Wanawake wote ndivyo mlivyo hata mkikataa. Wanaume kuweni makini katika maamuzi yenu

Wanawake wote ndivyo mlivyo hata mkikataa. Wanaume kuweni makini katika maamuzi yenu

usijaribu na mshukuru Mungu kwa kusaaidia mipango igonge mwamba

Mlee mwanao huko huko akiwa kwa mama ake.
Ni Vizuri kuwa na Mifano hai wanaume tuliozaa kabla ya ndoa mkuje mm nina mtoto mkubwa amelelewa kabla wengine hawajazaliwa mambo mengine ni nadharia zaidi na kukuzwa
 
Sijakutana na sina uzoefu kwenye hili ila sidhani kama naweza kumtesa mtoto asie na hatia.

Nilichoona mimi wanawake wengi wako tayari kulea watoto waliowakuta wameshazaliwa kwa roho nyeupe kabisa...... tatizo linaanziaga pale ambapo mwanaume anaendeleza mahusiano na mzazi mwenzie au analeta watoto wadogo kuliko umri wa ndoa yake.
Binti yangu mkubwa nimempata kwingine nimeishi nae toka akiwa na miaka 4 yuko kidato cha 3 zipi changamoto ila ni ndogo sana kama ulivyosema mara nyingi watoto ndo wana tatizo la Kujimwambafy ila tumekuza ......likizo anaenda kwa mama yake na sis tuna wasiliana openly kuhusu makuzi ya mtoto
 
Uko sawa Mkuu.....Haswaaaa
Hamna mahali popote pameandikwa mwanamke utakae zaa nae ndio unatakiwa umuoe awe mke waako wa ndoa"hakuna".

Ila pia hakuna mahali pameandikwa kwamba mwanamke utakae mzalisha usimpende wala usimpe huduma zote muhimu "hakuna"

Mwanaume unaweza kuwa ulishawahi kuwa na mtoto kwa mwanamke ambae si mkeo kwa sasa so kutokana na kujitambua kwako ukaona uendelee kutoa huduma zote za muhimu kwa mwanao kwasababu unajua fika ile ni damu yako,na hakuna mwingine wa kufanya hivyo zaidi yako.

Bahati nzuri ni kwamba mama mtoto wako (yule x) Anaolewa na mwanaume mwingine na Maisha yao kiuchumi si mazuri. Hata wewe umeona,unaamua kumwomba mama mtoto wako (yule x) umchukue mtoto ili asiteseke unamleta mwanao. Kuja kulelewa na mkeo nyumbani (makosa makubwa sana haya)

Acha nikwambie kitu,

Mkeo hatakwambia simtaki huyo mtoto (ila moyoni mwake kashakwambia)

Mkeo hatokwambia hapendi hata kumuona huyo mtoto (ila moyoni mwake jua hampendi)

Mwanaume wewe unamleta mwanao ukiamini atapata upendo kama wa kwa mama yake (unajidanganya)

Hata kama mama mtoto wako (yule x) utamuona anapitia maisha magumu kwa asilimia 200 usije thubutu mpokonya mtoto. Uje umlete kwa huyu mkeo ulie nae,Pamoja na shida atakazopitia mama mtoto wako (yule x) hatoruhusu shida zile zimpate

Mwanae na hata kama zikimpata mwanao mama yake atajua jinsi ya kumpa maneno mazuri ya kumbembeleza ajione naye yupo kawaida. Wanaume nataka tu muelewe jambo 1 hao wanawake mliowaoa (anakupenda wewe tu) usije jidanganya atampenda.

Mtu mwingine tofauti na wewe na wanae wa kuwazaa. Jitahidi uwezavyo kama una mtoto nnje na ulikua na mpango mwakani (umchukue uje uishi nae), acha maana unamleta jehanam mtoto wako mwenyewe (usijipe moyo kwa matendo yanayofanywa na mkeo ukiwepo) acha huo ujinga.

