Wanawake muelewe; kwa Sisi Wanaume watoto wote sio Sawa. Tunawapenda na kubariki wale wanaotusikiliza

Wanawake muelewe; kwa Sisi Wanaume watoto wote sio Sawa. Tunawapenda na kubariki wale wanaotusikiliza

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
WANAWAKE MUELEWE; KWA SISI WANAUME WATOTO WOTE SIO SAWA. TUNAWAPENDA NA KUBARIKI WALE WANAOTUSIKILIZA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kutuzalia Sisi tunaweza kukushukuru Sana lakini linapokuja suala la Upendo wa Baba kwa Mtoto ni kipengele kingine.
Yaani Baba kusema sasa huyu ndiye mtoto wangu hiyo ni Hatua ya juu kabisa ya thamani ya Baba na mwanaume kwenye maisha yake.

Mwanaume anaweza akapata watoto hata kumi lakini asiwe na mtoto hata Mmoja. Sio kwamba kabambikiwa nope! Alipata watoto kweli kibaolojia lakini asiwe na mtoto hata Mmoja ambaye anasema huyo ni Mtoto wangu.

Wanawake hutuona wakatili Sana. Wakati mwingine hushangaa kwa nini wanaume hukataaga mtoto tangu akiwa tumbonk yaani hukataa Mimba badala ya kufurahia. Zipo sababu nyingi Sana lakini kubwa kuliko ni Ile Sababu ya ndani ya Mwanaume kusema sasa huyu ni mtoto wangu.

Mwanaume ili ampende Mtoto yaani aseme sasa huyu ni mtoto wangu au hawa ni watoto wangu kuna Sababu kuu mbili ambazo ni;

1. Kuzaa na Mwanamke wanaopendana Sana(wote Mwanaume na mwanamke wanapendana)
Mwanaume ikitokea akaoa au kuzaa na Mwanamke anayempenda Sana ni hakika mtoto anayezaliwa atampenda automatically.
Mwanaume anapopenda mwanamke Akili yake na Mawazo yake hufikiria Mpaka watoto wataozaliwa hata kabla hajalala na huyo mwanamke
Ni mwanamke wa ndoto zake.
Kama mwanamke alikupenda na wewe ulimpenda kikamilifu hapana Shaka yoyote hata watoto wenu watapendwa na Baba na kumpenda Baba Yao. Hata yatokee mazingira gani.

2. Mwanamke Kumtii na Kumsikiliza MWANAUME.
Ni wazi kuwa mwanamke kama anakusikiliza hata watoto utakaozaa naye watakusikiliza.
Na mtoto Kumtii na kumheshimu Babaake NI kuuteka Moyo wa Baba.

Mwanamke anaathari kubwa katika malezi na makuzi ya mtoto
Mwanamke asipokuwa msikivu na Akawa jeuri huathiri upendo wa Baba kwa Mtoto wake.

Kuna wakati mwanaume hujuta kuwa na watoto. Na wababa wasioeavumilivu husema Kabisa kuwa wao hawana watoto licha ya kuwa wanawatoto
Wanaume wengine huchukua maamuzi magumu Kutafuta watoto kwa Wanawake wengine kujaribu bahati yao kuona kama watapata angalau mtu wa kumuita Mtoto.

Moja ya mambo yanayowaumiza wanaume watu wazima ni suala la kukosa watoto wanaowasikiliza hata Mmoja.

WATOTO WA BABA WANASIFA ZIFUATAZO;

1. Ni Alpha Male.
2. Wanaheshimu Baba Zao katika mazingira magumu.
3. Ni marafiki wa Baba Zao. Huwaambii kitu kuhusu Baba Zao.
4. Hawanaga Kisasi na vita na Baba zao.
5. Ni walinzi wa Baba Yao.
6. Hawakubali kuingilia ugomvi wa Baba na Mama isipokuwa wao huwa wapatanishi.
7. Wanajua kuwa Ili wawe Baba na Mume Bora lazima wawaheshimu Baba waliowazaa.
Na ili wawe Mama na Wake Bora lazima wamheshimu Baba.

