Wanawake mnaojenga nyumba kwa siri bila mwenza kujua huwa mnamaanisha nini?

Wanawake mnaojenga nyumba kwa siri bila mwenza kujua huwa mnamaanisha nini?

Mimi mama yangu kajenga mikoa tofauti na hadi mshua anaenda kaburini hajui lolote. Wakati wa uhai wake kampiga sana matukio hataki afanye kazi na hataki awe na maendeleo yoyote eti mke wa mtu na alimkuta kasoma na ana kazi tayari. Mtu hawazi ya mbele na ukoo wake ni ule wanaamini cha ndugu yoyote ni cha ukoo mzima. Akaona isiwe kesi katafuta mahala pengine kimya kimya. Na mzee alipofariki tu fujo zikaanza haya niambie kama hakua kajiongeza mapema hali ingekuaje.
Pole, hapo kwenye ndugu kuleta vurugu nakuelewa Sana.
 
Wanajiahami siku mkiachana vitu vyake visiwekwe kwenye mgao.

Jirani yetu anajenga tokea muda ila nyumba bado haijaisha huku mkewe tayari amejenga na nyumba imeisha kaweka wapangaji.
Mume hajui ila majirani tunajua.
Duuuh kudadekii ila sema Haina shidoo 🤣🤣

Nimejifunza jambo, kwamba si kila kitu uwe unamshirikisha mwanamke baadhi ya maendeleo fanya peke yakoo :ACTINUP: :AYOOO:
 
Unafikiri wanaume wote wapo kama mzee wako?.

Kiasili mwanamke ni MBINAFSI,hela yake ni chungu haijawahi kuwa tamu.Hela yake inamatusi na masimango.

Halafu unakuta nyie mnajenga kwa siri na tena inawezekana akawa ana mali nyingi, ila siku ya kuachana zinagawanywa za wanaume.
Kuna sehemu nimeandika wanaume wote wapo kama mzee wangu???? Huo ni mfano tu wenye uhalisia ila wanaume wa aina hiyo wapo tena wengi. Mwanamke mpaka anaamua kufanya mambo yake lazima kuna sababu. Kuna wengine kweli ni ubinafsi lkn kuna wengine matendo ya waume zao ndio sababu hufikia maamuzi ya kufanya mambo yao kimya kimya bila kushirikisha waume zao.
 
Nataka kujua ndio ujanja,umaarufu,ukisasa, usomi,kiburi,majigambo,majivuno,dharau,umwamba au!!?

Na tena wakati unafanya hivyo upo kwako na mlishajenga pa kuishi,na mwenza anakushirikisha Kila jambo la kifamilia analofanya!

MSAADA TAFADHALI,sio kwamba natumika baadae nitangulizwe baada ya mpangokazi wake wa ukwasi kukamilika!

Maoni yenu nitayazingatia!

Kataa ndoa mje pole pole!!

Na wale waume wenza mliopo humu mje pole pole nawajua!
Kuna jamaa yangu alimshtukia mkewe ana kibanda cha room 3 na kajenga kimya kimya. Kilichomfanya aanze kufanya uchunguzi ni mke kuanza kuwa jeuri kupitiliza. Alitafuta wahuni wakakivunja usiku, dada wa watu alitumia wiki kama mbili anaongea kwa ukwali huku akitema mate kama cobra bila kueleza kipi kimemkuta.
 
Ubinafsi hauna jinsia.
Kweli hauna jinsia ila nimekutana na kesi nyingi sana kila mtu anadai hii ni mali yangu haimuhusu mwenza wangu kuna tatizo kubwa sana africa ndoa ni taasisi unakuta mtu anathubutu kusema nyumba ni mali yangu haiwahusu watoto wangu au mke wangu unajiuliza huyu mtu ni kichaa, Tujalibu kuwaelimisha watu tofauti ya mali binafsi na za familia watu hawajui hata kuchukua mkopo kwa nyumba ya familia ni kosa anaona yuko sawa wakati hajashirikisha wana familia wenzake.
 
Hahahahahah Moto ushawaka tayarii 😅 😅 :Alarm:
 
Na hao wanawake unawaongeleaje ???

