Wanawake ukiona mume kakosa cheo mshukuru Mungu mke wa Rais Moi yalimkuta

Wanawake ukiona mume kakosa cheo mshukuru Mungu mke wa Rais Moi yalimkuta

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,900
Reaction score
52,056
Rais Moi na mkewe walioana wakiwa watu wa dini sana. Walikuwa walokole wakisali kanisa la African Inland Church.

Moi alipopanda cheo kuwa Makamu wa Rais wa Kenya tatizo kwenye ndoa likatokea hadi kusababisha ndoa kuvunjika.

Tatizo lenyewe lilikuwa Moi alianda sherehe ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Kenya Jomo Kenyatta. Akaja na mkewe Mama Ngina Kenyatta

Sherehe ile ilisindikizwa na muziki wa dance. Moi akainuka akaenda kumchukua Mama Ngina Kenyatta wacheze muziki wakaanza kusakata rumba.

Rais Kenyatta naye akaenda kumshika mke wa Moi ili wacheze naye muziki. Mke akagoma akasema yeye mlokole miziki ya kidunia kwake mwiko.

Alipogoma Rais Kenyatta akamuacha akamwambia Moi Mkeo kakataa tusicheze wote tena kaongea kwa sauti.

Moi akajaa mihasira ya kufa mtu akamwambia utacheza naye huchezi akasema sichezi wakaanza kufokeana. Mke akasema yaani wewe umeharibika kiasi hiki.

Moi toka siku ile akamtoa Ikulu akamswaga shambani huko porini hadi alipompa talaka rasmi.

Waliishi tu vizuri na kuzaa watoto nane lakini cheo kilipopanda tu ndoa ikafa.

Mara nyingine kidume kikikosa kupanda cheo mwanamke piga goti mshukuru Mungu. Habari ndio hiyo.
 
Mkewe Moi yupo hai? Kama yupo hai atakuwa anashangaa namna Walokole wanavyokata rumba (dance) ni zaidi wa wanenguaji wa Pepe Kale na Koffi Olomide.

Ni vizuri kusifu na kuimba ila now days hali ni mbaya sana hasa kwenye haya makanisa yanayoibuka kama uyoga.
 
Mkewe Moi yupo hai? Kama yupo hai atakuwa anashangaa namna Walokole wanavyokata rumba (dance)......ni zaidi wa wanenguaji wa Pepe Kale na Koffi Olomide......

Ni vizuri kusifu na kuimba ila now days hali ni mbaya sana hasa kwenye haya makanisa yanayoibuka kama uyoga.
Geuka umkumbatie jirani yako....au ile ya Mwamposa anakwambia Ailavyuu halafu mnamjibu ailavyuu tuu ......mlokole wa miaka ya 70 ataona maruweruwe tu
 
Mkewe Moi yupo hai? Kama yupo hai atakuwa anashangaa namna Walokole wanavyokata rumba (dance)......ni zaidi wa wanenguaji wa Pepe Kale na Koffi Olomide......

Ni vizuri kusifu na kuimba ila now days hali ni mbaya sana hasa kwenye haya makanisa yanayoibuka kama uyoga.
Namkumbuka mzee mmoja, haya mabadiliko ndani ya kanisa yalikuwa yanampa tabu sana, kwanza lilipokuja la wanawake kuanza kuhudumu, alikua anaahungulia kanisani, akijua mhubiri ni mwanamke anasepa.

Likaja hili la vyombo vya muziki katika kwaya, likamtoa imani kabisa.

Ikafika mahali kanisani lazima aende lakini mambo yaliyokuwa yakiendelea yanamkwaza, akapata option, kuwa akifika tu kanisani baada ya liturujia, basi analala mpaka ibada inakwisha wanamuamsha anaondoka zake.
 
Duuh aisee,maana saizi mziki ukipigwa watu wanasahau kabisa kuwa wapo church,anayeenda kwenye mkesha na anayeenda club kwenye suala la mziki ni sawa tu
 
Mke nae labda alileta tafrani sana mbele ya kadamnasi...labda angekataa kimya kimyaaa

shida nadhani sio cheo...ila ni mama kutoenda na wakati..alishaona mumewe kamfata mke wa mwenzie ye kashindwa nini kumchukua mume wa mwenzie wacheze kidogo..ni funzo pia...tuyasome mazingira
 
Back
Top Bottom