Kwa Sisi Watibeli kabla hatujaoa Mke lazima tujue huyo mwanamke tunayeenda kumuoa humchukulia vipi Babaake Mzazi.
Kwa sababu ni hakika vile anavyomchukulia Babaake ndivyo atakavyokuchukulia wewe.

8. Huunganisha familia na ndugu kuliko kuwatenganisha.
Watoto wa Baba ni wale wanaounganisha ndugu, jamaa na rafiki bila kujali kulikuwa na vita na migogoro. Hutafuta Nafasi ya kupatanisha wazazi na ndugu ili watu waishi pamoja.
Watoto wa hivi huitwaga watoto wa BABA

Na wengi ndio huachiwa familia na Baba zao bila kujali mtoto huyo ni wakike au wakiume ila Akiwa wakiume itapendeza zaidi. Ila kwa familia isiyo na kijana Basi wakike mwenye sifa hizo hupewa Mkoba na KUBEBA hiyo Familia.
Bila kujali ni Mtoto WA ndani au wa nje. Mtoto WA Mke Mkubwa au Mke mdogo.

Moja ya Hasara atakayopata mwanaume na Kufa mapema Kabisa au kuwa na uzee mbaya ni kukosa mtoto hata Mmoja.

Moja ya dalili kuwa familia Fulani Mzee Fulani Hana mtoto hata Mmoja ni kuangalia maisha ya Mzee MWENYEWE. Picha linaanza ametelekezwa, mwingine anatengwa na watoto wake.

Mtoto mwenye akili zilizotimia kamwe hatoweza kukubali Baba yake aishi maisha ya ajabu ilihali yeye anaishi maisha mazuri.
Watoto wa Baba hawapo hivyo. Nazungumzia Alpha Male.

Kizazi kisicho na Baba ni kizazi ambacho hakidumu. Hakiwezi Kupata mafanikio ya Muda mrefu.
Ni kizazi kitakachokuwa kinatumikishwa na familia au koo zingine zenye Baba.
Wapo baadhi ya watoto Wachache watakuwa wanaoteaotea mafanikio lakini wakiondoka ule ukoo unarudi kwenye umaskini Mkubwa tena.

Familia nyingi kubwa, zina Wababa.
Kwenye jamii au nchi yoyote Ile. Ili familia idumu walau kwa Karne kadhaa lazima watoto wawe watoto wa Baba.

Watoto wafundishwe kumheshimu Baba hata kwa namna yoyote Ile.

Tofauti na hapo, kizazi hiko kitaishia kuwa Watumwa wa familia na koo zingine zenye Wababa yaani wenye kumheshimu Baba.

Kitendo cha mwanamke kutaka kupewa sifa zaidi kuliko Baba mbele za watu ni dalili za Hatari Kabisa kuwa familia hiyo iko hatarini.

Mtoto mwenye AKILI na mwenye kuona Mbali, utukufu wake wa Kwanza lazima uanzie kwa Baba yake. Kisha mengine ndiyo yafuate.

Wanawake wenye Akili na wenye Maono.
Hata awe na uwezo Mkubwa Kiasi gani kumzidi Mumewe. Akisimama mbele za watu kuhusu mambo ya kifamilia lazima ampe utukufu Mumewe. Hata kama Mume ni goigoi.

Kuna watu hawawezi kunielewa hasahasa wale ambao wametoka kwenye familia za chini na wao ndio pengine wameotea mafanikio tena ya kutumikishwa na watu waliotokea kwenye familia zenye Baba(kumheshimu Baba).

Kuna wakati niliwahi kuandika, Mkeo asikuzidi umaarufu na nguvu. Andiko lile
Linaenda sambamba na hili. Ingawaje sio kila mtu anaweza kunielewa.
Mwanamke mwenye akili yeyote apitapo mbele za watu lazima ajitambulishe kwa jina la mumewe ili kukuza jina na heshima ya familia yake aliyoanzisha.

Swalk Linakuja, je wewe Baba yako anakutambua kama mtoto wake?
Je anajivunia?
Hapo ndipo ilipo Siri ya Mafanikio ya Muda mrefu na sio Yale ya mpito.

