Wanavyofanya Musukuma na Polepole ni ushahidi wa ukomavu wa Rais Samia kisiasa

Hapakuwa na ukanda Bali ukabila wa Kabila moja
Utajua tu Hilo kabila linabeba mikoa mingapi 2025.
Hangaya mwenyewe anajua hili,ndo maana kaenda huko Mara nyingi kuliko mkoa wowote bara.
 
Umeigomea wewe sio watanzania. Juzi nilikutana na mtu anaitafuta chanjo hata kwa kulipa laki 5 achanjwe, maana anataka kusafiri na bila chanjo hapewi hata booking ya ndege achilia mbali Visa
Hao wanaosafiri kwenda nje,ni wangapi kati ya watanzania wangapi?
Tatizo mnajiongelea nyie ambao ni vibaraka wa chanjo. Mbavu zenu
 
Mkuu CCM iina demokrasia ya kutosha. Ingekuwa ni huko kwa wachaga tena unaepinga siyo mchana cha moto ungekiona.
Hapa kwa hili unalosema tumsifu Rais Samia, Kikwete na Mzee Mwinyi enzi zao kidogo demokrasia ilikuwepo. Lakini kwa wakatoliki Nyerere, Mkapa na Magufuli kuwakosoa ilikuwa hatari kupita hatari.
 
Ufahamu wako kwenye haya mambo uko chini sana. Kama watalii hawaji, ndege haziji, wazungu wamejifungia lockdown, hakuna uzalishaji huko Ulaya na Marekani, hakuna masoko ya kuuza Mahindi yetu, korosho, madini, nk na wakati huohuo wananchi wetu Wanahitaji huduma za elimu, afya umeme, ulinzi, nk utafanya nini? Hivi unaweza kuwaambia askari subirini mtalipwa mishahara hali ya kiuchumi ikitengemaa?

Lazima utatafuta fedha kwa kupamdisha bei ya tozo na huduma ili angalau kumudu kulipa mishahara ya watumishi, kununua madawa, nk. Kumbe ungekuwa wewe ungefanyaje?
 
Utajua tu Hilo kabila linabeba mikoa mingapi 2025.
Hangaya mwenyewe anajua hili,ndo maana kaenda huko Mara nyingi kuliko mkoa wowote bara.
Unahitaji wasimamizi safi wa uchaguzi kushinda uchaguzi sio wapigakura safi sijui kabila gani huko, wewe mbona unakuwa kama mgeni wa nchi hii.
 
Kadanganye watoto, mtemi Hangaya angeshatokea ili awafurahishe waliozitoa.
Ziliexpire Jomba,ndo maana dudu feki la mchina likatua.
Kama watu hawazitaki wasingeleta nyingine tena.
 
Anawaacha wajikaange na mafuta yao yenyewe mwisho wao upo karibu watakukuta hakuna wa kuwatetea
 
Hahahaha yote uliyotaja 1-6,hakuna linalogusa moja kwa moja wapiga kura ambao ndo huamua Nani apite.

Hizi ni hoja za ujuajijuaji wa JF.

Kama chanjo siyo issue mbona Watanzania wameigomea?
Kama wamachinga siyo issue subiri 2025.
Kwani CCM inategemea sanduku la kura?
 
Mkuu CCM iina demokrasia ya kutosha. Ingekuwa ni huko kwa wachaga tena unaepinga siyo mchana cha moto ungekiona.
ukimaliza kunengua utuambie hiyo demokrasia ilianza lini humo fisiemu? Ukimkumbuka Kolimba hutosahau ya Bashiru na Nape.
 
"Polepole na Musukuma ni watu wanaopingana na Rais Mama Samia kwenye kila kitu."

😁😁

"Walipinga chanjo weeeeee lakini mwishowe nadhani na wawo walichanja kimyakimya."

😁😁

Hiiiiii bagosha!
Hao ndio ccm wachumia matumbo. Najiuliza tu "hii nchi ina undumilakuwili wa aina gani?" hayo maneno waliyokuwa wakibwata kina Polepole, Msukuma na Gwajiboy yangelitamkwa na mtu asiye CCM leo mtu huyo angekuwa na kesi ya ugaidi kama sio uhujumu uchumi! Watu walipimwa mkojo!! Watu wakaitwa wachochezi na leo hii kuna watu tuliaminishwa ni magaidi mambo yametibuka kumbe ni UONGO!!
 

"Hii nchi imechezewa sana." Mwisho wa kumnukuu 😁😁.
 
Msukuma na polepole si wanafiki kama alivyo Nape wao wako wazi kuweka hisia zao
 
Anawaacha wajikaange na mafuta yao yenyewe mwisho wao upo karibu watakukuta hakuna wa kuwatetea
Wapinzani walipokuwa wanataka Katiba mpya ambayo Rais amepunguziwa nguvu akina Polepole na Musukuma wakidhani ni kwaajili ya wapinzani tu. Sasa hivi wanaanza kumtisha Mama eti wamachinga watamnyima kura Mama 2025 kama atawaondoa kupisha njia za waendao kwa miguu na kuacha kuuza nyanya chini kwenye vumbi na tope. Wamesahau kuwa Rais wetu ndiye pia mwenyekiti wa Chama chetu tawala, wanasahau kuwa Rais anamteua na kumfukuza kila mtu nchini, wanasahau kuwa Rais ndiye Amirijeshi wetu mkuu.

Wanamtishia nyau mama asiwatendee haki walionyang'anywa njia zao za kukwepea magari, asitoe haki kwa wale ambao mitaa Yao inajaa maji wakati wa hata mvua kidogo TU kutokana na wahuni kuziba njia za majitaka kwa kisingizio eti wanatafuta riziki, yaani wewe riziki yako ndiyo isababishe ajali kwangu.

Kila Rais lazima aendleleze mazuri lakini na kunyoosha mabaya ya mtangulizi wake. Mazuri mengi ya Nyerere yameendelezwa sana lakini mabaya yake mengi pia yamenyooshwa na wenzake pia na mama Samia ataendelea kuyaendeleza na kuyanyoosha pia, asishikwe mikono kizembe.
 
Ongezea pia na wanaopenda TOZO, na wanaopenda mfumuko wa bei, pia wanaopenda ufisadi ndio watakaompa kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…