IDEGENDA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 4,492
- 5,350
Hiyo atakuwa mlutheri wa miaka ya 50Namkumbuka mzee mmoja, haya mabadiliko ndani ya kanisa yalikuwa yanampa tabu sana, kwanza lilipokuja la wanawake kuanza kuhudumu, alikua anaahungulia kanisani, akijua mhubiri ni mwanamke anasepa.
Likaja hili la vyombo vya muziki katika kwaya, likamtoa imani kabisa.
Ikafika mahali kanisani lazima aende lakini mambo yaliyokuwa yakiendelea yanamkwaza, akapata option, kuwa akifika tu kanisani baada ya liturujia, basi analala mpaka ibada inakwisha wanamuamsha anaondoka zake.
Sent using Jamii Forums mobile app