Maana umejibu kujumla
 
Thanks, pole zaidi nampasia bi mkubwa mana walimsumbua akachukua vilago vyake akahamia zake kwake.
Sheria ipo lakini, hata mki amua kuzi dai leo mna shinda.
japo Sina uhakika Kama mta pata amani au usalama wenu.

sisi tuli enda toe to toe na ndugu wa mzee, nili kuwa na miaka 20 tu ila wali jikuta mahakamani bila kupenda.
 
Mahakama ilitoa agizo vitu vya marehemu abaki navyo mjane ndio wakatulia kimya. Ila familia zetu za kimaskini hizi ni shida sana unakuta mtu anakaa anawaza kaka ana hiki na kile mbeleni vitakua vyangu.
 
Nataka kujua ndio ujanja,umaarufu,ukisasa, usomi,kiburi,majigambo,majivuno,dharau,umwamba au!!?

Na tena wakati unafanya hivyo upo kwako na mlishajenga pa kuishi,na mwenza anakushirikisha Kila jambo la kifamilia analofanya!

MSAADA TAFADHALI,sio kwamba natumika baadae nitangulizwe baada ya mpangokazi wake wa ukwasi kukamilika!

Maoni yenu nitayazingatia!

Kataa ndoa mje pole pole!!

Na wale waume wenza mliopo humu mje pole pole nawajua!
Acha uoga Mwamba,ulikuwa unaandakiwa suprise ila sasa umeshaifanya habari ya kawaida wewe mwenyewe.
 
Kama akili zenyewe ndio hizi acheni tu vijana wa siku hizi wawe wagumu kuoa.Sasa mtu yupo kwenye ndoa anatelekeza vipi mtoto? Ila cha ajabu siku wakija kuachana zinagawanywa na mwanaume ila mali a mwanamke haziguswi,halafu kesho mnalamika mnataka 50/50 ,haki sawa ila vya kwenu hamtaki usawa.

Kama bado unaroho ya UBINAFSI ndoa haikufai achana nayo, endelea kukaa mwenyewe ujenge nyimba zako ,ufungue biashara zako uendelea na maisha yako binafsi.
Hivi ni kweli hamna uelewa wa haya mambo ya migogoro ya kifamilia na kadhia za talaka au kutengana.

Wanaume wangapi wanaendelea kuhudumia watoto ipasavyo baada ya ndoa kuvunjika na bila kushurutishwa na ustawi wa jamii au mahakama? Wapo ila ni wachache, wengi wanaamini mkiachana jukumu la watoto ni la mama.

Ndoa ikivunjika, taratibu za kutafuta mpaka kupata talaka inaweza kuchukua miaka. Hicho kipindi chote hao watoto uliomwachia mkeo wanaishije? Kama mke hajasimama kiuchumi ni either watoto watateseka au atarudi kwao kusaidiwa kulea na ndugu zake.
Naona kama majadiliano mengine tunalazimisha tutoke nje ya maisha yetu ya kiuhalisia kwenye jamii.

Kuna shida kubwa sana ya malezi ya watoto na mwanamke kwa kiwango kikibwa ndiye anayeathirika ndoa ikivunjika. Sheria za mgawanyo zimewekwa ili kulinda maslahi wa wanandoa wote na watoto. Kisheria, ni kosa kuidanganya mahakama na kuficha mali iwe amefanya mwanamke au mwanaume.
 
Mahakama ilitoa agizo vitu vya marehemu abaki navyo mjane ndio wakatulia kimya. Ila familia zetu za kimaskini hizi ni shida sana unakuta mtu anakaa anawaza kaka ana hiki na kile mbeleni vitakua vyangu.
sisi kwetu tuko wa3, wa 1 Mimi, pili dogo na wa mwisho dogo.

hata nikifa Leo, nina uhakika amani ita kuwepo. Maana hamna mwenye roho mbaya ya kichawi.
 
Ni kama wanaume mnavyofanya mambo yenu kimya kimya basi na wanawake ni hivyo hivyo. Kuna dada alienda kununua kiwanja mahala hakumuambia mumewe kumbe mumewe nae katafuta kiwanja eneo hilo hilo bila kujua na hakumuambia mkewe. Mbeleni wamekuja kujua wamenunua viwanja eneo moja na kila mtu kamficha mwenzake.
Sasa si bora muwekani wazi kila mtu na vitu vyake ,nyiie muwe mna share ngono na watoto tu!!??
 
Back
Top Bottom