Mimi niseme tu ni kweli usaliti wa mwanamke hauvumiliki ni tofaut na mwanaume hiyo iko hivyo tangu kuumbwa kwa ulimwengu na hatuwezi libadilisha hilo.
Ila kitu kimoja nanyi wanaume mnajisahau sana jaribuni kutuheshim wake zenu maana tunajua dhahiri kuwa mnachepuka lakini msituonyeshe tafadhali fanyeni kwa akili na heshima,usipigiwe simu usiku,usitumiwe msg usiku,ukitumiwa picha futa,,hiyo simu yako ni yangu pia vipi nikishika nikakuta picha za ajabu za wanawake wengine?it hurts more.
Tambueni kwamba hakuna mwanamke mwenye akili timamu atachepuka endapo anatimiziwa kila mahitaji muhimu toka kwa mumewe na heshima anaipata wakati mwingine wanaume mnasababisha usaliti na mnajijua hamuwezi vumilia usaliti.
Nasi wanawake tuombe Mungu atupe uvumilivu na hekima ya kuhandle shida na namna sahihi ya kuzitatua