Kama hayo mahusiano ni mutual and fair, kwanini mwisho wa siku wakiachana halafu mwanaume akachelewa kuoa, na mwanamke akachelewa kuolewa anayetukanwa ni mwanamke
Na kwanini kwenye hayo mahusiano ikitokea wamepata mtoto, wakija kuachana anayetukanwa ni mwanamke na kuitwa single mother, ushawahi sikia mwanaume anatukanwa ni single father
Na kwanini kwenye hayo mahusiano ikitokea wameachana, halafu kila mmoja wao akapata mtu mwingine, mwisho wa siku anayetukanwa kuwa anabadilisha wapenzi na kuitwa malaya ni mwanamke
Na kwanini hamtaki haki sawa ikiwa mnalazimisha na wanawake nao watafute pesa kama mnavyotafuta ninyi, kwanini hamtaki haki sawa na kusema kwamba mwanaume na mwanamke hawawezi kuwa sawa, bado mnataka muwatawale ila hapo hapo mnataka majukumu sawa
Na kama hilo tendo wote mnalifaidi kwa usawa, kwanini wanaume ndio wana uhitaji mkubwa sana wa hilo tendo kuliko wanawake kiasi cha wao kulihangaikia sana kwa kutoa pesa, na je wanawake wakiacha kuwaombaomba pesa ndio mtawaheshimu na kuacha kuwachezea