Muache mtoto wako huko huko kwa mama ake kama ni matumizi mtunze akiwa huko huko kwa mama ake. Kama unahisi unampenda sana huyo mwanao hutaki ateseke (mrudie mama yake muoe). Sasa jitie kichwa ngumu (mletee mkeo mtoto wa mwanamke mwenzie) utaona what next.

Wanawake ndivyoo hivyo walivyo, waelewe then ishi nao kwa akili mingi mingi.

View attachment 1249705
 
ila BABA ukirudi nyumbani mtoto huyo huyo aliekua akifinywa mashavu ukiwa haupo

utamuona mama (mkeo) akimuita na kujifanya anampakata na kujitia anamdekeza (basi hapo mwanaume unaona yeees)

Kumbe zote zuga tu, ukiondoka kazini mambo ni yale yale.

Ni basi tu watoto hawawezi kusema kwa kuogopa vitisho alivyopewa (ole wako baba ako akija nikuone fyoko fyoko fyoko)
Mkuu Umemaliza kabisa
 
Unamwogopa mwanamke unayeishi naye ndani, unamwamini mwanamme mwingine aliyemuoa huyo ex akulelee mwanao nawe unakenua kwa amani kabisa.... huwezi kuwa sawa kichwani kuna namna dishi limecheza tu.
Yani wanaume sisi ni watu wa ajabu sana, mkeo au demu wako unaweza usimwachie simu, Mwanao au ATM card yako, ila UNAMPA DUSHE ANYONYE, bila kuhofia analing'ata abaki na kipande mdomoni.
 
Hongera kwa mada nzuri mkuu, lakini nipende kuongeza au kutofautiana na wewe katika hili, kimsingi hakuna malezi PERFECT, hata kati ya mama na mtoto hajawahi kuwa perfect. Kinacholeta hiyo hali ambayo tunai-percieve kama “perfection” ni UPENDO mkuu uliopo kati ya mama na mtoto. Mama na mtoto hata wakikoseana vipi automatically makosa yanafutika sababu ya upendo usio kuwa na mipaka, hisia zangu zinaniambia hakuna upendo unaoweza kuzidi huu wa mama na mtoto.

Tukija kwa upande wa wenzetu ambao wanalea watoto wa kambo, wapo wanaolea vizuri sana na sio wachache kama mnavyotuaminisha humu, binafsi nimewashuhudia lakini kinacholeta mushkeli ni ile hali ya jamii kuwa sensitive juu ya “u-kambo wa mtoto”. Kwamba hata huyu mama afanye namna gani bado lawama zitakuwa juu yake hata kama anafanya yale yale anayofanya kwa watotowe.

Sijakataa kuwa kuna wanawake wana roho mbaya na za ajabu kupata kutokea.
Miss you na nakuunga mguu. Kuna ile hali kama ya kuviziana/kutokuchukuliana mapungufu maybe kwa sababu ya kutokuwa na Ile "natural bond" kati yenu. Mama anaweza akamkosea mtoto ile kikawaida tu, lakini mtoto akachukulia kuwa kanifanyia hivi kwa kuwa sio mama yangu. Na kuna wakati mtoto anakosea tu, ila mama anaona huyu mtoto ananifanyia makusudi kwa sababu mimi sio mama yake. Au mtoto akidevelop tabia mbaya fulani, mama anahisi ooh anataka kunikomesha au atakuwa alifundishwa vibaya kwa mama ake alivyoenda likizo ili anikomeshe; so watanikoma.

Na hata sisi jamii na ndugu tunachangia kuleta migogoro kati yao, kwa kupenda kufuatilia au kujudge nini kinafanyika humo ndani na wakati mwingine hadi tunauliza kabisa "eeh anakupa chakula, hakufokei"? etc. Hivi kuna mzazi ambaye hajawahi kumfokea mwanae?. Kuna wamama wapo strict tu kwa nature yao, hata watoto wake wenyewe wanamuogopa, lakini akileta huo ustrict kwa watoto wake wa kambo, inaonekana kama anamfanyia roho mbaya. Na hata watoto hawawezi wote kuwa wema wakati wote, na wao wana mapungufu yao; ila ni rahisi kwa mama wa kambo kusema "huyu mtoto kanishinda simtaki kwangu" at the same time unaweza akawa na mtoto kibaka lakini kwa sababu ya upendo akasimama naye katika usumbufu wake wote na akamvumilia.

Ubaya sasa kwa mfano mtoto akienda kushtaki kwa ndugu huko, hakuna atakayetaka kuleta suluhisho, rather atachochea moto zaidi. Ni rahisi kuuchukulia/kuuignore udhaifu wa mtoto/mzazi yako, lakini akiwa wa mwenzako hali inakuwa tofauti kabisa. Hapa pana tatizo kubwa sana, na panabomoa sana.
 
Hamna mahali popote pameandikwa mwanamke utakae zaa nae ndio unatakiwa umuoe awe mke waako wa ndoa"hakuna".

Ila pia hakuna mahali pameandikwa kwamba mwanamke utakae mzalisha usimpende wala usimpe huduma zote muhimu "hakuna"

Mwanaume unaweza kuwa ulishawahi kuwa na mtoto kwa mwanamke ambae si mkeo kwa sasa so kutokana na kujitambua kwako ukaona uendelee kutoa huduma zote za muhimu kwa mwanao kwasababu unajua fika ile ni damu yako,na hakuna mwingine wa kufanya hivyo zaidi yako.

Bahati nzuri ni kwamba mama mtoto wako (yule x) Anaolewa na mwanaume mwingine na Maisha yao kiuchumi si mazuri. Hata wewe umeona,unaamua kumwomba mama mtoto wako (yule x) umchukue mtoto ili asiteseke unamleta mwanao. Kuja kulelewa na mkeo nyumbani (makosa makubwa sana haya)

Acha nikwambie kitu,

Mkeo hatakwambia simtaki huyo mtoto (ila moyoni mwake kashakwambia)

Mkeo hatokwambia hapendi hata kumuona huyo mtoto (ila moyoni mwake jua hampendi)

Mwanaume wewe unamleta mwanao ukiamini atapata upendo kama wa kwa mama yake (unajidanganya)

Hata kama mama mtoto wako (yule x) utamuona anapitia maisha magumu kwa asilimia 200 usije thubutu mpokonya mtoto. Uje umlete kwa huyu mkeo ulie nae,Pamoja na shida atakazopitia mama mtoto wako (yule x) hatoruhusu shida zile zimpate

Mwanae na hata kama zikimpata mwanao mama yake atajua jinsi ya kumpa maneno mazuri ya kumbembeleza ajione naye yupo kawaida. Wanaume nataka tu muelewe jambo 1 hao wanawake mliowaoa (anakupenda wewe tu) usije jidanganya atampenda.

Mtu mwingine tofauti na wewe na wanae wa kuwazaa. Jitahidi uwezavyo kama una mtoto nnje na ulikua na mpango mwakani (umchukue uje uishi nae), acha maana unamleta jehanam mtoto wako mwenyewe (usijipe moyo kwa matendo yanayofanywa na mkeo ukiwepo) acha huo ujinga.

Muache mtoto wako huko huko kwa mama ake kama ni matumizi mtunze akiwa huko huko kwa mama ake. Kama unahisi unampenda sana huyo mwanao hutaki ateseke (mrudie mama yake muoe). Sasa jitie kichwa ngumu (mletee mkeo mtoto wa mwanamke mwenzie) utaona what next.

Wanawake ndivyoo hivyo walivyo, waelewe then ishi nao kwa akili mingi mingi.

