Wanaume wenzetu ninyi mnaweza vipi kushona sare za vitenge na wake zenu? Ni nini siri ya hili?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Huenda ni malezi niliyokulia maana sikuwahi kabisa kumuona mzee wangu akivaa sare na mama yangu.

Ziwe sare za kanisani ama popote pale kwakweli sijawahi Ona hadi sasa wana zaidi ya miaka80!

Ninyi wanaume wenzetu ni Mahaba/upendo sana kwa wake zenu au ni limbwata pamoja na kupandwa kichwani na wake zenu?

Kwangu mimi naona ni ngumu mno kunivalisha sare. Pete ya ndoa nayo nahisi nilivaa siku zisizozidi 3 nikaweka kwenye bag japo hadi sasa ipo bi mkubwa akaitunza.

Leo nimeona jamaa yangu kavaa batiki la sare na mke wake pamoja na watoto. Kwakweli nimemuuliza kuwa jamaa wewe unaweza vipi?

Akanishangaa na mimi nikamshangaa kifupi tumeshangaana wote.

Wakuu huu ujasiri ninyi mnaweza vipi wajameni?
FB_IMG_1741972178096.jpg
 
😀😀😀😀 wanasema ukiona mwanamme amevaa sare na mke wake ujue hana sauti juu ya huyo mke wake. Yeye atakachoambiwa ni ndiyo mzee.
Lakini pia wanaoongoza kuvaa sare ya vitende ni hawa wanaosali makanisa ya kilokole hapo unakuta baba mchungaji kashawapiga semina ya upendo katika ndoa.
Kisha wanafuafiwa na wasabato nao wana huo ujinga wa sare sare.

Hayo mambo hukuti kwa waislam au waroman
 
Huenda ni malezi niliyokulia maana sikuwahi kabisa kumuona mzee wangu akivaa sare na mama yangu.

Ziwe sare za kanisani ama popote pale kwakweli sijawahi Ona hadi sasa wana zaidi ya miaka80!

Ninyi wanaume wenzetu ni Mahaba/upendo sana kwa wake zenu au ni limbwata pamoja na kupandwa kichwani na wake zenu?

Kwangu mimi naona ni ngumu mno kunivalisha sare. Pete ya ndoa nayo nahisi nilivaa siku zisizozidi 3 nikaweka kwenye bag japo hadi sasa ipo bi mkubwa akaitunza.

Leo nimeona jamaa yangu kavaa batiki la sare na mke wake pamoja na watoto. Kwakweli nimemuuliza kuwa jamaa wewe unaweza vipi?

Akanishangaa na mimi nikamshangaa kifupi tumeshangaana wote.

Wakuu huu ujasiri ninyi mnaweza vipi wajameni?View attachment 3270594
Waulize wanyakyusa, ndio zao hizo
 
Back
Top Bottom