Kwa maelezo yako hizo zinaweza kuwa dalili za tatizo linaloitwa secondary Dysmenorrhea. Haya ni maumivu makali na muda mwingine huweza kudumu kwa kipindi kirefu zaidi ya kipindi cha hedhi na yanatokea wakati wa hedhi. Baadhi ya wanawake hufikia hatua ya kulazwa hospitali hadi muda wa hedhi utakapoisha.
Wanawake wengi wenye maumbo yanayowavutia wanaume mara nyingi huwa na tatizo hili (utafiti wangu) na isitoshe nawe una umbo la namna hii[emoji23]
Sababu kuu ya tatizo hili inakisiwa kuwa ni ulemavu wa kiungo katika mfumo wa uzazi (disorder in the reproductive organs). Ninaweza kukubaliana na makisio haya kwa sababu wanawake wengi, kama siyo wote, waathirika wa hali hii, huwa wanayo shida ya kupata watoto.
Hivyo, ninakushauri. Tafadhali, kutana na daktari bingwa wa magonjwa ya kinanama kwa ushauri zaidi wa kitabibu. Achana na bush doctors la, sivyo, utakuja kujuta baadaye.
POLE SANA.