Mwanamke mwenye kazi, mshahara mnono, nyumba na gari, hawezi kumuheshimu mumewe vile inavopaswa.
Ndoa ni kama taasisi ya kitapeli ambayo mwanamke anaitumia kukidhi mahitaji yake. Kinyume na hapo, mwanamke hana haja na ndoa.
Kuna dada mmoja ni mwanasheria yupo Arusha, hawezi japo kumpikia chai mumewe. Muda wote yuko kazini, na akirudi hana muda.
Anajua mumewe ni kama kikaragosi ambacho hakimtishi kwa lolote.
Kwa mantiki hiyo, nihitimishe kwa kusema kwamba, unyenyekevu wa mwanamke katika ndoa ni danganya toto ili aweze kuendelea kupata mahitaji yake ikiwemo chakula na mavazi.
Akifanikiwa kuvipata hivyo bila usaidizi wako, atakunjua makucha yake rasmi akucharange kama shumileta.
Unyenyekevu ni utapeli. Hadaa ya kuchuma mali.
Mwanamke mwenye fedha ni mwanaume mwenzio. Ukimkoromea anakucharaza bakora.
MY TAKE: Wanawake wafukuzwe kazi.
Anyway...............
Ndoa ni mojawapo wa taasisi mbili zilozo anzia Eden, ya pili ni sabato
Hivi vitu viwili vinapigwa vita sana na shetani mwenyewe. na kuna kundi kubwa limekuwa recruited kushambulia hizi tasisi . utaratibu upo namna mume na mke wanaweza kuhusiana bila mgongano. kila mmoja ana majukumu yake
ni sawa na magari yanapokuwa barabarani. magari yanayoenda yana upande wake na yanayorudi yana upandea wake.
Ukilazimisha kuendesha gari upande usio wako utaleta taharuki na ajali
wanaume tubaki na majukumu yetu na wanawake wabaki na ya kwao
Baada ya Hawa kushawishiwa na kula tunda na kumlisha mumewe Adamu, Hawa aliambiwa atazaaa kwa uchungu na mumewe atamtawala.
Uhusiano wa mke na mume ni uhusiano wa mtawala na mtawaliwa. naomba ubaki hivyo
Mwa 3:16 SUV
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo,
naye atakutawala.
Waefeso 5:22-33
Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana. Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake. Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote. Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake. Alifanya hivyo ili kwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada ya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji, kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safi kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo. Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. ( Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake; badala ya kuuchukia, huulisha na kuuvika. Ndivyo naye Kristo anavyolitunza kanisa, maana sisi ni viungo vya mwili wake). “Kwa sababu hiyo, mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja.” Kuna ukweli uliofichika katika maneno haya, nami naona kwamba yamhusu Kristo na kanisa lake. Lakini yanawahusu nyinyi pia: Kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.