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mimi niliowazaa ndo najua uchungu wa kila mmoja wao. Hata kama hawakusikilizi wewe

Hatukuzuii wewe kuwa na uchungu
Ila kuuona uchungu wako nasi tuuone hapo ndipo nazungumzia

Sisi tunaona uchungu kwa watoto wanaotuheshimu, kututii na ambao Mama zao ni wake Bora kwetu
Hao kwa kweli Roho zetu zinatuumaga Sana tukishindwa kuwapa mahitaji Yao.
Lakini hatuumii kwa Sababu tuna watoto tuu waliozaliwa
 
Bond ya Baba na mtoto inatengenezwa lakini bond ya mama na mtoto ni automatic!!
So mtoto ni wa mama katika mazingira yoyote!

Sio kweli

Bond zote zinatengenezwa.
Wapo watoto hawakaa na Mama na hawana bond na Mama zao. Hata humu JF wapo na wanatoaga ushuhuda.

Vivyohivyo na kwa Wababa. Bond inatokana na makuzi na kuwa Karibu.

Ila mtoto mwenye akili bila kujali anabond au Hana na Baba yake ni lazima ahakikishe Baba anamkubali kwa kutenda mambo Mazuri
 
Sio kweli

Bond zote zinatengenezwa.
Wapo watoto hawakaa na Mama na hawana bond na Mama zao. Hata humu JF wapo na wanatoaga ushuhuda.

Vivyohivyo na kwa Wababa. Bond inatokana na makuzi na kuwa Karibu.

Ila mtoto mwenye akili bila kujali anabond au Hana na Baba yake ni lazima ahakikishe Baba anamkubali kwa kutenda mambo Mazur

Sio kweli

Bond zote zinatengenezwa.
Wapo watoto hawakaa na Mama na hawana bond na Mama zao. Hata humu JF wapo na wanatoaga ushuhuda.

Vivyohivyo na kwa Wababa. Bond inatokana na makuzi na kuwa Karibu.

Ila mtoto mwenye akili bila kujali anabond au Hana na Baba yake ni lazima ahakikishe Baba anamkubali kwa kutenda mambo Mazuri
Labda kama hajakaa nae kabisa huyo mama yake lakini kama ameishi nae automatic Tu bond inatengenezwa tofaut na Baba,Baba akijitenga kidogo Tu na mtoto ndo nitolee hivyo!!!!
 
Labda kama hajakaa nae kabisa huyo mama yake lakini kama ameishi nae automatic Tu bond inatengenezwa tofaut na Baba,Baba akijitenga kidogo Tu na mtoto ndo nitolee hivyo!!!!

Ukisema kitu kipo automatic huwezi kusema Mpaka akae naye.

Ukaribu ndio unaleta bond. Na sio zaidi ya HAPO.
Familia nyingi kubwa za kitajiri watoto wanaukaribu na Baba zao kuliko Mama zao
 
Bond ya Baba na mtoto inatengenezwa lakini bond ya mama na mtoto ni automatic!!
So mtoto ni wa mama katika mazingira yoyote!
Mtoto ni wa Baba maana baba ndo anatoa mbegu hii ni nature ndo maana watu wanoishi maisha magumu Sana hapa duniani ni single mother ambao wanapambana kuwaalisha watoto sumu kuwa baba zao ni wabaya.
 
Wazazi nao ni watu tu, hawajakamilika.

Hata kina mama wana upendeleo kwa watoto.

Hasara nyingine ya kuzaa kama sungura ndo hii.
 
Mtoto ni wa Baba maana baba ndo anatoa mbegu hii ni nature ndo maana watu wanoishi maisha magumu Sana hapa duniani ni single mother ambao wanapambana kuwaalisha watoto sumu kuwa baba zao ni wabaya.
Mliambiwa mtilie mkazo elimu, mkapuuza. Ona sasa haya mambo 👆 ya kuja kujiaibisha kwenye hadhara 🤦‍♀️

Reproduction.png
 
Back
Top Bottom