BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,767
- 23,198
Mwiaho wa siku kila mtu apambane na fallopian tubes zake ili kuondoa lawama
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwanini mnaenda kuoa wanawake halafu unamletea watoto wako? je na yeye akileta wa kwake utampenda?
100% mwanaume mwingine ana uwezo wa kumpenda mwanao kama vile ni wake
ila hamna mwanamke wa kumpenda mtoto wa mwanamke mwingine (tena aliezalishwa na mume wake)
kama wake aliyemzaa.
Uwezo huo wanao wanaume TU.
Cha utundu ntamfinyaa masikiooo😂😂😂acha nimlete kale ka cha utundu wangu huko kale good time
Wanawake walezi walikuepo zamani enzi zile za mtoto wa mwenzio kama mtoto wako ila asahivi tabu tupu wanawake wamekua wa hovyo sana dahh!!
upo sahihi sanaHata hao wa zamani walitesa sana watoto na kama hawakuonekana kufanya hivyo basi ni kwasababu ya umasikini uliokithiri waliokuwa nao (hawakuwa na namna)
Wanawake wa zamani walitesa watoto balaa basi tu mitandao ya kuwasema haikuwepo.
Japo hapo kwa kumpa house girl wanao mi naona ni yale yale tu
Halafu ni bora ungekua na katoto kamoja then ndio house girl amleleee (kidogo afadhali)
ila kama una watoto zaidi ya mmoja Amini kwamba House girl hawezi wapenda watoto wote wawili au watatu upendo sawa
yupo ataependelewa yupo atae onewa (house girl ni binadamu nae)
Malezi perfect yanatoka kwa REAL MAMA pekeee no any other place.
uko sahihi mkuuHongera kwa mada nzuri mkuu, lakini nipende kuongeza au kutofautiana na wewe katika hili, kimsingi hakuna malezi PERFECT, hata kati ya mama na mtoto hajawahi kuwa perfect. Kinacholeta hiyo hali ambayo tunai-percieve kama “perfection” ni UPENDO mkuu uliopo kati ya mama na mtoto. Mama na mtoto hata wakikoseana vipi automatically makosa yanafutika sababu ya upendo usio kuwa na mipaka, hisia zangu zinaniambia hakuna upendo unaoweza kuzidi huu wa mama na mtoto.
Tukija kwa upande wa wenzetu ambao wanalea watoto wa kambo, wapo wanaolea vizuri sana na sio wachache kama mnavyotuaminisha humu, binafsi nimewashuhudia lakini kinacholeta mushkeli ni ile hali ya jamii kuwa sensitive juu ya “u-kambo wa mtoto”. Kwamba hata huyu mama afanye namna gani bado lawama zitakuwa juu yake hata kama anafanya yale yale anayofanya kwa watotowe.
Sijakataa kuwa kuna wanawake wana roho mbaya na za ajabu kupata kutokea.
Kwa sisi tuliokuliaa polygamy family tunayajua haya vizuri sana, yaan unanyanyaswa mpk unajiona kabisa unastahili kufa na si vinginevyoUkitaka kuwalea watoto wako usioe. Tafuta housegirl alee watoto wako kama unataka kuoa tafuta nyumba nyingine ukae na huyo mwanamke tofauti na hapo watoto wako watateseka sana. Hawa wanawake ni wazuri sana kuwaona yaani hata ukimuoa mgumba bado watoto wako watateseka sana. Mwanaume anaweza kuishi na mtoto siyo wake vizuri bila matatizo yoyote ila kwa mwanamke kati ya wanawake 200,000 unaweza kumpata mmoja tu naye ni mcha Mungu.