buku.
Roho za Malipizi, kwa lugha nyepesi ni Kisasi namanisha Kuwa kile ambacho unamtendea mwenzeko basi hicho ndo kitacho tendeka kwako means kinajirudia kwako, haijalishi ni kibaya au kizuri
Ogopa sana ndugu mtu anae ishi maisha ya kumlaumu mwingine, mfano mtu anasema Fulani ndo amesababisha niwe hivi, aisee hiyo ni Mbaya sanaa machozi anayo yatoa siyo Bure, yanaweza yakaja kutokea kwako au kwa watoto wako aidha kwa kizazi chako ukawa na watoto wa kike au wa kiume ukashangaa Hawaoi au hawaolewi, kiufupi huyo Dada anateseka na hayo mateso umemsababishia wewe na anakulaumu wewe.

Swala la Majuto, huyo Dada hajakubali ku move on na hiyo kwa sabab ya Hali anayo pitia so anapo pita kwenye hiyo hali ndo anakukumbuka ulio mfanyia na anamua kukutafuta, nawewe anapokutafuta ndo nawewe Roho ya huruma inakuingia unaanza kujuta lakin kama ange move on usingeleta Thread hapa unajuta but kwa sabab Bado anateseka na anakutafuta lazma ujute kwa ulichomfanyia
Muombe Mungu wako hiyo Laana ya machozi yake isikupate
 
Daaaaah.
Ulizingua sana Kiongozi.

Japo Binti nae alizingua, genye zilimponza. Kuna mabinti sasa wanaenda chuo, wajifunze kipitia hili.

Ukiwa na genye na usidinywe kwani unakufa?.

Angalia namna Kiongozi upunguze kovu la Binti wa watu. Daaaaah inasikitisha Sana.
 
Roho za Malipizi, kwa lugha nyepesi ni Kisasi namanisha Kuwa kile ambacho unamtendea mwenzeko basi hicho ndo kitacho tendeka kwako means kinajirudia kwako, haijalishi ni kibaya au kizuri
Ogopa sana ndugu mtu anae ishi maisha ya kumlaumu mwingine, mfano mtu anasema Fulani ndo amesababisha niwe hivi, aisee hiyo ni Mbaya sanaa machozi anayo yatoa siyo Bure, yanaweza yakaja kutokea kwako au kwa watoto wako aidha kwa kizazi chako ukawa na watoto wa kike au wa kiume ukashangaa Hawaoi au hawaolewi, kiufupi huyo Dada anateseka na hayo mateso umemsababishia wewe na anakulaumu wewe.

Swala la Majuto, huyo Dada hajakubali ku move on na hiyo kwa sabab ya Hali anayo pitia so anapo pita kwenye hiyo hali ndo anakukumbuka ulio mfanyia na anamua kukutafuta, nawewe anapokutafuta ndo nawewe Roho ya huruma inakuingia unaanza kujuta lakin kama ange move on usingeleta Thread hapa unajuta but kwa sabab Bado anateseka na anakutafuta lazma ujute kwa ulichomfanyia
Muombe Mungu wako hiyo Laana ya machozi yake isikupate
Ni kweli kabisa kuna mambo sisi wanaume kutokana na hali na mwenendo wa maisha yetu ya ujana kuna baadhi ya matendo ambayo hujikuta tunafanya halafu gharama zake ni kubwa sana yametugharimu wengi....kwa kuongozwa na mihemko tu

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom