Sister Abigail
JF-Expert Member
- Sep 2, 2020
- 4,817
- 14,925
Mtetee but ukiangalia Kwa kina ni kama mtu alieumizwa na ana vinyongo au machungu.Hii ni kama elimu tu haina mwisho kila siku inapaswa akili ipate jambo jipya ili kuendana na mazingira yanavyotaka,kingine wewe unaona ni mgogoro kwa sababu haupo upande wa kiume ukiona vipi anzisha na wewe darasa uwaelimishe wanawake wenzako yale unayajua.
Kwanini unadhani mtu kukataliwa ni lazima awe amekosa hela?mtu anaweza akakataliwa kwa sababu anaonekana smart kichwani haendekezi ujinga ujinga anaoletewa na mwanamke so hapa haachwi kwa sababu hana hela anaachwa kwa sababu ana akili nyingi.
Hata wanawake humu tunapitia magumu lakini huwezi Kuta Jan-Dec mada zake ni kuwasema wanaume...
Kama anawapa elimu mbona haandiki mazuri?au wanawake wamejaa mabaya tu?