Wanawake pindi mnapokuwa na miaka 17-25 kwanini huwa hamshauriki mkasikia?

Wanawake pindi mnapokuwa na miaka 17-25 kwanini huwa hamshauriki mkasikia?

Kama anajitambua na amemalizana na hekaheka za huko mabarabarani atafaidi sana wallahi. Nawaombea mpwa!

➡️➡️➡️ Akianza kukuzingua nipe nimpe nondo za wazee wa Kisukuma mpaka aombe poo 😂
Kwako lazima nimletee mpwa najua nondo za kutosha
Hapa atakaa tu sina muda mm wa kuanza kutafuta penz jipya 😃
 
KUNA MSHAURI MMOJA @ MAISHA HALISI TZ,

Aliandika hivi kwenye page yake



Ukiwa na miaka 17-19, utapoteza usichana wako, na kuanza kuongeza body counts.

Miaka 20-22, utaanza kuwaona wanafunzi wenzio ni wavulana wadogo kwasababu ya pesa na zawadi unazopokea kutoka kwa wazee wenye umri sawa na baba yako.

Miaka 23-25, ataanza kumezwa na mitandao, akishiriki kila challenge ya kubinua makalio, (internet haisahau)

Miaka 26-27, mwanaume mwenye nia ya dhati ya kumuoa, atamkataa kwasababu hayupo tayari kubanwa kwenye starehe zake.

Miaka 28-30, ataanza kuona rafiki zake wakiolewa, huku yeye akipata presha ya jamii kuwa anahitaji kupata mume kama wenzie.

Miaka 31-34, atakimbilia kanisani, akiamini ndugu Emmanuel atamuogopa Mungu hivyo hatojaji kuhusu historia yake iliyopita.

Miaka 35-37, atageuka feminist, na kujaribu kuwashawishi wasichana wadogo wawe kama yeye.

Utaanza kumuona mtandaoni akilaani kila kitu kuhusu wanaume, na namna ndoa ilivyo ni utapeli wa furaha.

Adui wa mwanamke ni umri, usikubali kuwa retirement plan ya mwanamke aliyekupuuza nyakati za ubora wake.

BY
#MadamKasema
@maisha_halisitz
Tukutane kwenye huduma zangu za ushauri na group la wachumba nichek WhatsApp no 0656832100
 
Wanaochezesha aviator wanacheza na akili za watu.

Uki-stake hela kindenge kinaanguka chap.
Ila usipoweka kidude kinahesabu mpaka 300.

Mchezo WA kuibia watu sijapata kuona😁😁😁👽
🤣🤣🤣 Tatizo ulimwacha Mungu,umemkana Mara tatu hata jogoo alipowika bado hukutubu
 
Hakuna shida. Yuko Medical School John Hopkins University ila mwezi wa tisa anakuja Bongo na wenzake 14 katika Study Abroad Program; na watakuwa hapo Taasisi ya Moyo ya JK. Hajui Kiswahili wala Kisukuma so wahi kwa Ras Simba kama kimalkia hakipandi. Na kwa mabinti zangu wala huwa sitozi mahari! 😂
Nimecheka kinoma mzee🤣Dah hii haina comeback

Sema Nina kingereza cha kuombea maji 🤣si haba
 
Wanaochezesha aviator wanacheza na akili za watu.

Uki-stake hela kindenge kinaanguka chap.
Ila usipoweka kidude kinahesabu mpaka 300.

Mchezo WA kuibia watu sijapata kuona😁😁😁👽
Kuwa mwangalifu sana. Ukizama huko kuondoka ni shida. Kimbia kungali mapema!

IMG_20250203_083051_758.jpg
IMG_20250203_083149_381.jpg
 
Nimelea mabinti 7 na madume matatu. Na wote walitoka vizuri tu hakuna aliyezingua kivile. Mabinti saba wote hakuna aliyepata mimba kabla ya ndoa na watano wako kwenye ndoa zao huko wametulia. Mmoja yeye anajitafuta kwanza na keshasema yeye hana hamu kabisa na kuolewa. Ka mwisho ndo kako chuo kanapambana na medical school. Madume hayo sasa ndo yako vizuri balaa; and we are just true buddies!

Siri kubwa niliyoigundua ni upendo na URAFIKI. Wewe baba jenga urafiki sana na mabinti zako. Yaani mpaka inafikia mahali wanakuwa na uhuru wa kukwambia cho chote. Upendo na urafiki huu ndiyo utakujengea heshima kwao na inafika mahali wanaona aibu kufanya kitu ambacho wanadhani kitakukasirisha; na au kukuvunjia heshima haijalishi kama upo nao au wako mbali. Na kamwe usitumie ukali tu na maguvu!

Unajengaje urafiki na mabinti zako?

Anza kwa kumpenda sana mama yao na kumfanya kuwa rafiki yako mkubwa. Na uonyeshe kwa vitendo. Na wewe na mama yao ni lazima muwe timu moja katika hili. Wakiona jinsi unavyom-treat mama yao itakuwa rahisi sana kwao kujenga ukaribu nawe mpaka mnakuwa washikaji wakubwa. Hiyo inakupa wewe nafasi nzuri ya kuanza kucheza na saikolojia yao changa na kuwa-mold unavyotaka wawe. Ukiweza na kuwaingiza kwenye mambo ya Mungu wakamjua Mungu vizuri basi unakuwa umemaliza kila kitu.

Hiki kibinti cha mwisho kitinda mimba kimeanza kudeti kinakuja kuniambia eti huyu kijana Anthony nimeanza kumkubali sana dad maana ni gentleman mno...ha ha ha nikacheka weeee! Nakiambia, 99.99% lengo kuu la Anthony ni kukupelekea moto tu hakuna kingine hivyo kuwa macho na hilo. Na hiyo inakuwa ni nafasi nyingine ya ku-cement ambacho tayari tulishaongea kuhusu hiyo ishu ya kupelekewa moto kabla ya ndoa; na athari zake.

Usilazimishe watoto wako wakuheshimu. Wapendee sana mama yao. Jenga urafiki nao. Wasogeze kwa Mungu...kazi kwisha! 🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️
Mkuu hongera sana Kwa Hilo. Lakini mwanangu Hadi afikie hatua ya kuniambia katongozwa na Fulani nankamuelewa kwangu ni hapana.
 
Back
Top Bottom