View attachment 1249705
Asante sana mkuu kwa ujumbe.
Hakika umeongea ukweli mtupu sijui kwanini viumbe hawa wanaroho mbaya kiasi hicho
 
Heaven Sent Say it no more mam, lazima sote tujifunze misingi mizuri ya kufanya judgments ama sivyo tutabomoa vitu vingi badala ya kujenga, Hii mada ni ya kitambo kidogo, hope umechelewa kufika kama kawaida yako 😀😀. Missing you more....
 
Kiufupi tu kaeni mkijua hakuna kiumbe cha kike kinacho mpenda mtoto wa mwanamke mwenzie iwe mbuzi kuku ndio usisemee... Yaaani wanyama wote
 
Kama ni Mimi kwa mfano,mke wangu Ana mtoto wake kazaa huko namlea vizuri halafu yeye amzingue mwanangu,aiseeeee ! Namtimua siku hiyo hiyo Bora nibaki na mwanangu,sitaki ujinga mimi,
Siwezi kumuacha mwanangu kwa Bibi yake kiss namuhofia mke wangu wakati Mimi ndo fadher house?
Namuambia kabisa,ukikaa vizuri na huyu mtoto ndo Visa yako ya kuishi hapa utaendelea kurenew,ukikaa nae vibaya happy ndo mwisho na nampa taarifa hiyo live mbele ya watoto wake na wangu, sitaki uficho.
 
Ukitaka kuwalea watoto wako usioe. Tafuta housegirl alee watoto wako kama unataka kuoa tafuta nyumba nyingine ukae na huyo mwanamke tofauti na hapo watoto wako watateseka sana. Hawa wanawake ni wazuri sana kuwaona yaani hata ukimuoa mgumba bado watoto wako watateseka sana. Mwanaume anaweza kuishi na mtoto siyo wake vizuri bila matatizo yoyote ila kwa mwanamke kati ya wanawake 200,000 unaweza kumpata mmoja tu naye ni mcha Mungu.
Wanawake wanaojifanya wacha Mungu hao hua ni hatari sana mkuu hao wanakuwaga na roho mbaya sana yani katika maisha usikosee mahesabu na kumzalisha mwanamke halafu usije muoa huyo utake kuoa mwanamke mwingine..
 
Zote ni risk sababu huyo mtoto pia yupo kwa baba wa kambo what if baba wa kambo kamfanya mke anamkula mkewe akiwa hayupo au kama wa kiume anaweza kuwa anamuingilia mlango wa uani yani anamlawiti.
Solution ni kuacha kuzaa zaa hovyo kama paka kuwepo na familia ya baba, mama na watoto haikuwa kwa bahati mbaya.
Kuna mdada nilikua nadate nae alinichana kabisa yani kama una mtoto niambie tuachane mapema sitaki dhambi maana haitakaa nimpende nikamwambia sina.
Kwa ninavyojifahamu huyo mwanamke ningemuacha hata kama sina mtoto...
 
Kama ni Mimi kwa mfano,mke wangu Ana mtoto wake kazaa huko namlea vizuri halafu yeye amzingue mwanangu,aiseeeee ! Namtimua siku hiyo hiyo Bora nibaki na mwanangu,sitaki ujinga mimi,
Siwezi kumuacha mwanangu kwa Bibi yake kiss namuhofia mke wangu wakati Mimi ndo fadher house?
Namuambia kabisa,ukikaa vizuri na huyu mtoto ndo Visa yako ya kuishi hapa utaendelea kurenew,ukikaa nae vibaya happy ndo mwisho na nampa taarifa hiyo live mbele ya watoto wake na wangu, sitaki uficho.
Mzee ukija kutoa hio sentensi mtoto wako atateseka dunia nzima
 
Kunao wanawake wengi wazuri ambao wamelea watoto wasio wao. Si sahihi kujumlisha wanawake wote eti ni makatili wasioweza kuishi na watoto wa kambo. Kunao akina mama walio kwenye viwango vya pekee wasiobagua wana waliozaliwa na wake wengine tofauti na wao.Mgalla muue lakini haki mpe.
 
Back
Top Bottom