Wanawake mnawezaje kuishi na mwanaume anayefokafoka?

Wanawake mnawezaje kuishi na mwanaume anayefokafoka?

Habari zenu jamani.

Naomba kuuliza, inawezekana mie nimesahau mafundisho ya shangazi, wanawake wenzangu mnawezaje kuishi na mwanaume anaye fokafoka? Maana mimi naona yamenifika hapa!

Huyu mwanaume amenizidi umri kwa miaka saba, sasa sijui ananichukulia mimi mdogo yake! Yaani nikikosea kitu kidogo atafoka huku ananikata jicho kali, haijalishi kuna dada wa kazi karibu, ni atafoka tu! Huyo dada wa kazi nae anafokewa hadi namuonea huruma mtoto wa watu.

Huwa nanyamaza kisha namtafutia pose zuri namwambia anavyonikwaza ila routine ni ile Ile, nahisi kukonda, kugombana nae siwezi atanibonda nife.

Naombeni mbinu jamani nifanyeje, yamenifika kwa koo mwenzenu?!
Unaishi na mgodi huo

Wasiliana na prodyuza wa bongofleva amtengenezee beat atoe single moja matata

Mwanaume kufokafoka ni ongezeko la hormons za kike mwilini kwake
 
Elimu tuko Sawa, amenizidi kipato....Yani afoke Mimi niwashe redio, naweza Kula mateke....akifoka Mimi nikae nimsikilize, niombe msamaha....ndo nakuwa mwanamke mwenye adabu.
Kinachomfokesha sasa hata hakiingii akilini, mfano umekosea kuzima TV, umezima direct kwenye socket atafoka mashetani ya mtaa mzima yatajua....nyiee
Aaa weee 😳 ha ha haa,huyo kakuchoka aisee
 
Nishajiliza, nishanuna....Ila haachi, Hadi sasa nimeamua nijifanye mjinga, nijishushe!
Ila inaniumiza jamani, naumia....kuna wakati nawaza au mapenzi yameisha! Watu wengine anaongea nao vizuri Mimi ananifokea!
Jamani! Pole sana i feel bad jinsi unavyo express your feelings... Kama mi ndo ningekua that man na kupitia huu uzi ningekuomba msamaha mkubwa kabisa na ningebadilika to be that bae you want
 
Elimu tuko Sawa, amenizidi kipato....Yani afoke Mimi niwashe redio, naweza Kula mateke....akifoka Mimi nikae nimsikilize, niombe msamaha....ndo nakuwa mwanamke mwenye adabu.
Kinachomfokesha sasa hata hakiingii akilini, mfano umekosea kuzima TV, umezima direct kwenye socket atafoka mashetani ya mtaa mzima yatajua....nyiee

asikutese kiasi hicho mpe altimatum na kama habadiliki chukua maamuzi ya kutengana. ikibidi mtengane vyumba au uhame kabisa mtengane kwa muda fulani mpeane nafasi akiona ana kuhitaji basi akubali sharti la kubadilika, la habadiliki achana nae huyo atakupa stress tu.
inaonekana hajiamini ndio mana anafoka, kwa nini umfokee mtu mzima ambaye hakatai maelekezo ukimuelekeza? kama mtu ni jeuri ni sawa akifokewa ila kama wewe sio jeuri basi anakuonea.

siku nyengine mrekodi kwa siri asijue halafu baadae utoke nae nje ya mji huko akiwa ametulia msikilizishe upuuzi wake halafu muulize kama ni yeye ndio anafanyiwa hivyo angejisikiaje?
 
Elimu tuko Sawa, amenizidi kipato....Yani afoke Mimi niwashe redio, naweza Kula mateke....akifoka Mimi nikae nimsikilize, niombe msamaha....ndo nakuwa mwanamke mwenye adabu.
Kinachomfokesha sasa hata hakiingii akilini, mfano umekosea kuzima TV, umezima direct kwenye socket atafoka mashetani ya mtaa mzima yatajua....nyiee
Again pole sana. This is so emotional. Pole sana. I pray for you this problem to go away.

So far unaonekana unadili nae kwa akili. Una akili sana. Endelea ivo ivo.
 
kwa nini ulikubali kuolewa na baba yako... au kwa kuwa ulibeba mimba yake kabla ya ndoa......
 
Hahahahah kiukweli nimecheka,pole ila uyo mtu usikute ndo ivyo alivyo ama ndo tabia yake,kwani wewe kama mke bado haujamsoma mwezako mpaka sa hi? ,na kumbadilisha mtu mzima KAZI kweli kweli......mwombe mungu yataisha
 
Ni vitu Gani hivyo vinavyomfanya akufokee mara nyingi am sure ukibadilika na kufuata anavyokuelekeza hatofoka tena.
Otherwise keep on minding your mouth, wanaume hawapendi mwanamke Mwenye kelele.
 
Back
Top Bottom