Wanawake hivi na nyinyi mkikuta mwanaume ana mtoto mnakataa kuolewa naye?? 🤔🤔

Wanawake hivi na nyinyi mkikuta mwanaume ana mtoto mnakataa kuolewa naye?? 🤔🤔

Hao watoto wake wanazuia vipi huba langu?
Me naangalia mapenzi na huduma muhimu hayo ya watoto nitawalea kiroho safi, na mama zao hawantishi!! 🤣🤣🤣
Mpenzi unajidanganya hao watu hawana shukurani
 
Ni vile Kuna uhaba wa wanaume..

Ila simshauri Binti kuolewa na mwanaume mwenye mtoto...

Tatizo sio kupasha kiporo na huyo mwanamke, wala tatizo sio huyo mtoto ambaye ni malaika...

Tatizo ni huyo mwanamke ambaye atakuloga na kukufanyia vituko na amani ya ndoa hutaiona...
 
Wanawake ni wazuri kuchagua wa kuingia nae kwenye mkataba wa ndoa. Kama una maokoto utawaoa tu. Kama huna anakuja kufuata nini na tayari una mtoto? Ukiwa na kid hakikisha una maokoto utawaoa sana
 
Kuwa fair, si mwanamke wala mwanaume anapenda kuoa au kuoewa na na mtu mwenye mtoto ilihali yy hana. Ndio maana tunasema kila siku inapendeza mwenye mtoto apate mwenye mtoto mwenzie
 
1. Kama sio mgane basi watoto sio zaidi wawili wa mama mmoja na wakae kwa mama yao kama yupo hai.
2. Baba uwe na kipato cha kueleweka kuhudumia mbegu zako zote kikamilifu
3. Mipaka kati yako na baby mama
( mfano... Kuna dada ameolewa akiwa na mtoto mmoja, mawasiliano kati ya baba na mtoto na mahitaji yote yanapitia kwa baba wa kufikia na shuleni... mama na baby daddy hawana uhusiano wa karibu tena)
N.B siwezi kulea mtoto wa mtu ilihali aliyembeba tumboni yupo na afya tele.
 
Back
Top Bottom