Watu kama wewe mnaowadanganya hawa mabinti hamjielewi.
Na mmesababisha hawa mabinti kuamini kwenye mapenzi kunalipa kuliko kufanya kazi.
Leo hii tunawahitimu wa vyuo ambao mawazo yao ni kupata danga limnunulie Iphone kali, limpangishie nyumba nzuri n.k nasio kutumia maarifa waliyonayo kujitegemea.
Mnawadanganya hawa mabinti, sasa wamekuwa makahaba kwa kigezo cha kutafuta wanaume wenye pesa nasio kufanya kazi wajitegemee. Ili apate pesa nyingi inamlazimu kuwa na wanaume wengi.
Binti akitoa penzi apewe penzi nasio atoe penzi apewe penzi na Pesa.
Moja wapo ya vitu vinatufanya tuendelee kuwa masikini ni pamoja na hili, kuna kundi linaweza kufanya kazi na kuzalisha ila limegeuka kundi tegemezi, lenye tabia za kimalaya malaya limekuwa ombaomba.
Tukiendelea kushabikia huu ujinga tutakuwa na Taifa la washenzi wanaowekeza kwenye kujipodoa, kufuga kucha na mawigi, kutoa mimba wakiamini watapata nyumba na magari.
Wahimizeni wanawake wafanye kazi ili wasigeuze mahusiano kuwa kitega uchumi