Wanawake ndoa ni utii, acheni kujaza ujinga wadogo zenu

Wanawake ndoa ni utii, acheni kujaza ujinga wadogo zenu

shida ni hao wanatoa mafunzo kwenye hizo media wanapewa airtime kuongea kuhusu ndoa na mashauri ya kuwaasa wanawake sijui wanatokeaga wapi maarifa yao kwenye maswala hayo wametoa wapi lakini ndio jamii inawasikiliza ........imefika wakati mwanaume ukimwambia mkeo kitu afanyi ata kama kizuri kisa tu itaonekana unamuendesha kweli hiyondio heshima
 
Paragraph ya mwisho ndo mnaishia kufa kwa stress au kujiua.

Tiba ya usaliti ni KISASI.
Siwezi kufa kisa mwanaume, aisee na ugali ulivyomtamu huu [emoji16][emoji16]. Kwani si ndo mana Kuna neno "kuachana" my dear?. Na kama ulisoma vizuri, nimesema kwamba "ukiona manyanyaso na mateso yamezidi ni haki yako kujisogeza pembeni na kulea watoto wako,ni marufuku kuvumilia manyanyaso na mateso. Ni sawa kuachia ngazi lakini si sawa kutenda Yale ambayo yeye anatenda ukifikiri kwamba unamkomoa mwanaume kumbe unajiharibia mwenyewe sifa yako mtaani. Kwa sababu mwanaume ni malaya na ww unageuka malaya, utakufa kwa magonjwa. Ilhali una uwezo wa kusogea pembeni ukafanya mambo yako. Kamwe usivumilie ukatili katika ndoa, imekushinda, basi sogea pembeni.
 
Pesa na elimu vikae mbali na ndoa jamani
Tunajazana ujinga nowdays mnoo....ila Kuna mwanamke kaolewa ukute anapowachonja wenziwe wasihudumie Waume zao Sasa!!!hahahaaa yeye kwake mpolee
Siku Moja shoga angu akaniambia weee!!!!twende kwake Fulani tumekuta anapika mmewe kaja kampokea vzr
Mzeee Sina hamu ,akaniambia za kuambiwa changanya na zako huyuu mnaafiki ukimsikia anavyopotosha wenziweee sasa
[emoji1][emoji1][emoji1] kweli za kuambiwa changanya na zako. We unafanya anayosema, kumbe mwenzio akifika kwa mumewe anapoa na huduma zote anampatia mumewe.
 
Assalamualaikum nnawatakia mifungo mema.

Dear girl child kama una malengo ya kuolewa ukae ukijua mwanaume ni kiongozi wa familia aliumbwa yeye ikapita miaka 40 ndo ukatolewa ubavu wake akaumbwa mwanamke. Mungu fundi hakuna sababu ya kuumba sote wawili mmoja ametokana na mwenziwee awe msaidizi wake, hizi feminists activities zinazoendelea ni kuharibu mpango wa Mungu.

Hakuna usawa kati ya mke na Mume isipokua katika kuutafuta ufalme wa mbinguni au kujua lengo la kuumbwa na namna ya kulifikia. Nyie mastrong sijui super woman msituharibie watoto wetu wa kike, asili ya mke ni heshima, mwanaume ni kiongozi wa mwanamke.

Tena siye waislam tunaambiwa kabisa Pepo yako iko kwa mumeo, kumtii mumeo ndo lango la wewe kuiona falme ya Mungu, haijalishi ni kibe10, kizee kikongwe whatever huyo Mume alivo mradi tu anawajaibika kama Mume na anabeba majukumu yake ya kiunaume.

Kuna Wanawake wakiwa nje wanapondea ndoa ila wakiwa Kwa waume zao wanatulia tulii wanafanya majukumu yao mpaka baasi ukiwasikiliza unapotea. Za kuambiwa changanya na zako, ewe mtoto wa kike
Kwenye ndoa hakuna kutoa taarifa kuna kuomba ruhusa Kwa mume, kwenye ndoa hakuna mashindani kuna maelewano.

Sijui lengo la wanaharakati wa ndoa ni lipi. Binti kama anapigiwa, anadhalilka na kufanyiwa unyama hapa hata akiresist ni sawa na ni bora talaka kuliko kuuana.

Wanaharakati wamezalisha kizazi cha wanawake wachepukaji, tusio walezi wazuri, waongo na unaafiki mwingi tunajifanya tunashinda kwenye nyumba za Ibada ila tuna machafu kibao. Ingawa Toka zamani uchepukaji ulikuwepo kwa jinsia ke ila Sasa imezidi tena sio Siri tena.

Kwa Sasa jamii zina macho lakini hazioani, zina masikio lakini hazisikii. Ifike mahala wanawake tujitambue na ktk kujitambua sio kudharau ndoa yako, hiyo ni dhambi kubwa sana tunafanya. Shida iliyopo wanaume wengi siku hizi wanakimbia majukumu yao ya ubaba na ulezi ni sperm donors tu, ila hiyo haifanyi sababu ya mwanamke awe juu.

Ukiona umeshindwa toka, Kaa pembeni lea watoto wako vizuri kabisaa kuliko kuishi na mtu asiyejitambua
Ila kama umepata mwenza muungwana mstaarabu mheshimu, mpende na jengeni familia yenu vizuri, achaneni na wanaharakati uchwara wenye stress na maisha yao.

Ndoa ni kitu kizuri na baraka Kwa wenye akili na uelewa tu.
Mpaka roho imeniuma yaani....

Siku nikikutana na Baba Minza lazima nimpe za uso. Alifanya upopoma sana na hatakaa apate Mwanamke anayejitambua hivi. Huko aliko si ajabu anapelekeshwa hatari na lisupa wumani limoja lililoshindikana...

Asante sana nkwela wane [emoji1545]
 
Kunahawa wanajifanya makungwi kufundisha watu
Thanks kupiga nyundo!!! kabisaa yaani Mimi hua pia nawaambiaga tujifunze kwa waliofaulu sio Kila mwanamme mbaya na sio Kila ndoa mbaya,zipo ndoa nzuri Tena both male and female Wana pesa but wanaheshimiana
Baadhi ya wanawake kuwapanda Waume zenu kichwani sio kanuni ya kidunia ,wanatuharibia watoto wa kike,50/50 haipo na haitakaa iwepo
Wazazi wetu walitusomesha Ili tujitambue ila sio kuja kuharibu mpango wa Mungu ndoa ziheshimiwa na watu wote
Kweli bint akitaka kuolewa wampeleke Kwa wamama walioshika dini na walio kwenye ndoazao wawafundishe mabint kulingana na mafundisho ya dini nani mwanamke majukumu yake na anatakiwa aishije

Sikuhiz wanatufanyia kitchen party kungwi mwanamke alieachika mara 8 anakuja kumueleza nn bint anaeingia kwenye ndoa akichanganya ya mafeminist akili uozo mtupu😂😂😂
 
Back
Top Bottom