Wanawake wenzangu mnazoeaje maumivu haya ya tumbo?

Wanawake wenzangu mnazoeaje maumivu haya ya tumbo?

Status
Not open for further replies.
Pole sana dear, nadhani wanawake pekee tunayoyapitia hayo ndiyo tunakuelewa zaidi, unaweza umwa mpaka ukaulaani ukoo wa shetani na wajukuu wake wote,

Halafu ninyi kina Babu Fyee na wenzio ambao mtu anaelezea ugonjwa ninyi mnadindisha ovyo ovyo kama jogoo, mngekuwa madaktari wa magonjwa ya wanawake mngefanyaje majukumu yenu..??
 
Niliwahi kuskia uzile wa kuchemsha ni mzuri kwa tumbo la P. Ila pia tumia panadol special za P zile kubwa unawekaga kwenye maji zinachemka kama dawa za gesi. Sijui sasa kama TZ zipo zile. Hivi juzijuzi nilimskia mtu anasema toothpaste za forever living pia nzuri unaweka kdg kwenye maji unachanganya then unakunywa. Jarib ivo na Mungu Atakusaidia, pole sn
 
Kama umewahi kumtenda mwanaume katika maisha yako amini nakuambia tafuta namna yyt ya kupata suluhu naye. Mama yangu mdogo alipatwa na hali kama hii uliyoelezea alihangaika mno! Kumbe kuna jamaa kafanya mambo yake.

Nilikuwa-ga mbishi mno kwenye mambo ya kuamini kuwa ushirikina upo, ohoooooo!! Dunia ina mambo mengi
Kwamba😳😳😳🤔
 
Habari ya asubuhi,

Wenzangu huwa mnazoeaje haya maumivu jamani?😓😓

Yaani iko hivi, tumbo linauma kama mtu yupo tumboni anavutavuta utumbo, yaani kama yuko na kijiko anakwangua ukoko kwenye sufuria vile. Sasa ushuke chini kiuno jamani, ni kinakamaaa kama sijui nini, ukijinyoosha tu maumivu yake ni shida khaa!🤨🤨

Kuja sehemu nyingine huku chini ni kama sindano zinachomwa chomwa huko ndani, ni full shida yaani haaaa.😭😭😭 Hapo bado uje kwenye matiti ni yanauma jamani,😥😥 yamesimaa halafu ni mekundu, yaana moto kama sijui kitu gani yaani, bra yenyewe nimepata shida kuvaa maana nikivuta tu mkanda nasikia maumivu sio ya nchi hii.

Yaani nimekunywa dawa zote unazozijua za kutuliza maumivu lakini wapi.😓😓 Wakasema ninywe maji ya moto ila nakaribia kumaliza chupa hapa lakini sioni dalili ya maumivu kupungua, mkojo tu unabana nikienda chooni kuchuchumaa nako tabu haaaa!😖😖

Yaani hapa niko ofisini siwezi kukaa, natembea tembea tu muda wote, nasubiri kila mtu aingie ofisini kwake nibebe PC yangu nikajilaze kwenye kochi la wageni pale reception. Maana nina tabu jamani kusimama muda wote, nikisema nikae yaani kama nakalia sindano haaa!😭😭

Wenzangu mnawezaje kuzoea, maana mimi nashindwa jamani? Sijui Mungu aliwaza nini kuniumba wa kike, naumia mwenzenu, 😥😥😥nifanyeje eti?
Kienyeji nakushauri, kama kuna mwanamke wa kihaya mtu mzima jirani yako, muone akumalizie matatizo yako.

Inaweza kuwa UTI tu inakusumbuwa au kingine chochote. Wanawake (watu wazima) wa kihaya ni mabingwa kwa mambo hayo.
 
Yani hapo Hadi litulie ndo kichwa kinatulia hasira Sasa mwee mtu akikusalimia unaona kama amekutukana
😀😀Sikumoja niliumwa rafiki yangu alichanganyikiwa akaenda kuwaita watu acha wajae kakazangu alafu sijavaa vizuri nyie 😂😂😂
😂😂😂😂🙌
 
Acha kulalamika wewe hiyo ni hali ya kawaida kabisa. The more unaiona hali ya ajabu na ndivyo itazidi kukufanya ujione mgonjwa.

Miaka ya nyuma bibi na mama zetu hata tulikuwa hatujui kuwa wanapitia hali hizi ila walijikaza na kuyapotezea hadi miili yao ika adopt na ikawa ni kitu cha kawaida sana kwao kiasi kwamba ukilalamika wanawake wenzako wanakushangaa na wanaweza kukucheka.

Ila mabinti wa miaka hii changamoto kweli eneo hilo, mnadeka utadhani hizo hali ni za kubambikiwa au mlipewa kama adhabu kumbe ni maumbile tu. Jifunzeni kukubaliana na asili yenu utaona hata mwili una anza kuadopt na hautakuwa unakuwa sensitive na hiyo hali.

Najua mtamind ila huo ndio ukweli.
Asante kwa ushauri mzuri kiongozi 🙏🙏
 
Usipende kusikiliza watu wa mitaani tumia dawa flani, tumia kile.
Wauzaji wa duka za dawa za mitaani wanatoa dawa ovyo bila prescription.
Bila kujua historia ya magonjwa, wanatoa dozi kubwa sana.
Hiki no chanzo kikubwa cha matatizo ya figo na moyo.

Zinafuatia dawa za kienyeji. Hizi zinaua Sana figo za watu.

Ukipata bahati kukutana na daktari bingwa wa matatizo ya figo au moyo muulize kuhusu hili utanikumbuka.
Asante kwa ushauri mzuri kiongozi
 
Polee dear
Tumia dawa ya (Complete phyto-energizer) supplements

Au kila unapo maliza P tumia karafuu, chemsha kunywa for 7 days asubuhi kabla haujala chochote

Kuna watu wamefanya hivyo wakapona wengine haikuwasaidia.
Asante sana kipenzi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom